Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu na kumsifu Daima..
Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote! Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe! Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu. Yeye ndiye aliyetuumba, nasi ni mali yake; sisi ni watu wake, ni kondoo wa malisho yake. Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani, ingieni katika nyua zake kwa sifa. Mshukuruni na kulisifu jina lake. Mwenyezi-Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele, na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Tunakushuru eeh Mungu wetu,Baba yetu,Mwamba wetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi..Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo.. Asante kwa yote uliyotutendea/unayoendelea kututendea,Imani na Tumaini tunaweka kwako..
Asante kwa kutuchagua tena kuendelea na kutupa kibali cha kuiona siku hii Baba wa Mbingu..Neema/Rehema zako zatutosha Mwenyezi-Mungu,Faraja yako inatutosha Baba,Upendo wako wadumu milele,Hakuna wa kufanana nawe Jehovah..!! Hakuna na hatokuwepo Yahweh..!! Mungu usiye sinzia wala kulala..Mungu unayejibu na kutenda,Mungu unayebariki,Mungu uponyae..wewe watosha Baba wa Mbinguni...wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho Yahweh..!! Mfalme wa Amani tuyaweka maisha yetu mikononi mwako..Baba ukatubariki tuingiapo/tutokapo,vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri na tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Jehovah..! Mfalme wa Amani ukabariki Kazi zetu,Bishara zetu,Masomo na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba ukavitakase kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo..
Baba ukatutakase Miili yetu na Akili zetu..Ukatuokoe na yule Mwovu na kazi zake zote..Ukatufunike na Damu ya mwanao Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Yeye aliteseka pale msalabani ili sisi tupate kupona..
Yahweh..!! Tazama wenye Shida/Tabu, wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,waliokuwa vifungoni,wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao.. Baba tunaomba kwa mkono wako ukawaguse na kuwaponya..wapate kupona kimwili na kiroho,,Baba ukaonekane kwenye shida zao.. Baba tunakuja mbele zako kwa kujinyenyekeza na tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Jehovah..! kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutokujua.. Baba tunaomba nasi utupe Neema yakuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Ee Mwenyezi-Mungu, utusikie; utusamehe ee Mwenyezi-Mungu. Ee Mwenyezi-Mungu, kwa hisani yako utusikie na kuchukua hatua, wala usikawie, ee Mungu wangu, kwa ajili ya mji huu na watu hawa wanaoitwa kwa jina lako!
Asante Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako,Tunakusifu na kukushukuru katika yote..Tukiamini ya kwamba wewe ni Mungu wetu na Mwokozi wetu.. Amina..!!
Muwe na wakati mwema wote
mliopita hapa na Mungu aendelee kuonekana Maishani mwenu.
|