Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 1 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..5.


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..


Haleluyah..!Haleluyah..!Haleluyah!!
Mungu wetu yu mwema sana na Fadhili zake za dumu milele..

Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Baba yetu,Mungu wetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo ni mali yako,Mfalme wa Amani,Muweza wa Yote,Baba wa Yatima,Mume wa Wajane,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Yahweh..,Jehovah, Eli Shaddai, Wewe Ndimi Mwenyezi- Mungu,wewe ndimi Mungu wetu..Unatosha Baba wa Mbinguni, Hakuna kama wewe..!!
Leo ni siku mpya Baba wa Mbinguni Tazama Jana imepita na kesho ni siku nyingine..!
Tazama tumemaliza vyema mwezi wa 5 na tunaanza mwezi huu mpya wa 6 Jehovah..!
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako..

Asante kwa ulinzi wako usiku wote na siku zote umekuwa nasi ..
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha  kuendelea kuiona tena siku hii/Mwezi huu..
Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..

Tunaomba utusamehe Dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kusameheana na kuchukuliana..

Jehovah utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..
Utufunike kwa Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Roho Mtakatifu atuongoze kwenye kunena/kutenda na tukawe na kiasi..

Jehovah..Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo yeye alikufa ili sisi tupate kupona..
Baba wa Mbinguni ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe Neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Ukatubariki tuingiapo/tutokappo na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..


Mfalme wa Amani tunapoanza mwezi huu Baba wa Mbinguni uwe nasi na ukatubariki na kutufungulia milango ya Neema na Baraka,Tusipungukiwe mahitaji yetu na ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Ukatuongoze,tupate kutambua/kujitambua,ukatupe Amani ya moyo,Furaha,Utuwema,Upendo wa kweli,Upole kiasi,Unyenyekevu,msukumo/shauku ya kujua zaidi/kujifunza zaidi Neno lako na likawe kinga,likawe mwanga,likawe nguzo,lika stawi maishani mwetu,likatufae sisi na wengine pia..
Jehovah ukaonekane kwenye maisha yetu na ukatufanye chombo kipya na tukatumike sawaswa na mapenzi yako..

Furaha ya kweli

(Luka 6:20-23)
“Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa. Heri walio na huruma, maana watahurumiwa. Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu. Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu. Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao. “Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
Ukawaguse na mkono wako wenye nguvu na kuwaponya wote wanaopitia magumu/majaribu/mapito mbalimbali..Ukawafungue waliokatika vifungo mbalimbali na ukawaponye kiroho na kimwili pia..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako tuliyoyanena na tusiyoyanena
Baba unajua mioyo yetu na unatujua kuliko tunavyojijua..


Tunakushukuru na kukuabudu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..

Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana..
wote mnaopitia hapa..sina Neno zuri kwenu zaidi ya kuwaombea

na Mungu aendelee kuwabariki..
Nasema..Asanteni sana sana ..
Nawapenda mno.


Sadaka nyingine za kuondoa dhambi

1“Kama mtu yeyote akitakiwa kutoa ushahidi kwenye baraza juu ya jambo aliloona au kulisikia naye akakataa kusema kitu, basi, huo ni uovu na atauwajibikia. 2Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia. 3Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia. 4Au, kama mtu akiapa kufanya chochote kile, chema au kibaya, kama wafanyavyo watu bila kufikiri, atakapojua atakuwa na hatia. 5Basi, mtu akiwa na hatia kuhusu mambo hayo lazima akiri dhambi yake aliyotenda 6na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
7“Lakini kama hawezi kutoa mwanakondoo wa sadaka ya kuondoa hatia kwa ajili ya dhambi aliyotenda, basi atamletea Mwenyezi-Mungu hua wawili au makinda mawili ya njiwa: Mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 8Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamtoa mmoja awe sadaka ya kuondoa dhambi kwa kumkongonyoa shingo yake bila kukichopoa kichwa chake. 9Sehemu ya damu yake ataipaka pembeni mwa madhabahu na ile nyingine ataimimina chini kwenye tako la madhabahu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi. 10Kisha atamtoa yule wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa kulingana na maagizo. Kuhani atamfanyia huyo mtu upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
11“Ikiwa hawezi kutoa hua wawili au makinda mawili ya njiwa kama sadaka yake ya kuondoa dhambi aliyotenda, basi, ataleta unga kilo moja. Lakini hatautia mafuta wala ubani kwani ni sadaka ya kuondoa dhambi. 12Atamletea kuhani, naye atachukua unga huo konzi moja na kuuteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho, pamoja na sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi. 13Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho kwa ajili ya dhambi, naye atasamehewa. Unga unaobaki utakuwa wake kuhani kama ifanyikavyo kuhusu sadaka ya nafaka.”

Sadaka za fidia
14Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 15“Kama mtu yeyote akikosa kwa kutenda dhambi bila kujua kuhusu kutotoa vitu vitakatifu anavyotolewa Mwenyezi-Mungu, atamletea kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake. Wewe utapima thamani yake kulingana na kipimo rasmi cha mahali patakatifu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia. 16Zaidi ya hayo, huyo mtu atalipa madhara yote aliyosababisha kuhusu vitu vitakatifu kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake na kumpatia kuhani yote. Basi, kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa huyo kondoo dume aliye sadaka ya kuondoa hatia, naye atasamehewa.
17“Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake. 18Atamletea kuhani kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake akiwa na thamani sawa na ile ya sadaka ya hatia. Na kuhani atamfanyia upatanisho kwa kosa alilofanya, naye atasamehewa. 19Hiyo ni sadaka ya hatia; yeye ana hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu.”

Mambo Ya Walawi5;1-19


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday, 31 May 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..4...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu yeye yu mwema..

