Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 15 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..31




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu..
Asante Mungu wetu,Baba yetu na mlinzi wetu..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Muweza wa yote,Mfalme wa Amani..
Utukuzwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Mungu wetu..
Unastahili sifa Baba..Uabudiwe daima Mungu wetu..
Hakuna kama wewe,wewe ni Alfa na Omega..!!
Asante Mungu wetu kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii

Tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya Jehovah na kesho ni siku nyingine Yahweh..!
Tunashuka mbele zako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu
 Baba wa mbinguni utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Yahweh maisha yetu yapo mikononi mwako..
Tunaomba utubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa rehema ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Mungu wetu ukaonekane  popote tupitapo,tunenapo tukanene yaliyoyako..
ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako..
Ukatupe neema ya Hekima,Busara,Upendo,unyenyekevu na kuchukuliana..
Utuepushe na  Hasira,majivuno/kujisifu na kufuata mambo yetu yanayokwenda kinyume nawe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema Mungu wetu nasi tukatumike ipasavyo..

Tazama wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu,walio katika vifungo mbalimbali Mungu Baba tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,wakapate uponyaji wa mwili na roho..
ukawape neema ya kusimamia Neno,Amri na sheria zako nazo zikawaweka huru ..

Baba wa Mbinguni tunawaweka viongozi wetu wote wa Kiroho mikononi mwako..
Mungu wetu ukawatendee na kuwaongoza katika huduma zao..
Ukawainua na pale walipojikwaa wakatambue na kukurudia Mungu,wakafuate matakwa yako Mungu wetu na si yao wenyewe,wakatuongoze katika roho na kweli,ukawaepushe katika roho za Tamaa,Majivuno,Dharau,masimango,masengenyo,ugombanishi na yote yanayokwenda kinyume nawe,wakatende sawasawa na mapenzi yako..
Nasi washarika/waumini ukatupe neema ya kutii na kuchukuliana,kupendana,kushirikiana,kuonyana kwa wema na upendo
tusimpe adui nafasi na kazi ya Mungu iende kama inavyopaswa kuenda..
 injili iende mbele na Neno lita simama..

Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu. Watumwa ambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharau kwani ni ndugu zao. Badala yake, wanapaswa kuwatumikia hata vizuri zaidi, maana hao wanaopata faida kutokana na kazi yao ni waumini ambao wanawapenda. Unapaswa kufundisha na kuhubiri mambo haya. Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya uchaji wa Mungu, huyo amejaa majivuno na wala hajui chochote. Ni mtu wa kupenda ubishi na magombano juu ya maneno matupu, na hiyo husababisha wivu, ugomvi, matusi, shuku mbaya, na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya kujipatia utajiri. Kweli kumcha Mungu humfanya mtu awe tajiri sana, ikiwa anatosheka na vitu alivyo navyo. Maana hatukuleta kitu chochote hapa duniani, wala hatutachukua chochote. Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo. Lakini wale wanaotaka kutajirika huanguka katika majaribu, na kunaswa katika mtego wa tamaa nyingi mbaya za kipumbavu, ambazo huwavuta mpaka kwenye uharibifu na maangamizi. Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi. Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, upendo, subira na unyenyekevu. Piga mbio kadiri uwezavyo katika shindano la mbio za imani, ukajipatie tuzo la uhai wa milele uliloitiwa wakati ulipokiri imani yako mbele ya mashahidi wengi. Mbele ya Mungu anayevipa vitu vyote uhai, na mbele ya Yesu Kristo aliyetoa ushahidi na kukiri ukweli mbele ya Pontio Pilato, nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka siku ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo. Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaao uliopangwa na Mungu mwenye heri na aliye Mtawala pekee, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana. Yeye peke yake anaishi milele katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina. Waamuru watu walio matajiri katika mambo ya maisha ya sasa, wasijivune, wasiweke tumaini lao katika mali isiyoweza kutegemewa; bali wamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimu hutupatia vitu vyote tuvifurahie. Waamuru watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, na wawe wakarimu na walio tayari kuwashirikisha wengine mali zao. Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uhai ambao ni uhai wa kweli. Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine “Elimu.” Maana wengine wamejidai kuwa na hiyo elimu, na matokeo yake wamepoteza imani. Nawatakieni nyote neema!


