Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana? Tumshukuru Mungu kwa maana Fadhili zake ni za milele.. Asante Mungu Baba kwa kutuchagua sisi na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..si kwamba sisi ni wema sana,kwamba ni wenyenguvu/utashi,si kwamba sisi ni bora mno, si kwamba wengine ni wakosaji sana hapana Baba wa Mbinguni ni kwa Neema/Rehema yako tuu..
Tazama Jana imepita Baba Leo ni siku mpya Kesho ni siku nyingine Yahweh...!!Tunakuja mbelezako tukijinyenyekeza na Tunaomba ukabariki maisha yetu Baba..Maisha yetu yapo mikononi mwako Jehovah..!!Wewe unatujua kuliko tunavyojijua Baba wewe ni Mungu wetu,Muumba wetu,wewe ni Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Wewe Ndimi Mwenyezi-Mungu ujapokuwa nasi hakuna linaloshindikana,Wewe ni kila kitu hakuna kama wewe na hatokuwepo..Wewe ni Alfa na Omega..!!! Tunaomba utubariki Tuingiapo/tutokapo,vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!! Ukabariki kazi zetu,Biashara,Masomo na ukaguse na kutakasa vyote tunavyo enda kutumia,Ukatutakase Miili yetu na Akili zetu Baba wa Mbinguni na Damu ya mwanao mpendwa Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Aliteseka na kumwaga damu ili sisi tupate kupona.. Tunakwenda kinyume na Mwovu, Nguvu za Giza,Nguvu za Mizimu,Nguvu za mapepo,Nguvu za Mpinga Kristo Zishindwe katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti...
“Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji. “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!” Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo.
Tunakuja mbelezako Baba tukiomba na utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..kwakujua/kutojua,kwakunena/kwakutenda na kwakuwaza..
Baba ukatupe Neema ya sisi kuweza kuwasamehe wote waliotukosea.
Mfalme wa Amani tunaomba ukawaponye na ukawaguse wenzetu walio wagonjwa,wasiojiweza,wafiwa ukawe mfariji wao,wenye shida/tabu,waliokatika vifungo mbalimbali baba ukawaponye kimwili na kiroho..wanaopitia Magumu/majaribu..Baba Yatima na wajane na walidhurumiwa haki zao zikapatikane.. Jehovah..Yahweh..!!Mfalme wa Amani..Tunayaweka haya yote mikononi mwako..Sifa na Utukufu ni wako,Tukishukuru na kuamini wewe ni Mungu wetu..Jana Leo na hata milele na ilele..
Amina..!!
Mimi Yohane nayaandikia makanisa saba yaliyoko Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi, na kutoka kwa Yesu Kristo, shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka kwa wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda, na kwa damu yake ametufungua kutoka vifungo vya dhambi zetu, akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina. Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Nguvu , aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Mungu aendelee kuwabariki.
|