Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Mungu wetu Baba yetu,Baba wa Mbinguni,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...!
Mfalme wa Amani Tunakuja mbele zako tukijinyeyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah...
Asante kwa wema na fadhili zako Mungu Baba..Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii...
Asante Mungu wetu kwa ulinzi wako wakati wote..
Utukuzwe Mungu wetu,Uabudiwe milele,Unastahili sifa,Unatosha Jehovah..Hakuna kama wewe..
Mungu wa wajane,Baba wa yatima,Baba wa Upendo,Muweza wa yote..Alfa na Omega..!!
Yahweh..!Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah.. nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Mungu wetu utuepushe katika majaribu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...
Mfalme wa Amani tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Ukabariki Kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu Baba tukatende sawasawa na mapenzi yako..tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kamainavyokupendeza wewe..
Ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na amapenzi yako..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Endeleeni kupendana kindugu. Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua. Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao. Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi. Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.” Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?” Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao. Yesu Kristo ni yuleyule jana, leo na milele. Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata. Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi hawana haki ya kula vitu vyake. Kuhani mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa tambiko kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji. Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake. Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu. Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu. Mtuombee na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima. Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi Waebrania 13:1-19
Tazama wenye shida/tabu,wagonjwa na wenyedhiki,waliokatika vifungo vya yule mwovu..Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye kiroho na kimwili pia..ukawape neema ya kusimamia neno lako na kufuata Amri Sheria zako wakapate kujua jinsi wewe ulivyo na wakawe huru..
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe mwenyezi-Mungu
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe mwenyezi-Mungu
Mungu amemfufua katika wafu Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa Mungu awe nanyi daima..
Nawapenda.
1Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa kisha uniletee fahali saba na kondoo madume saba.”2Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema. Basi, wakatoa juu ya kila madhabahu kafara fahali mmoja na kondoo dume mmoja.3Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima. 4Mungu akakutana naye. Balaamu akamwambia, “Nimetayarisha madhabahu saba na kutoa kafara fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.”
5Mwenyezi-Mungu akampa Balaamu maneno atakayosema na kumwambia arudi kwa Balaki. 6Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama palepale karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, pamoja na maofisa wote wa Moabu.
7Balaamu akamtolea Balaki kauli yake, akasema,
“Balaki amenileta hapa kutoka Aramu,
naam, mfalme wa Moabu amenileta kutoka milima ya mashariki.
‘Njoo uwalaani watu wa Yakobo kwa ajili yangu,
naam, njoo uwalaumu Waisraeli!’
8Nitamlaanije mtu ambaye Mungu hakumlaani?
Nitawalaumuje watu ambao Mwenyezi-Mungu hakuwalaumu?
9Kutoka vilele vya majabali nawaona;
kutoka juu ya milima nawachungulia.
Hilo taifa likaalo peke yake,
lisilojiona kuwa sawa na mataifa mengine.
10Nani awezaye kuwahesabu wingi wa watu wa Yakobo,
au kukisia umati wa Waisraeli?
Nife kifo cha waadilifu,
mwisho wangu na uwe kama wao.”
11Hapo, Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nimekuleta hapa uwalaani adui zangu, lakini badala yake umewabariki!” 12Balaamu akamwambia Balaki, “Sina budi kusema maneno aliyonipa Mwenyezi-Mungu.”
Unabii wa pili wa Balaamu
13Baadaye, Balaki akamwambia Balaamu, “Twende mahali pengine ambapo utaweza kuwaona; hata hivyo utaona tu sehemu yao, hutaweza kuwaona wote. Kisha uwalaani kutoka huko kwa niaba yangu.” 14Basi, Balaki akamchukua Balaamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Hapo akajenga madhabahu saba na kutoa juu ya kila madhabahu kafara ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.
15Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende kule ngambo kukutana na Mwenyezi-Mungu.” 16Mwenyezi-Mungu akakutana na Balaamu, akampa maneno atakayosema, na kumwambia arudi kwa Balaki. 17Basi, Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na maofisa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Mwenyezi-Mungu amekuambia nini?” 18Hapo, Balaamu akamtolea Balaki kauli yake:
“Inuka, Balaki, usikie,
nisikilize ewe mwana wa Sipori.
19Mungu si mtu, aseme uongo,
wala si binadamu, abadili nia yake!
Je, ataahidi kitu na asikifanye,
au kusema kitu asikitimize?
20Tazama, nimepewa amri ya kubariki,
naye amebariki wala siwezi kuitangua.
21Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo,
wala udhia kwa hao wana wa Israeli.
Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao,
Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao,
yeye huzipokea sifa zao za kifalme.
22Mungu aliyewachukua kutoka Misri,
huwapigania kwa nguvu kama za nyati.23:22 kwa nguvu … nyati: Au lina nguvu kama ya nyati.
23Hakika ulozi hauwezi kuwapinga watu wa Yakobo,
wala uchawi dhidi ya watu wa Israeli.
Sasa kuhusu Israeli, watu watasema,
‘Tazameni maajabu aliyotenda Mungu!’
24Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike,
wanasimama kama simba dume.
Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake,
na kunywa damu ya mawindo.”
25Ndipo Balaki akamwambia Balaamu, “Basi, usiwalaani wala usiwabariki kabisa!” 26Lakini Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikukuambia kwamba anachosema Mwenyezi-Mungu ndicho ninachopaswa kufanya?”
27Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo; nitakupeleka mahali pengine. Labda Mungu atakubali uwalaani watu hao kutoka huko kwa ajili yangu.” 28Basi, Balaki akamchukua Balaamu mpaka kwenye kilele cha Mlima Peori, ambapo mtu akisimama anaona jangwani. 29Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa, unitayarishie fahali saba na kondoo madume saba.”30Balaki akafanya kama alivyoambiwa na Balaamu, kisha akatoa juu ya kila madhabahu kafara fahali mmoja na kondoo dume mmoja.
Hesabu23;1-30
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.