Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote.. Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..! Baba wa Mbinguni.. Mungu wetu, Baba yetu, Muumba wetu na Muumba wa Mbingu na Nchi vyote vilivyomo Baba ni mali yako..Hata sisi Baba ni mali yako.. Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..Baba wa Yajatima,Mume wa wajane..Muweza wa yote Alpha na Omega..!! Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Mfalme wa Amani.. Asante kwa ulinzi wako wakati wote.. Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona Leo hii..Si kwa uwezo wetu wala nguvu zetu Mungu Baba ni kwa rehema/neema zako Muumba wetu.. Si kwamba wale waliotangulia/kufariki na wanaougua na wengine wamekata hata kauli hawawezi hata kutamka jina lako Mungu Baba.. kwamba ni wabaya sana au hawafai..hapana ni kwamapenzi yako..
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile. Baba ampenda Mwana, na humwonesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu. Kama vile Baba huwafufua wafu na kuwapa uhai, vivyo hivyo naye Mwana huwapa uhai wale anaopenda. Baba hamhukumu mtu yeyote; shughuli yote ya hukumu amemkabidhi Mwana, ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba ambaye amemtuma. “Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai. Kweli nawaambieni, wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia, wataishi. Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo pia alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai. Tena amempa mamlaka ya kuhukumu kwa sababu yeye ni Mwana wa Mtu. Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake, nao watafufuka: Wale waliotenda mema watafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu watafufuka na kuhukumiwa.
Baba wa Mbinguni tunashuka mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako..Mungu Baba tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua.. Mungu Baba tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..Utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..Mungu Baba ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Yeye aliteseka kwanza ilisisitupate kupona...
Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa, tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema. Basi, sema mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote,Tupate kutambua na kujitambua na tukasimamie Neno lako sheria na Amri zako Mungu wetu na tukawe na kiasi.. Ukatufanye chombo chema na tukatumike kama inavyokupendeza wewe...
Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure. Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa; sasa ndiyo siku ya wokovu! Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuizi chochote. Badala yake, tunajionesha kuwa kweli watumishi wa Mungu kwa kila kitu: Kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu. Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula. Tunajionesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki, kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande. Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli; kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote; kama waliokufa, lakini mwonavyo, sisi ni hai kabisa. Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu. Ndugu Wakorintho, tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetu iko wazi kabisa. Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu nyinyi wenyewe, na si kwa upande wetu. Sasa nasema nanyi kama watoto wangu: Wekeni mioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya.
Baba wa Mbingu tunaomba ukatubariki na kubariki Nyumba zetu/familia na ukabariki Kazi zetu,Biashara,Msomo na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Mungu wetu ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu na ukawaponye wote wanaotaabika,wenyeshida/tabu,waliokatika vifungo mbalimbali na wanaopitia magumu/majaribu yoyote..Mungu wetu ukawepe neema ya kujua na kusimamia Neno lako na wakaijue kweli nayo iwaweke huru. Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu.. Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu Baba.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..!
Mbarikiwe sana wote mnaotembeale/kusoma.. Mungu awenanyi daima.. Nawapenda.
|