Haleluyah..!Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Muweza wa yote,Yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho,Alfa na Omega..!Yahweh..!Jehovah..!Unatosha Baba.. Hakuna kama wewe..!

Tazama Jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya Kesho ni siku nyingine...!!
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako,Umekuwa nasi usiku wote na wakati wote..
Asante kwa kutupa kibali cha kuendelea tena kuiona Leo hii ..

Tunakuja Mbele zako tukijinyenyekeza,Tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
Tunaomba utusamehe pale tupokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni kwa kuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua...
Mungu wetu tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe nasi waliotukosea..
Tunaomba utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..

Tunaomba ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike na Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na kutenda na tukawe na kiasi..


Tunaomba ukabariki kuingia kwetu/kutoka kwetu,Vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..

Ukabariki vilaji/vinywaji,Kazi zetu,Biashara,Masomo na vyote tunavyoenda Kugusa/Kutumia Mfalme wa Amani ukavitakase kwa Damu  ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Ukabariki Ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi utupe Neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Baba wa Mbinguni..


Ukawaguse na mkono wako wenye Nguvu wote wanaopitia Magumu/majaribu Mbalimbali,walio kwenye vifungo mbalimbali na Ukawainue wanyonge na waliodhulumiwa wakapate haki yao..
Ukaonekane Jehovah..!! kwenye shida/tabu zao na wote wanaokulilia ukawafute machozi,wanaokuomba Baba ukawajibu sawasawa na mapenzi yako.
Wapendwa yanini mteseke na mizigo ?
Yanini kuteseka na kuugua rohoni?
Yanini kukata tamaa na kuwa na hofu/mashaka?
Baba anawapenda sana..
Asema..


 Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha...!!


Wakati huo Yesu alisema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafunulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza. “Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anapenda kumfunulia. Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”


Mfalme wa Amani tuyaweka maisha yetu mikononi mwako..Baba wa Mbinguni Tazama watoto wetu wanaondelea na mitihani na wanaojindaa na mitihani ukawabariki na ukawaguse na mkono wako wenye nguvu..wapate kukumbuka na kuelewa yote waliyofundishwa.. wakawe kichwa na si mkia..


Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza, bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
Asante Mungu wetu Baba yetu Tunaweka Ndoa zetu Mikononi mwako Mfalme wa Amani ..Kila mmoja akafuate/kufanya jukumu lake..
Mke na akawe mke kama ulivyoagiza,Mume na akawe Mume kama ulivyoagiza..ukatupe kuelewa na kujtambua katika Nyumba zetu na tufuate Neno lako Mungu wetu na si Maneno ya Binadamu..



Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya heshima mliyo nayo kwa Kristo. Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote. Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. Alifanya hivyo ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. ( Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, maana sisi ni viungo vya mwili wake). “Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.” Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
Kanisa linaanzia Nyumbani ..!
 Hasa wa mama mmhh..tumekuwa na mambo mengi mengi kisingizio Maombi,Mikutano,Makundi,Kusaidiana,kushikamana,sisi tunaosema hivyo ndiyo sisi wakwanza kusahau majukumu yetu..Maombi yooote,Mungu tunayemtafuta saa zooote, Mafundisho tunayopeana kila wakati sijui yanaishia wapi..?

 Msinielewe Vibaya  sipingani na haya mambo ya wamama hapana .. Basi yakazae matunda na tuwe na kiasi ..

Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.

Ee-Mungu Baba tusaidie tuijue kweli yako na tujitambue..
Mungu akinipa kibali cha kuongelea hili ipo siku nitaongea..

Asante Mungu wetu.Tunakushukuru na kukuabudu wewe..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Kwakua Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata milele..
Amina..!!

Asanteni sana kwa wote mnaotembelea hapa..
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea 

sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda sana.



