Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu,Muumba wa Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo.. Asante kwa ktuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii.. Si kwamba sisi ni wema sana au wazuri mno zaidi ya wengine waliotangulia/fariki leo hii au walio vitandani kwa magonjwa mbalimbali.. wengine wanahitaji hata kuita jina la Mungu lakini hawawezi.. Tumempa nini Mungu?Hapana ni kwa Rehema/Neema zake tuu Mungu wetu..
Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho. Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe. Ndani yake zimefichika hazina zote za hekima na elimu. Basi, nawaambieni, msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa maneno ya uongo hata kama ni ya kuvutia sana. Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
Basi Mungu wetu akatuongoze tukatumie wakati huu vizuri..
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako.. Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu.. Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizoziwaza,tulizozinena,tulizozitenda,kwakujua/kutojua..Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea.. Utuepushe na majaribu,utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote.. Ututakase Miili yetu na Akili zetu,Utufunike kwa Damau ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti.. Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote tupate kutambua na kujitambua na tukawe na kiasi.. Tunayakabidhi maisha yetu mikononi mwako Jehovah...
Maadamu nyinyi mmemkubali Kristo Yesu aliye Bwana, basi, ishini katika muungano naye. Muwe na mizizi ndani yake, mjijenge juu yake na kuwa imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele. Angalieni, basi, mtu asiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wa hekima ya kibinadamu, ambayo chanzo chake ni mafundisho ya mapokeo ya watu na ya pepo watawala, na wala si Kristo mwenyewe! Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu, nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote. Katika kuungana na Kristo nyinyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi. Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo mlifufuliwa pia pamoja naye kwa kuamini katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kwa sababu nyinyi mlikuwa watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa nyinyi uhai pamoja na Kristo. Mungu ametusamehe dhambi zetu zote; alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani. Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake. Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au Sabato. Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye Kristo. Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganyifu za kidunia na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
Ukatubariki na kubariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukafanye sawasawa na mapenzi yako.. ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/kutumia..
Tazama wenye shida/tabu,wamaotaabika na kukata tamaa,wenye hofu/mashaka,waliokatika vifungo mbalimbali,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali.. Mungu wetu ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,Ukawape macho ya kuona na masikio ya kusikia, ukawaonyeshe njia na wakafute sheria na Amri zako..Wakapate kuijua kweli nayo itawaweka huru na kuwaponya kiroho na kimwili..wakapate Ulinzi uliowako na kusimamia Neno lako.. wakajue jinsi ulivyo na kwamba wewe ni muweza wa yote.. Tunakwenda kinyume na roho zote mbaya,nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu,nguvu za mpinga Kristo.. Zishindwe katika Jina lililokuu Jina la Bwana wetu Yesu Kristo...
Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti: “Msishike hiki,” “Msionje kile,” “Msiguse kile!” Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu. Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima kwa namna ya ibada wanayojishurutishia, unyenyekevu, na kuutendea mwili kwa ukali; lakini hayafai chochote kuzuia tamaa za mwili.
Wapendwa Mungu wetu yupo na ni mwema sana.. Tumtafute kwa bidii na kufuata njia zake ili tupate kupona..
Asante Mungu wetu tunayaweka haya yote mikononi mwako.. tukiamini na kushukuru daima.. Sifa na utukufu tunakurudishia wewe Baba wa Mbinguni....
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..!
Asante sana waungwana/wapendwa kwa kuwanami/kunisoma.. Mungu aendelee kuwabariki na msipungukiwe katika mahitaji yenu.. na Mungu akawape sawasawa na mapenzi yake.. Nawapenda. |