Asante Mungu wetu katika yote..
tunayaweka haya mikononi mwako,tukiamini na kushukuru daima..
wewe ni Mungu wetu na kimbilio letu..
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe...
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami..
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea katika yote..
msipungukiwe katika mahitaji yenu,Mungu akawape kama itakavyompendeza yeye..
Nawapenda.


Vita vitakatifu dhidi ya Midiani


1Mwenyezi-Mungu aliongea na Mose, akamwambia, 2“Walipize kisasi Wamidiani mambo waliyowatenda Waisraeli; kisha wewe utafariki.”
3Basi Mose akazungumza na watu akawaambia, “Watayarisheni watu kwa vita waende kuwashambulia Wamidiani kumlipizia Mwenyezi-Mungu kisasi. 4Kutoka kila kabila la Israeli, mtapeleka watu 1.000 vitani.”
5Basi, watu 1,000 walitolewa kutoka kila kabila miongoni mwa maelfu ya Waisraeli, jumla wanaume 12,000 wenye silaha. 6Mose aliwapeleka vitani chini ya uongozi wa Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akiwa na vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kutoa ishara. 7Waliishambulia nchi ya Midiani, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose, wakawaua wanaume wote. 8Miongoni mwa watu hao waliouawa, kulikuwako wafalme watano wa Midiani: Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori.
9Waisraeli waliteka nyara: Ng'ombe, kondoo na mali yao yote. 10Miji yao yote, makazi yao na kambi zao zote waliziteketeza kwa moto. 11Walichukua nyara zote na mateka yote, ya watu na ya wanyama, 12wakampelekea Mose na Eleazari, na jumuiya yote ya Waisraeli iliyokuwa kambini katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya Yordani karibu na Yeriko.

Kurudi vitani

13Mose, kuhani Eleazari, na viongozi wote wa jumuiya ya Waisraeli walitoka kambini, wakaenda kuwalaki wanajeshi. 14Mose alikasirishwa na maofisa wa jeshi na makamanda waliosimamia makundi ya majeshi 1,000 na makundi ya wanajeshi mamia waliorudi kutoka vitani. 15Mose akawauliza, “Kwa nini mmewaacha wanawake hawa wote hai? 16Taz Hes 25:1-9 Kumbukeni kwamba wanawake ndio waliofuata shauri la Balaamu, wakasababisha Waisraeli wamwasi Mwenyezi-Mungu kule Peori hata maradhi mabaya yakawajia watu wake Mwenyezi-Mungu. 17Kwa hiyo basi, waueni watoto wote wa kiume na kila mwanamke aliyewahi kulala na mwanamume. 18Lakini msiwaue wasichana wote ambao hawajapata kulala na mwanamume; waacheni hai kwa ajili yenu wenyewe. 19Wote wale walio miongoni mwenu ambao wameua mtu au kugusa maiti ni lazima wakae nje ya kambi kwa muda wa siku saba; jitakaseni pamoja na mateka wenu katika siku ya tatu na ya saba. 20Ni lazima mtakase pia kila vazi, kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa manyoya ya kondoo au kwa mti.”
21Kuhani Eleazari akawaambia wanaume waliorudi vitani, “Hii ndiyo sheria ambayo Mwenyezi-Mungu amempa Mose. 22Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati na madini ya risasi, 23yaani vitu vyote ambavyo vinastahimili moto, vitatakaswa kwa kupitishwa motoni. Hata hivyo, ni lazima vitakaswe kwa maji ya utakaso. Vitu vingine vyote ambavyo haviwezi kustahimili moto vitatakaswa kwa maji ya utakaso. 24Siku ya saba ni lazima muyafue mavazi yenu; ndipo mtakapokuwa safi na kuruhusiwa kuingia kambini.”