Sadaka kwa ajili ya dhambi zisizokusudiwa
1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waambie watu wa Israeli hivi: Kama mtu ametenda dhambi bila kukusudia, akafanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu, atafanya kama ifuatavyo: 3Ikiwa kuhani ambaye amepakwa mafuta ndiye aliyetenda dhambi hata akawatia watu hatiani, basi huyo atamtolea Mwenyezi-Mungu fahali mchanga asiye na dosari awe sadaka ya kuondoa dhambi. 4Atamleta huyo fahali mchanga kwenye mlango wa hema la mkutano, mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye ataweka mkono wake juu ya kichwa cha fahali huyo na kumchinja mbele ya Mwenyezi-Mungu. 5Huyo kuhani, aliyepakwa mafuta atachukua kiasi cha damu na kuingia nayo ndani ya hema la mkutano. 6Atachovya kidole chake katika damu hiyo na kuirashia mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu upande wa mbele wa pazia la mahali patakatifu. 7Kuhani atachukua sehemu ya damu na kuzipaka pembe za madhabahu ya kufukizia ubani wa harufu nzuri, mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyoko karibu na mlango wa hema la mkutano. 8Kisha atayaondoa mafuta yote ya ng'ombe huyo: Mafuta yanayofunika matumbo, 9figo mbili na mafuta yaliyo juu yake na yale yaliyo kiunoni, na yale yaliyoshikamana na figo na ini; hizi ni sehemu zilezile zinazoondolewa kwa mnyama wa sadaka ya amani. 10Kuhani atazichukua na kuziteketeza juu ya madhabahu ya kuteketezea sadaka. 11Lakini ngozi ya huyo ng'ombe, nyama, kichwa, miguu, matumbo na mavi yake, 12yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
13“Iwapo jumuiya yote nzima ya Israeli imetenda dhambi bila ya kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu 14mara dhambi hiyo itakapojulikana, jumuiya yote itatoa fahali mchanga awe sadaka ya kuondoa dhambi. Watamleta kwenye hema la mkutano. 15Wazee wa jumuiya ya watu wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo fahali, kisha atachinjwa mbele ya Mwenyezi-Mungu. 16Yule kuhani aliyeteuliwa rasmi kwa kupakwa mafuta ataleta sehemu ya damu ya huyo fahali ndani ya hema la mkutano. 17Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza mbele ya pazia mara saba, mbele ya Mwenyezi-Mungu. 18Kisha, sehemu ya damu atazipaka pembe za madhabahu iliyoko katika hema la mkutano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyo karibu na mlango wa hema la mkutano. 19Mafuta yote ya mnyama huyo atayachukua na kuyateketeza kwenye madhabahu. 20Kwa hiyo atamfanya fahali huyu kama alivyomfanya yule mwingine wa sadaka ya kuondoa dhambi. Basi, huyo kuhani atawafanyia watu ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi, nao watasamehewa. 21Kisha atamchukua fahali huyu na kumpeleka nje ya kambi na kumteketeza kwa moto kama alivyomfanya yule mwingine. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi ya jumuiya.
22“Ikiwa mtawala ametenda dhambi bila kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, na hivyo akawa na hatia, 23mara akijulishwa dhambi hiyo aliyotenda, ataleta sadaka yake ya beberu asiye na dosari. 24Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha beberu na kumchinjia mahali wanapochinjia sadaka za kuteketezwa mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi. 25Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka. 26Mafuta yote ya beberu huyo atayateketeza madhabahuni, kama afanyavyo na mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa hiyo kuhani atamfanyia mtawala ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
27 # Taz Hes 15:27-28 “Kama mtu wa kawaida ametenda dhambi bila kukusudia, kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu na hivyo akawa na hatia, 28mara atakapojulishwa kuwa ametenda dhambi, ataleta sadaka ya mbuzi jike asiye na dosari kwa ajili ya kuondoa dhambi aliyotenda. 29Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi huyo wa sadaka ya kuondoa dhambi, na kumchinjia mahali wanapochinjia wanyama wa sadaka za kuteketezwa. 30Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu iliyobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu. 31Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama aondoavyo mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, naye kuhani atayateketeza madhabahuni, na harufu yake nzuri itampendeza Mwenyezi-Mungu. Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.
32“Ikiwa mtu huyo ataleta mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, basi, ataleta mwanakondoo jike asiye na dosari. 33Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mwanakondoo huyo wa sadaka ya kuondoa dhambi, na kumchinjia mahali pale wanapochinjia wanyama wa sadaka za kuteketezwa. 34Kisha kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu. 35Kisha atayaondoa mafuta yote kama aondoavyo mafuta ya mwanakondoo wa sadaka ya amani, na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka zitolewazo kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Naye kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.”

Mambo Ya Walawi4;1-35


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday, 30 May 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..3...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Asante Baba wa mbinguni kwa wema na fadhili zako..
Asante kwa ulinzi wako usiku wote na wakati wote..
Asante kwa kutuamsha salama na wenye Afya..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuina leo hii..
Tunashuka mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah..!

Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Yahweh..!utuepushe na majaribu utuokoe na yule mwovu na kazi zake..
Baba wa Mbinguni ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Mungu wetu ukatamalaki katika nyumba zetu na ukatuatamie na kutubariki katika yote..

Baba wa Mbinguni ukabariki kazi zetu,Biashara,Masomo,vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri,Tuingiapo/tutokapo, tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!

Tazama wenye shida/tabu,wanaopitia magumu/majaribu ,walio kwenye vifungo mbalimbali,Wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao,waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye Hofu/mashaka Baba wa mbinguni ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye na kuwaokoa katika mapito yao, Mfalme wa Amani ukaonekane kwenye mahitaji yao..
Baba wa Mbinguni wapate kupona kimwili na kiroho na ukawape sawasawa na mapenzi yako..

Nyinyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu. Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu. Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu. Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika, hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu nyinyi mmeokolewa. Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni. Ndivyo alivyopenda kuonesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu. Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu. Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu. Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.
Baba wa Mbinguni ukatupe Hekima, Busara katika yote tusiwe watu wakujisifu,kujivuna,kutaka mambo yetu wenyewe yasiyompendeza Mungu, tusiwe wenye kiburi,dharau,kujiona na wenye chuki na kisasi..
tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Tunashukuru na kuyaweka haya yote mikononi mwako..
Tukiamini wewe ni Mungu wetu..
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe..
Amina..!
Asanteni sana wote mnaopitia Hapa..
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea..
msipungukiwe na mahitaji yenu..
Mungu wetu yu mwema sana
na akawaguse na mkono wake wenye nguvu..
Nawapenda.



Sadaka za muungano

1“Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu. 2Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mlangoni mwa hema la mkutano. Hao makuhani wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote. 3Mafuta yote yanayofunika na yaliyo juu ya matumbo ya mnyama wa sadaka hiyo ya amani atayateketeza kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. 4Atatoa pia zile figo mbili na mafuta yake pamoja na ile sehemu bora ya ini. 5Wazawa wa Aroni wataiteketeza madhabahuni pamoja na sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni; hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
6“Kama sadaka hiyo ya kufanya amani unayomtolea Mwenyezi-Mungu ni kutoka kundi la kondoo au mbuzi, basi achaguliwe dume au jike asiye na dosari. 7Kama mtu atatoa mwanakondoo kuwa sadaka yake, basi, atamtolea mbele ya Mwenyezi-Mungu, 8akiweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mbele ya hema la mkutano. Makuhani wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote. 9Kisha, kutoka katika sadaka hiyo ya amani anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atamtolea sehemu zifuatazo: Mafuta yake, mkia wenye mafuta mzima uliokatwa karibu kabisa na uti wa mgongo pamoja na mafuta yote yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo kwenye matumbo, 10zile figo mbili na mafuta yake pamoja na sehemu bora ya ini. 11Kuhani ataviteketeza hivyo vyote juu ya madhabahu kama chakula anachotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.
12“Kama sadaka yake ni mbuzi, basi, atamtolea mbele ya Mwenyezi-Mungu 13akiweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mbele ya hema la mkutano. Wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote. 14Kisha, mafuta yote yanayofunika matumbo 15na zile figo mbili na mafuta yake pamoja na sehemu bora ya ini, atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto. 16Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula kinachotolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto kutoa harufu ya kumpendeza Mungu. Mafuta yote ni ya Mwenyezi-Mungu. 17Ndiyo maana siku zote na mahali popote mtakapokaa ni lazima kushika kanuni hii. Kamwe msile mafuta wala damu.”

Mambo Ya Walawi 3;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday, 29 May 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..2...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na Fadhili zake..
Asante Baba wa Mbinguni, Mungu wetu, Baba yetu, Muumba wetu,Muumba wa Mbingu na Nchi na Vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..


Asante Kwa ulinzi wako na kutuamsha salama..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku/wiki hii..


Tazama Jana imepita Baba Leo ni Siku mpya na Kesho ni siku Nyingine Jehovah..
Tunakuja Mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Yahweh..!
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwa kuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Tunaomba  Mungu wetu nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Roho mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na kutenda Baba wa Mbinguni tukawe na kiasi..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu Jehovah na tupate kutambua/kujitambua..
Ukatuepushe na hila zote za Mwovu na kazi zake..
Utuokoe na kutufunika na Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..

Mfalme wa Amani tunaiweka Siku/wiki hii na maisha yetu mikononi mwako..Tunaomba ukaibariki na kutubariki katika yote tunayoenda kutenda/kufanya tukafanye sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe Neema ya kuwabariki  wenye kuhitaji..
Ukatuongoze ee Mungu wetu na Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Tazama wenye shida/Tabu Wagonjwa,Wafiwa ukawe mfariji wao,waliokata tamaa,Waliokataliwa,wenye hofu/mashaka na wote waliokatika vifungo mbalimbali Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu ukawaponyae na kuwaokoa,wakapate kupona kimwili na kiroho pia..Baba ukaonekane kwenye magumu/mapito yao..


Baba wa Mbinguni ukatupe Hekima, Busara na ufahamu katika kuongoza Familia zetu,Nyumba zetu na tukaambatane na walio wako..
Rafiki mwema anatoka kwako,Jirani mwema anayetoka kwako..yeyote anayetukaribia kwenye maisha yetu Baba wa mbinguni tunaomba awe wako.. sisi hukaribisha kila mtu Baba lakini ukatupe macho ya kuona ukatupe Neema ya kutambua na kujitambua katika mahusiano yetu..

Wapendwa tumkabidhi Mungu mahusiano/familia  zetu,Si wote wanaopenda kuona watoto wako wanafanya vyema,si kila rafiki anapenda kuona nyumba yako inasimama, si kila jirani niwakuombana chumvi,si kila anayekuchekea anacheka kutoka moyoni..si kila anayesema Mungu/Bwana na anamoyo safi..


[Mama yangu alikuwa anatuambia Nyumba njema si mlango..]

[waswahili wa leo wanasema Jiongeze...Hahahaha..!]

Kuishi katika mwanga

Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana nyinyi ni watoto wake wapenzi. Upendo uongoze maisha yenu kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama tambiko yenye harufu nzuri na sadaka impendezayo Mungu. Kwa vile nyinyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu. Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa. Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu. Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii. Basi, msishirikiane nao. Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga, maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana. Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni. Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. Lakini kila kitu kikifichuliwa na mwanga, ukweli wake hudhihirishwa; na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: “Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangaza.” Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima. Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana. Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Asante Mungu wetu..tunayaweka haya yote mikononi mwako..
kwakua Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu Hata Milele..
Amina..!!
Asanteni sana wote mnaopita hapa..
Mungu akawabariki katika yote..
Akawape sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.


Sadaka za nafaka
1“Mtu yeyote akileta sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi-Mungu, sadaka hiyo iwe ya unga laini. Atautia mafuta na ubani. 2Kisha, atawaletea hao makuhani wa ukoo wa Aroni. Atachukua konzi moja ya unga huo laini wenye mafuta na ubani na kumpelekea kuhani mmojawapo ambaye atauteketeza juu ya madhabahu uwe sadaka ya ukumbusho kwa Mwenyezi-Mungu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. 3Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.
4“Kama mtu anamtolea Mungu sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, hiyo itakuwa ya mikate isiyotiwa chachu ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni, au ya mikate myembamba isiyo na chachu na isiyopakwa mafuta. 5Iwapo sadaka unayotoa ni ya mkate uliookwa kwenye kikaango, hiyo itakuwa ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni lakini bila chachu. 6Mikate hiyo itakatwakatwa na kumiminiwa mafuta; hiyo ni sadaka ya nafaka. 7Kama sadaka unayotoa ni ya mikate iliyopikwa katika sufuria, hiyo itakuwa ya unga laini na imetiwa mafuta. 8Utaleta sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivyo mbele ya Mwenyezi-Mungu; na kuhani ataipeleka kwenye madhabahu. 9Kuhani atachukua sehemu ya sadaka hiyo ikiwa ni sadaka ya ukumbusho na kuiteketeza juu ya madhabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. 10Sehemu inayobaki ya sadaka ya nafaka, ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka inayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.
11“Sadaka yoyote ya nafaka utakayomletea Mwenyezi-Mungu ni lazima iwe imetengenezwa bila chachu; kwani hakuna ruhusa kamwe kutumia chachu wala asali katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. 12Unaweza kumletea Mwenyezi-Mungu mazao yako ya kwanza kama sadaka. Lakini hayo hayatatolewa madhabahuni kama harufu ya kumpendeza. 13Utakoleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Kamwe usiache kuweka chumvi katika sadaka yako ya nafaka, kwani chumvi ni ishara ya agano alilofanya Mungu pamoja nanyi.
14“Ukimtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mazao yako ya kwanza utaitoa hiyo ikiwa imechomwa katika masuke yake, au utaitoa katika mikate ya kuokwa iliyotengenezwa kwa ngano iliyosagwa. 15Utaitia mafuta na kuweka ubani; hiyo ni sadaka ya nafaka. 16Kuhani ataiteketeza sehemu ya sadaka hiyo ya nafaka iliyopondwa na mafuta pamoja na ubani wake wote, iwe sadaka ya ukumbusho; hiyo ni sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Mambo Ya Walawi 2;1-16