Kugawa nyara na mateka

25Mwenyezi-Mungu akaongea na Mose, akamwambia, 26“Wewe na kuhani Eleazari, pamoja na viongozi wa koo za jumuiya ya Waisraeli, fanyeni hesabu ya nyara ya vitu, watu na wanyama. 27Gaweni nyara katika mafungu mawili, fungu moja la wanajeshi waliokwenda vitani na fungu lingine kwa ajili ya jumuiya nzima. 28Kisha kutokana na lile fungu la wanajeshi waliokwenda vitani, tenga zaka kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu: Kitu kimoja kutoka kila vitu 500, iwe ni watu, ng'ombe, punda, kondoo au mbuzi, 29umpe kuhani Eleazari kuwa sadaka kwa Mwenyezi-Mungu. 30Kutoka lile fungu la jumuiya nzima, chukua sehemu moja ya kila hamsini, iwe ni watu, ng'ombe, punda, kondoo na mbuzi. Hivyo utawapa Walawi ambao wana wajibu wa kuhudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.” 31Mose na kuhani Eleazari walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
32Nyara walizoteka wanajeshi zilikuwa: Kondoo 675,000, 33ng'ombe 72,000, 34punda 61,000, 35na wasichana ambao hawakuwa wamelala na mwanamume 32,000. 36Nusu yake, sehemu ambayo iligawiwa wanajeshi waliokwenda vitani, ilikuwa kondoo 337,500, 37katika hao 675 walitolewa kwa Mwenyezi-Mungu. 38Ngombe wa wanajeshi walikuwa 36,000, na katika hao 72 walitolewa zaka kwa Mwenyezi-Mungu. 39Punda wao walikuwa 30,500, na katika hao 61 walitolewa zaka kwa Mwenyezi-Mungu. 40Watu walikuwa 16,000, na katika hao sehemu ya Mwenyezi-Mungu ilikuwa ni watu thelathini na wawili. 41Basi, Mose akampa kuhani Eleazari zaka hiyo iliyotolewa kwa Mwenyezi-Mungu, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
42Ile nusu waliopewa Waisraeli, ambayo Mose aliitenga na ile nusu waliyopewa wanajeshi waliokwenda vitani, 43ilikuwa kondoo 337,500, 44ng'ombe 36,000, 45punda 30,500, 46na watu 16,000. 47Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.
48Kisha maofisa wa majeshi, makapteni na makamanda wa askari wakamwendea Mose, 49wakamwambia “Watumishi wako tumewahesabu askari wote walio chini yetu na tumeona kwamba hakuna hata mmoja wao anayekosekana. 50Basi, tumeleta vyombo vya dhahabu, vikuku, bangili, pete za mhuri, vipuli na shanga ambavyo kila mtu alipata. Tumevitoa ili nafsi zetu zifanyiwe upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.” 51Mose na kuhani Eleazari wakapokea vitu vyote vilivyonakshiwa kwa dhahabu. 52Jumla ya dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu ilikuwa karibu kilo 200. 53(Kila askari alijichukulia nyara zake binafsi). 54Basi, Mose na kuhani Eleazari wakaipokea dhahabu hiyo kutoka kwa makamanda wakaipeleka katika hema la mkutano, iwe ukumbusho wa Waisraeli mbele ya Mwenyezi-Mungu.



Hesabu31;1-54



Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday, 14 August 2017

Mtanzania Ashinda Tuzo ya Mhasibu Kiongozi London 2017


Baada ya kuhitimu Uhasibu na kufanya kazi kwa  bidii na nidhamu Mtanzania Joyce Materego aliteuliwa mmoja wa viongozi bora, London,  karibuni. 
Mahojiano yake na KSTL ,  yadokeza kifupi ilikuwaje




Mhasibu, mkalimani, mzazi, mpenzi wa sanaa na fasihi- mchapa kazi Joyce Materego. Kati ya Watanzania Ughaibuni wenye bidii. Anatueleza jinsi alivyozawadiwa kazini kwake kama mhasibu kiongozi sekta yake, London, 2017.


Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..30



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..!
Baba wa Mbinguni,Mungu wetu,Muumba wetu..
Muumba wa Mbingu na Nchi,Mwenyezi-Mungu,
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Yahwe..!Jehovah..!Mungu wa Wajane,Baba wa Yatima..
Utukuzwe Baba wa Mbinguni,Usifiwe Muumba wetu..
Uhimidiwe Mungu wetu,Unatosha Mungu wetu..
Hakuna kama wewe,Baba wa Upendo,Mfalme wa Amani..

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Si kwamba sisi ni wema sana,Si kwamba sisi tunajua sana,Si kwamba sisi ni wazuri mno,Wala si kwa nguvu zetu wala si kwa utashi wetu..
Ni kwa Neema/Rehema zako Mungu wetu sisi leo hii kuwa hivi tulivyo..

Tunajishusha na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya..
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa rehema tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wote waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Mfalme wa Amani ukatawale maisha yetu..
Tunaomba utubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu wetu tukatende kama itakavyo kupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mfalme wa Amani ukatupe kama inavyokupendeza wewe..

Mungu Baba tunayaweka maisha yetu mikononi mwako,Ndoa/Nyumba zetu ,watoto wetu/familia,ndugu na wote wanao tuzunguka Mungu wetu ukawalinde na kuwafunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..


Mungu asema hivi: “Enyi wakazi wa mbali nyamazeni mnisikilize! Enyi mataifa jipeni nguvu; jitokezeni mkatoe hoja zenu, na tuje pamoja kwa hukumu. “Nani, ila mimi, aliyemwita shujaa toka mashariki, mtu ambaye hupata ushindi popote aendako? Mimi huyatia mataifa makuchani mwake, naye huwaponda wafalme chini ya miguu yake! Upanga wake huwafanya kuwa kama vumbi, kwa upinde wake huwapeperusha kama makapi. Yeye huwafuatia na kupita salama; huenda kasi kana kwamba hagusi chini. Nani aliyefanya yote haya yatendeke? Ni nani aliyepanga wakati wa kila tukio? Mimi Mwenyezi-Mungu nipo tangu mwanzo, mimi nitakuwapo hata milele. “Wakazi wa mbali wameona niliyotenda, wakaogopa; dunia yote inatetemeka kwa hofu. Watu wote wamekusanyika, wakaja. Kila mmoja anamhimiza mwenzake akisema, ‘Haya! Jipe moyo!’ Fundi anamhimiza mfua dhahabu, naye alainishaye sanamu kwa nyundo, anamhimiza anayeiunga kwa misumari. Wote wanasema, ‘Imeungika vizuri sana!’ Kisha wanaifunga kwa misumari isitikisike. “Sikiliza ewe Israeli, mtumishi wangu, wewe, Yakobo ambaye nimekuchagua, wewe mzawa wa Abrahamu, rafiki yangu; wewe niliyekuleta toka miisho ya dunia, wewe niliyekuambia: ‘Wewe u mtumishi wangu; mimi sikukutupa, bali nilikuchagua.’ Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi. “Naam! Wote waliokuwakia hasira, wataaibishwa na kupata fedheha. Wote wanaopingana nawe, watakuwa si kitu na kuangamia. Utawatafuta hao wanaopingana nawe, lakini watakuwa wameangamia. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia: ‘Usiogope, nitakusaidia.’” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Enyi watu wa Yakobo dhaifu kama mdudu, enyi Waisraeli, msiogope! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema nitawasaidia. Mimi ni Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli. Nitawafanya muwe kama chombo cha kupuria, chenye meno mapya na makali. Mtaipura milima na kuipondaponda; vilima mtavisagasaga kama makapi. Mtaipepeta milima hiyo, nao upepo utaipeperushia mbali, naam, dhoruba itaitawanya huko na huko. Nanyi mtafurahi kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu; mtaona fahari kwa sababu yangu Mungu Mtakatifu wa Israeli. “Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate, wakiwa wamekauka koo kwa kiu, mimi Mwenyezi-Mungu nitawajibu; mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha. Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu, na chemchemi katika mabonde. Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji, na nchi kame kuwa chemchemi za maji. Nitapanda miti huko nyikani: Mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni; nitaweka huko jangwani: Miberoshi, mivinje na misonobari. Watu wataona jambo hilo, nao watatambua na kuelewa kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo, mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo.”

Isaya 41:1-20



Tazama wenye Shida/tabu na wote wanaotaabika,waliokatika majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu wakapate uponyaji wa mwili na roho,Ukawape neema ya kusimamia Amri,Sheria na Neno lako nalo likawaweke huru..

Asante Mungu wetu katikayote..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako,Tuliyoyanena na tusiyo yanena Baba wa Mbinguni unayajua na kutujua sisi zaidi ya tunavyojijua..
Sifa na utukufu tunakurudishia Mungu wetu..

Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapenda/waungwana kwakuwa nami..
Mungu akawabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.