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday, 28 May 2017

Natumaini Jumapili Ilikuwa Njema/inaendelea Vyema;Burudani-Miriam Lukindo Mauki - Hakuna Wa Kubadili Na Eunice Njeri - Nani Kama Wewe ..!!




Ni Nani kama wewe Nakuinua Mungu wangu Leo Nani kama wewe Nakupendaaa..!!
Miguuni pako Nakuinamia Bwana  Heshima na utukufu Baba nakupa Yesu..!!Nimekuja nikuinue Nimekuja nikupendeeh Miguuni pako Nakupendaaa..!!

Haleluyahh.! Mungu wetu  yu mwema sana. Haijalishi nini unapitia,Haijalishi umejikwaaje..!Inuka na uendelee na safari   hakuna mwingine tena kama Mungu..

Wapendwa/Waungwana Natumaini mlikuwa na Jumapili Njema/mnaendelea vyema na Jumapili hii..
Mungu aendelee kuwabariki na kuwapa sawasawa na mapenzi yake..
Amina ooh Amina oohh Amina Mileleeeh..!!
1Mungu wenu asema:
“Wafarijini watu wangu,
nendeni mkawafariji.

Neno la Leo;Isaya 40:1-31 



Tumaini la kuponywa katika Yerusalemu
1Mungu wenu asema:
“Wafarijini watu wangu,
nendeni mkawafariji.
2Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole,
waambieni kwamba utumwa wao umekwisha,
wamesamehewa uovu wao.
Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufu
kwa sababu ya dhambi zao zote.”
3 40:3 Taz Mat 3:3; Marko 1:3; Yoh 1:23 Sauti ya mtu anaita jangwani:
“Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia,
nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu. 40:3-5 Taz Luka 3:4-6
4Kila bonde litasawazishwa,
kila mlima na kilima vitashushwa;
ardhi isiyo sawa itafanywa sawa,
mahali pa kuparuza patalainishwa.
5Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa,
na watu wote pamoja watauona.
Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”
6 40:6-8 Taz Yak 1:10-11; 1Pet 1:24-25 Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!”
Nami nikauliza, “Nitangaze nini?”
Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani;
uthabiti wao ni kama ua la shambani.
7Majani hunyauka na ua hufifia,
Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake.
Hakika binadamu ni kama majani.
8Majani hunyauka na ua hufifia,
lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”
9Nenda juu ya mlima mrefu,
ewe Siyoni, ukatangaze habari njema.
Paza sauti yako kwa nguvu,
ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema.
paza sauti yako bila kuogopa.
Iambie miji ya Yuda:
“Mungu wenu anakuja.”
10 40:10 Taz Isa 62:11; Ufu 22:12 Bwana Mungu anakuja na nguvu,
kwa mkono wake anatawala.
Zawadi yake iko pamoja naye,
na tuzo lake analo.
11 40:11 Taz Eze 34:15; Yoh 10:11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji,
atawakusanya wanakondoo mikononi mwake,
atawabeba kifuani pake,
na kondoo wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Bwana ameshakubali hakuna wakubadili..!!
 Ameshasema ndiyo Leo hakuna wa kubadili
Yeye ni Bwana wa Ma Bwana Hakuna wakubadili...!
Yeye ni Mwamba wa miamba hakuna wa Kubalidili..!!


Mungu wa Israeli hana kifani
12Nani awezaye kupima maji ya bahari kwa konzi yake,
kuzipima mbingu kwa mikono yake?
Nani awezaye kuutia udongo wa dunia kikombeni;
kuipima milima kwa mizani
au vilima kwa kipimo cha uzani?
13 40:13 Taz Rom 11:34; 1Kor 2:16 Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu,
au kuwa mshauri wake na kumfunza?
14Mwenyezi-Mungu alimtaka nani shauri,
ndipo akapata kuwa mwenye ujuzi?
Nani aliyemfunza njia za haki?
Nani aliyemfundisha maarifa,
na kumwonesha namna ya kuwa na akili?
15Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo,
ni kama vumbi juu ya mizani.
Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
16Kuni zote za Lebanoni
na wanyama wake wote
havitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.
17Mataifa yote si kitu mbele yake;
kwake ni vitu duni kabisa na batili.
18 40:18-19 Taz Mate 17:29 Mtamlinganisha Mungu na nini basi,
au ni kitu gani cha kumfananisha naye?
19Je, anafanana na kinyago?
Hicho, fundi hukichonga,
mfua dhahabu akakipaka dhahabu,
na kukitengenezea minyororo ya fedha!
20Au ni sanamu ya mti mgumu?
Hiyo ni ukuni mtu anaochagua,
akamtafuta fundi stadi,
naye akamchongea sanamu imara!
21Je, nyinyi bado hamjui?
Je, hamjapata kusikia?
Je, hamkuambiwa tangu mwanzo?
Je, hamjafahamu mwanzo wa dunia?
22Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu;
kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi!
Yeye amezitandaza mbingu kama pazia,
na kuzikunjua kama hema la kuishi.
23Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu,
watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu.
24Mara tu wanaposimikwa na kuanza kuota,
hata kabla hawajatoa mizizi kama miti udongoni,
Mwenyezi-Mungu akiwapulizia hunyauka,
kimbunga huwapeperusha kama makapi!
25Mungu Mtakatifu auliza hivi:
“Nani basi, mtakayemlinganisha nami?
Je, kuna mtu aliye kama mimi?”
26Inueni macho yenu juu mbinguni!
Je, ni nani aliyeziumba nyota hizo?
Ni yule aziongozaye kama jeshi lake,
anayeijua idadi yake yote,
aziitaye kila moja kwa jina lake.
Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi,
hakuna hata moja inayokosekana.
27Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo,
kwa nini mnalalamika na kusema:
“Mwenyezi-Mungu hatujali sisi!
Mungu wetu hajali haki yetu!”
28Je, nyinyi bado hamjui?
Je, hamjapata kusikia?
Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele;
yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani.
Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu.
Maarifa yake hayachunguziki.
29Yeye huwapa uwezo walio hafifu,
wanyonge huwapa nguvu.
30Hata vijana watafifia na kulegea;
naam, wataanguka kwa uchovu.
31Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu,
watapata nguvu mpya.
Watapanda juu kwa mabawa kama tai;
watakimbia bila kuchoka;
watatembea bila kulegea.