Mwongozo kuhusu nadhiri

1 Taz Kumb 23:21-23; Mat 5:33 Kisha Mose alizungumza na viongozi wa makabila ya Israeli, akawaambia, “Hili ndilo neno lililoamriwa na Mwenyezi-Mungu:
2“Mtu akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu au akiahidi kwa kiapo na kujifunga nafsi yake kwa ahadi, ni lazima atimize ahadi yake; ni lazima atekeleze yote yale aliyotamka kwa kauli yake.
3“Msichana ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu na kujifunga mwenyewe kwa ahadi, 4na baba yake akawa amesikia ahadi hiyo, asimpinge, basi, nadhiri zake alizoweka zitambana na kila ahadi aliyotoa itambana. 5Lakini kama baba yake akisikia juu ya nadhiri hiyo, akampinga, basi nadhiri zake na ahadi yake havitambana. Mwenyezi-Mungu atamsamehe kwa sababu baba yake amelipinga jambo hilo.
6“Ikiwa msichana ataolewa baada ya kuweka nadhiri, au kuahidi bila ya kufikiri vizuri kwanza, na akajifunga mwenyewe, 7halafu mumewe akasikia jambo hilo asimpinge, basi nadhiri zake zitambana na ahadi zake zitambana. 8Lakini kama mume wake akisikia jambo hilo akampinga, basi huyo mumewe atabatilisha nadhiri ya mkewe na tamko lake alilotoa bila kufikiri; naye Mwenyezi-Mungu atamsamehe.
9“Lakini nadhiri au ahadi yoyote aliyoiweka mama mjane au mwanamke aliyepewa talaka ambayo kwayo amejifunga, ni lazima imbane.
10“Mwanamke aliyeolewa akiweka nadhiri au akiahidi kwa kiapo akiwa nyumbani kwa mumewe, 11kisha mume wake akasikia jambo hilo lakini asimpinge, wala kumwambia kitu, basi, nadhiri zake zote zitambana; kadhalika na ahadi zake zote zitambana. 12Lakini kama mumewe atakaposikia habari zake, akizitangua na kuzibatilisha, basi, hata kama alitaka kutimiza nadhiri au ahadi zake, hatawajibika kuzitimiza; mumewe atakuwa amezitangua na Mwenyezi-Mungu atamsamehe. 13Mumewe anaweza kuthibitisha au kutangua nadhiri au ahadi yoyote inayomfunga. 14Lakini ikiwa mumewe hatasema neno lolote tangu siku atakaposikia habari za nadhiri au ahadi za mkewe, basi atakuwa amezithibitisha siku hiyo alipopata habari zake kwa sababu hakusema chochote. 15Lakini akizibatilisha na kuzitangua muda fulani baada ya kusikia habari zake, basi yeye atakuwa na lawama kwa kosa la mkewe.”
16Hizi ndizo kanuni ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya mume na mkewe; baba na binti yake, huyo binti akiwa bado kijana na anakaa nyumbani kwa baba yake.



Hesabu30;1-16



Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday, 11 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..29




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..!Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru kwa wema na fadhili zake kwetu..

Asante Baba Wambinguni ,Baba yetu na Mungu wetu..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Yahweh..!Jehova Nissi,Jehovah Shammah..!Jehovah Rapha..!Jehovah Shalom..!Jehovah Jireh..Jehovah Roi..!
Baba wa uzima..!Baba wa Rehema..!Baba wa Upendo..!Kimbilio letu..!
Utukuzwe Mfalme wa Amani,Hakuna kama wewe Mungu wetu,Unatosha Baba wa Mbinguni..!

Asante Mungu wetu  kwakuwa nasi  na kutulinda wakati wote..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Sikwamba sisi ni wema sana au wajuaji mno..
Hapana ni kwa neema/rehema zako Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo..

Tunakuja mbele zako Baba wa Mbingu,Tukijishusha,tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako Jehovah..Tunaomba utusamehe dhambi zetu tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Jehovah..Ukatubariki na ukabariki kazi za mikono yetu,masomo na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama itakavyo kupendeza wewe..
Ukabariki ridhiki zetu nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..


“Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya toka miongoni mwa watu mnakokaa. Nitawakusanya kutoka nchi ambako mlitawanywa. Nitawarudisha nchini Israeli. Nanyi mtakaporudi nchini mwenu nitaondoa vitu vyote vichafu na machukizo yote. Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa ule moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii, ili mpate kufuata kanuni zangu na kuyatii maagizo yangu; nanyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu. Lakini hao ambao moyo wao umeambatana na vitu najisi na machukizo yao, nitawaadhibu kadiri ya mienendo yao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama wenye shida/tabu na wote wanaotaabaka,waliokatika vifungo mbalimbali Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu wakapate uponyaji wa mwili na roho..ukawape neema ya kukujua wewe na kusimamia Neno,Amri na Sheria zako nazo ziwaweke huru..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika kunanena,tukanene yaliyo yako,akatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako,tukawe wenye hekima,busara,kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema Mungu wetu nasi tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Msifuni Mwenyezi-Mungu! Jinsi gani ilivyo vizuri kumwimbia sifa Mungu wetu! Yeye ni mwema na astahili kuimbiwa sifa. Mwenyezi-Mungu anajenga tena mji wa Yerusalemu; anawarudisha Waisraeli waliokuwa uhamishoni. Anawaponya waliovunjika moyo; na kuwatibu majeraha yao. Anaamua idadi itakayokuwako ya nyota, na kuzipa zote majina yao. Bwana wetu ni mkuu, ana nguvu nyingi; maarifa yake hayana kipimo. Mwenyezi-Mungu huwakweza wanyenyekevu, lakini huwatupa waovu mavumbini. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu nyimbo za shukrani, mpigieni kinubi Mungu wetu! Yeye hulifunika anga kwa mawingu, huitengenezea nchi mvua, na kuchipusha nyasi vilimani. Huwapa wanyama chakula chao, na kuwalisha makinda ya kunguru yanapolia. Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari; lakini hupendezwa na watu wamchao, watu wanaotegemea fadhili zake. Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee Yerusalemu! Umsifu Mungu wako, ee Siyoni! Maana yeye huimarisha milango yako, huwabariki watu waliomo ndani yako. Huweka amani mipakani mwako; hukushibisha kwa ngano safi kabisa. Yeye hupeleka amri yake duniani, na neno lake hufikia lengo lake haraka. Hutandaza theluji kama pamba, hutawanya umande kama majivu. Huleta mvua ya mawe kama kokoto na kwa ubaridi wake maji huganda. Kisha hutoa amri, maji hayo yakayeyuka; huvumisha upepo wake, nayo yakatiririka. Humjulisha Yakobo ujumbe wake, na Israeli masharti na maagizo yake. Lakini hakuyatendea hivyo mataifa mengine; watu wengine hawayajui maagizo yake. Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Sifa na utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakunitembelea/kunisoma
Mungu aendelee kuwa nanyi katika yote..
Nawapenda.


Sadaka ya sikukuu ya mwaka mpya

(Lawi 23:23-25)

1“Siku ya kwanza ya mwezi wa saba, mtafanya mkutano mtakatifu. Msifanye kazi. Hiyo ni siku ya kupiga tarumbeta. 2Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga wawili, kondoo madume wawili, na wanakondoo wa kiume saba wa mwaka mmoja, wote wawe wasio na dosari yoyote. 3Mtatoa pia sadaka yake ya nafaka ya unga safi uliochanganywa na mafuta: Kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo dume, 4na kilo moja kwa kila mwanakondoo. 5Tena mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi ili kuwafanyia upatanisho. 6Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mpya na sadaka yake ya nafaka, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji kama inavyotakiwa kuwa harufu nzuri ipendezayo, ni sadaka kwa Mwenyezi-Mungu iliyoteketezwa kwa moto.

Matoleo ya siku ya kufanyiwa msamaha

(Lawi 23:26-32)

7 Taz Lawi 16:29-34 “Siku ya kumi ya mwezi wa saba mtafanya mkutano mtakatifu. Siku hiyo ni lazima mfunge na msifanye kazi. 8Mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, wanakondoo saba wa mwaka mmoja. Wote wasiwe na dosari. 9Licha ya vitu hivi mtatoa sadaka ya unga safi uliochanganywa na mafuta kilo tatu pamoja na huyo fahali, kilo mbili pamoja na yule kondoo dume, 10na kilo moja kwa kila mwanakondoo. 11Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kufanyiwa upatanisho, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.

Sadaka ya sikukuu ya vibanda

(Lawi 23:33-43; Kumb 16:13-17)