"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Friday, 26 May 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..1.

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Haleluyahh..!!Mungu wetu yu mwema sana..Yeye anaweza yote,Yeye ni Mungu wetu na Baba yetu, Yeye ni Mwanzo na Yeye ni Mwisho,Yeye atosha..!!


Ni siku nyingine tena Mungu ametupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Si kwamba sisi ni wema sana zaidi ya wengine waliotangulia/fariki sasa hivi, usiku au walio hoi vitandani kwa Magonjwa mbalimbali..
Wengine hawawezi hata kutamka Neno la Mungu wala kuomba au Kutubu..
Tumempa nini Mungu ?
Si kwanguvu zetu wala uwezo wetu..ni kwa Neema/Rehema zake Mungu wetu..
Basi Wapendwa/Waungwana tuitumie nafasi hii vizuri na Tumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kwetu..
Asante Mungu wetu Babayetu,Muumba wetu,Muumba wa Mbingu na Nchi, Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Asante kwa ulinzi wako usiku wote na wakati wote umekuwa nasi Jehovah..
Asante kwa kutuchagua tena kuendelea na kuwa hai na wenye Afya..


Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni tukijinyenyekeza tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni..Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika kunena na kutenda Baba tukawe na kiasi..


Baba wa Mbinguni utuepushe na Majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..

Mfalme wa Amani tunaiweka siku hii na maisha yetu mikononi mwako..
Baba ukatubariki katika yote tunayoenda kufanya,Baba tusipungukiwe na mahitaji yetu..lakini utupe sawasawa na mapezni yako..

Asante Mungu wetu kwa kuanza Neno hili[Kitabu hiki cha Walawi]
Mungu wetu ukatuongoze na tukapate  kulielewa Neno hili..Baba wa mbinguni tukapate kukuona na kusikia na  yote uliyoyaweka humu yakawe Faida na Tukapande Mbegu  nzuri kwetu na kwa wengine..
Tukapate msukumo/Shauku zaidi  ya kutaka kukujua zaidi..
Nasi tukalitumie vyema Neno Lako Mungu wetu..Sifa na utukufu
tunakurudishia wewe Baba wa Mbinguni..



Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.


Maana, kama Habari Njema tunayohubiri imefichika, imefichika tu kwa wale wanaopotea. Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu. Maana hatujitangazi sisi wenyewe, ila tunamhubiri Yesu Kristo aliye Bwana, sisi wenyewe tukiwa watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Mungu ambaye alisema, “Mwanga na uangaze kutoka gizani,” ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa Kristo. Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi wenyewe. Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa; twateseka, lakini hatuachwi bila msaada; na ingawa tumeangushwa chini, hatukuangamizwa. Kila wakati tumekuwa tukichukua mwilini mwetu kifo cha Kristo, ili uhai wake Yesu pia udhihirike katika miili yetu. Naam, muda tuishipo tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uhai wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa. Hii ina maana kwamba ndani yetu kifo kinafanya kazi, lakini ndani yenu uhai unafanya kazi. Maandiko Matakatifu yasema: “Niliamini, ndiyo maana nilinena.” Nasi pia, tukiwa na moyo huohuo wa imani, tunaamini, na kwa sababu hiyo twanena. Tunajua kwamba yule aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuweka mbele yake pamoja nanyi. Yote haya ni kwa faida yenu, hata neema ya Mungu inapowafikia watu wengi zaidi na zaidi, shukrani nazo ziongezeke zaidi, kwa utukufu wa Mungu.
Tunayaweka haya yote mikononi mwako kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na utukufu hata milele..
Amina..!
Asanteni sana wote kwakutembela hapa..
Mungu aendele kuwabariki katika yote..
Nawapenda.

Sadaka za kuteketezwa
1Mwenyezi-Mungu alimwita Mose na kuongea naye katika hema la mkutano, akamwambia, 2“Waambie Waisraeli kwamba kama mtu anapenda kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mnyama, mnyama huyo atamchagua kutoka kundi lake la ng'ombe, kondoo au mbuzi.
3“Kama sadaka anayotoa mtu ni ya kuteketezwa, atamchagua mnyama dume asiye na dosari kutoka kundi lake, atamtolea mbele ya mlango wa hema la mkutano ili apate fadhili ya Mwenyezi-Mungu; 4ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka ya kuteketezwa, ambayo itakubaliwa kwa ajili ya kumfanyia huyo mtu upatanisho. 5Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote. 6Huyo mtu atamchuna huyo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kumkata vipandevipande. 7Hao makuhani wazawa wa Aroni watazipanga kuni juu ya madhabahu na kuwasha moto. 8Kisha makuhani hao watachukua vile vipande vya nyama, kichwa na mafuta, na kuviweka juu ya kuni juu ya madhabahu. 9Lakini matumbo na miguu ya mnyama huyo mtu ataviosha kwa maji. Kuhani ataiteketeza sadaka yote juu ya madhabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
10“Kama sadaka yake ya kuteketezwa ataitoa katika kundi la kondoo au mbuzi, basi, atachagua dume asiye na dosari. 11Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu, mbele ya Mwenyezi-Mungu, hao makuhani, wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu pande zake zote. 12Kisha huyo mtu atamkata vipandevipande, akivitenga kichwa pamoja na mafuta yake, na kuhani ataviweka kwenye moto juu ya madhabahu. 13Lakini matumbo na miguu yake ataviosha kwa maji. Kuhani ataiteketeza yote juu ya madhabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
14“Ikiwa anamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa ya ndege, basi, ataleta sadaka yake ya hua au kinda la njiwa. 15Kuhani atamleta ndege huyo kwenye madhabahu, atamkongonyoa kichwa chake na kukiteketeza juu ya madhabahu. Damu yake itanyunyiziwa ubavuni mwa madhabahu. 16Kibofu chake pamoja na uchafu wake ataviondoa na kutupa upande wa mashariki wa madhabahu ambako majivu huwekwa. 17Atamshika mabawa na kumpasua, lakini asimkate vipande viwili. Kisha, kuhani atamteketeza kwenye madhabahu, juu ya kuni. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.”

Mambo Ya Walawi 1;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday, 25 May 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Kutoka 40- Mwisho wa kitabu cha Kutoka...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu wetu....

Mungu wetu, Baba yetu, Muumba wetu, Muumba Mbingu na Nchi na Vyote vilivyomo ni mali yako..Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Yahweh.!Jehovah..!El shaddai..!Muweza wa yote, Alfa na Omega,Wewe ni Mwanzo na wewe ni mwisho,Hakuna kama wewe..!!


Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako.
Asante kwa ulinzi wako na kutuamsha salama..

Asante kwakutuchagua tena  na umetupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Si kwa nguvu zetu wala Akili zetu,si kwamba sisi ni wema sana,si kwamba sisi wazuri mno..hapana ni kwa Neema/Rehema zako sisi kuiona leo hii...
Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,kujishusha na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani ..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwa kuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua,kutojua..
Baba wa mbinguni tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Utuepushe na majaribu Baba wa mbinguni na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Mungu Baba tunaomba ukatutakase Miili yetu na Akili zetu tupate kutambua na kujitambua..

Tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo,vyombo vya usafiri, tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..Mungu wetu ukabariki Kazi zetu,Biashara,Masomo,vilaji/vinywaji na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Mfalme wa Amani ukavitakase kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..

Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu na kuwaponya wote wanaopitia majaribu mbalimbali,shida/tabu,wafiwa ukawe mfariji wao,wagonjwa na wote walio katika vifungo mbalimbali Baba ukawafungue na kuwaokoa, wakapate kupona kimwili na kiroho pia,Baba ukaonekane kwenye shida zao wote wanaokuomba na kukulilia Mungu wetu ukawafute machozi yao..

Tunakushuru Mungu wetu kwa uwezo wako na kutupa Neema hii ya kuweza kusoma Neno Lako Baba wa Mbinguni..

leo tumemaliza kusoma Neno lako kwenye kitabu hiki..Baba wa mbinguni isiwe mwisho na iwe ndiyo mwanzo tukawe na Shauku ya kusoma Neno lako..
 Tunaomba utubariki na kutupa mwangaza zaidi kwenye neno lako..na tusomapo tuondoke na faida na tupate kuelewa na kulitunza likapate kutusaidia sisi na wengine..
Yesu anafafanua mfano wa mpanzi
(Mat 13:18-23; Luka 8:11-15)



Basi, Yesu akawauliza, “Je, nyinyi hamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfano wowote? Mpanzi hupanda neno la Mungu. Watu wengine ni kama walio njiani ambapo neno lilipandwa. Lakini mara tu baada ya kulisikia, Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao. Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu walisikiapo hilo neno hulipokea kwa furaha. Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno, mara wanakata tamaa. Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaosikia hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu, anasa za mali na tamaa za kila namna huwaingia na kulisonga hilo neno, nao hawazai matunda. Lakini wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri. Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea, wakazaa matunda: Wengine thelathini, wengine sitini na wengine mia.”

Mungu wetu ukatupe masikio tusikie na macho ya kuona.. Tukawe kama zile mbegu zilizopandwa kwenye udongo mzuri..
Tukawe barua njema na tukasomeke popote tutakapo pita sawasawa na mapenzi yako...


Mfano wa mbegu inayoota


Yesu akaendelea kusema, “Ufalme wa Mungu ni kama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegu shambani. Usiku hulala, mchana yu macho na wakati huo mbegu zinaota na kukua; yeye hajui inavyofanyika. Udongo wenyewe huiwezesha mimea kukua na kuzaa matunda: Kwanza huchipua jani changa, kisha suke, na mwishowe nafaka ndani ya suke. Nafaka inapoiva, huyo mtu huanza kutumia mundu wake, maana wakati wa mavuno umefika.”
Mungu wetu ukatupe Neema ya kupanda  mbegu njema na tupate kukua kiimani/kiroho na kuvuna yaliyo mema..
 Mungu wetu tunapanda mbegu zako kwa wote wasioamini na wapate kujua wewe Mungu wetu na wema wako..Sifa na utukufu tunakurudishia wewe Daima..


Asante Mungu wetu katika yote.
Tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini wewe ni Mungu wetu na Tumaini letu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na utukufu hata Milele..
Amina..!
Mungu wetu yu mwema sana wapendwa..

kwa uwezo wake na mapenzi yake kwetu leo tumemaliza kitabu hiki..
ninaimani kuna tuliokuwa nao sambamba tangu mwanzo..
Mungu aendele kukupa shauku ya kuendelea kusoma Neno lake..

haijalishi uko busy kiasi gani lakini huwezi kukosa muda kidogo kwa ajili yake yeye Mungu aliyekupa hiyo shughuli ya kukufanya ukawa Busy..
kusikiliza Neno kanisani tuu haitoshi lazima tujibidishe na kujipa msukumo wa kujisomea katika mazingira yoyote tunayopitia tuweke  Mungu kwanza..
Mungu aendelee kutufunulia na kutupa mwanga zaidi..
tunachokipanda kipate kumea/kukua vyema..
Asanteni sana kwakutembelea hapa..
Mungu awabariki na kuwapa Amani ya Moyo..
Nawapenda sana. 

Hema lasimikwa na kuwekwa wakfu

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, utalisimika hema takatifu la mkutano. 3Ndani ya hema hilo utaweka lile sanduku la ushuhuda, kisha weka pazia mbele yake. 4Utaiingiza meza na kupanga vyombo vyake juu. Utaingiza kile kinara pia na kuziweka taa zake juu yake. 5Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia ubani utaiweka mbele ya sanduku la ushuhuda, kisha utatundika pazia kwenye mlango wa hema takatifu. 6Ile madhabahu ya kuteketezea sadaka utaiweka mbele ya mlango wa hema takatifu la mkutano. 7Birika la kutawadhia utaliweka katikati ya hema la mkutano na madhabahu na kulijaza maji. 8Utazungushia ua na kutundika pazia penye lango lake.
9“Kisha, utaliweka wakfu hema takatifu pamoja na vyombo vyake vyote kwa kuvipaka yale mafuta ya kupaka, nalo litakuwa takatifu. 10Halafu, utaiweka wakfu madhabahu ya kuteketezea sadaka na vyombo vyake vyote kwa kuipaka mafuta, nayo itakuwa takatifu kabisa. 11Birika la kutawadhia na tako lake pia utaliweka wakfu kwa namna hiyohiyo.
12“Utamwita Aroni na wanawe waje mlangoni mwa hema la mkutano, kisha uwatawadhe. 13Mvike Aroni yale mavazi matakatifu; utampaka mafuta na kumweka wakfu, ili aweze kunitumikia kama kuhani. 14Waite wanawe na kuwavisha zile kanzu. 15Kisha uwapake mafuta kama ulivyompaka baba yao, ili nao pia wanitumikie kama makuhani. Kupakwa mafuta huku kutawaingiza katika ukuhani wa kudumu katika vizazi vyao vyote.”
16Basi, Mose alitekeleza kikamilifu kabisa maagizo yote ya Mwenyezi-Mungu.
17Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza mwaka wa pili baada ya kutoka Misri, hema la mkutano lilisimikwa. 18Mose aliweka vikalio vyake, akainua mbao zake, akashikamanisha pau zake na kusimamisha nguzo zake. 19Alitandaza pazia juu ya hema takatifu na kuweka kifuniko cha hema juu yake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 20Kisha alichukua vile vibao viwili vya mawe na kuviweka katika lile sanduku. Aliipitisha ile mipiko katika vikonyo vya sanduku na kukiweka kiti cha rehema juu yake. 21Kisha akaliweka lile sanduku la maamuzi ndani ya hema na kutundika pazia, na kwa namna hiyo akalisitiri sanduku la maamuzi, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
22Aliweka meza ndani ya hema la mkutano, upande wa kaskazini, sehemu ya nje ya pazia, 23na juu yake akaipanga mikate iliyotolewa kwa Mwenyezi-Mungu, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 24Alikiweka kinara ndani ya hema la mkutano, upande wa kusini, mkabala wa meza. 25Humo, mbele ya Mwenyezi-Mungu, akaziwasha taa zake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 26Aliiweka ile madhabahu ya dhahabu katika hema, mbele ya pazia, 27na kufukiza ubani wenye harufu nzuri juu yake, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 28Alitundika pazia kwenye mlango wa hema takatifu, 29akaweka hapo langoni mwa hema takatifu madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, akatolea juu yake sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 30Aliliweka birika la kutawadhia katikati ya hema la mkutano na madhabahu, na kutia maji ya kutawadha. 31Mose, Aroni na wanawe, wote walinawa mikono na miguu yao humo. 32Kila walipoingia ndani ya hema au walipokaribia ile madhabahu, walinawa, kama Mose alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 33Mwishowe Mose akatengeneza ua kulizunguka hema takatifu na madhabahu, na kuweka pazia kwenye lango la ua. Hivyo,
Mose akaikamilisha kazi yote.


Wingu juu ya hema la mkutano

34Kisha, lile wingu likalifunika lile hema la mkutano, na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukalijaza hema. 35Mose alishindwa kuingia ndani ya hema la mkutano kwa sababu hilo wingu lilikaa juu yake, na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukajaa humo. 36Katika safari zao zote Waisraeli hawakuanza safari kamwe isipokuwa wakati wingu hilo lilipoinuliwa kutoka juu ya hema. 37Kama wingu hilo halikuinuliwa wao hawakuanza safari; walingoja mpaka wakati lilipoinuliwa. 38Katika safari zao zote, Waisraeli waliweza kuliona lile wingu la Mwenyezi-Mungu juu ya hema wakati wa mchana na ule moto ukiwaka juu yake usiku.

Kutoka40;1-38

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.