12“Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtafanya mkutano mtakatifu. Hamtafanya kazi siku hiyo. Mtaadhimisha sikukuu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu kwa siku saba. 13Mtatoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, iliyo harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga kumi na watatu, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja. Wote wawe bila dosari. 14Sadaka itakayoandamana nazo itakuwa unga safi uliochanganywa na mafuta: Kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo, 15na kilo moja kwa kila mwanakondoo. 16Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
17“Siku ya pili mtatoa: Fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari. 18Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za vinywaji pamoja na wale fahali, kondoo na wanakondoo, kulingana na idadi yao. 19Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya sadaka ya kuteketezwa ya kawaida pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
20“Siku ya tatu mtatoa: Fahali kumi na mmoja, kondoo wawili, wanakondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari. 21Mtawatolea pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji kama ilivyotakiwa kulingana na idadi yao. 22Vilevile mtatoa beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
23“Siku ya nne mtatoa: Fahali kumi, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne, wasio na dosari. 24Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali na kondoo na wanakondoo kulingana na idadi yao, kama inavyotakiwa. 25Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
26“Siku ya tano, mtatoa fahali tisa, kondoo wawili, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na dosari. 27Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali na kondoo na wanakondoo kulingana na idadi yao kama inavyotakiwa. 28Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
29“Siku ya sita mtatoa fahali wanane, kondoo madume wawili, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na dosari. 30Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali, kondoo dume na wanakondoo kulingana na idadi yao, kama inavyotakiwa. 31Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.
32“Siku ya saba mtatoa fahali saba, kondoo madume watatu, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari. 33Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na hao fahali, kondoo dume, na wanakondoo, kulingana na idadi yao, kama wanavyotakiwa. 34Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka yake ya kinywaji.
35“Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa. Msifanye kazi siku hiyo. 36Mtatoa sadaka ya kuteketezwa iliyo harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wanakondoo madume saba wa mwaka mmoja wasio na dosari. 37Mtatoa pia sadaka ya nafaka na sadaka za kinywaji pamoja na huyo fahali, huyo kondoo dume, na wale wanakondoo kulingana na idadi yao kama inavyotakiwa. 38Pia mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka ya kinywaji.
39“Haya ndiyo maagizo kuhusu sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na sadaka za amani mtakazomtolea Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu zenu zilizopangwa. Licha ya hizi zote, zipo pia sadaka za kuteketezwa, za nafaka na za kinywaji, ambazo mnamtolea Mwenyezi-Mungu kutimiza nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari.”
40Basi, Mose akawaambia Waisraeli kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.




Hesabu29;1-40


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday, 10 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..28




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Yeye aliyetupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Yeye aliye mlinzi wetu wakati wote..
Yeye aliyetuamsha salama na wenye afya..
Yeye atuongozaye katika yote..
Wema na fadhili zake ni za Ajabu mno...

Atukuzwe Mungu wetu na Baba yetu..
Asifiwe na kuabudiwa daima..
Tumshukuru Mungu wetu kwa maana anastahili sifa..
Ahimidiwe,Atukuzwe,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..

Asante Baba wa Mbinguni katika yote uliyotutendea/unayoendelea kututendea..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu..
Muumba wa Mbingu, Nchi na vyote vilivyomo Baba ni mali yako..

Tunaomba Mungu Baba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyenda kufanya/kutenda Mungu wetu tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu..Baba wa Mbinguni ukatupe kama itakavyokupendeza wewe..
Mfalme wa Amani ukatawale na kutuatamia katika maisha yetu..
Nyumba zetu/ndoa,watoto/familia,ndugu/jamaa na wote wanaotuzunguka..

Mungu Baba tazama wafiwa ukawe mfariji wao..Jehovah..tazama wenye Shida/tabu,wagonjwa,waliokatika vifungo mbalimbali,waliokata tamaa na waliokataliwa..Mungu wa Rehema ukawaguse na mkono wako wenye nguvu..wakapate kupona kimwili na kiroho pia..
wakapate neema ya kujua neno lako na kusimami sheria na Amri zako..
wakaijue kweli yako nayo iwaweke huru..



Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: Kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake; maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na, amri zake si ngumu, maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu. Nani, basi, awezaye kuushinda ulimwengu? Ni yule anayeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Asante Baba wa Upendo,Baba wa Rehema,Baba wa faraja..
Mungu wa wajane,Baba wa yatima..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Kazini,shuleni na kila sehemu tupitapo/tuingiapo Mungu wetu ukaonekane..
Tunenapo tukanene yaliyoyako..
Ukatupe macho ya rohoni na masikio ya kusikia kuona na kusikia sauti yako katika maisha yetu..
Ukatupe kiu ya kukutafuta wewe na kukujua zaidi..
Tukasimamie Neno lako na Sheria,Amri zako Mungu wetu..


Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnao uhai wa milele nyinyi mnaoamini kwa jina la Mwana wa Mungu. Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza. Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba hutupatia yote tunayomwomba. Mtu akimwona ndugu yake ametenda dhambi isiyompeleka kwenye kifo, anapaswa kumwombea kwa Mungu, naye Mungu atampatia uhai. Nasema jambo hili kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi yenye kumpeleka mtu kwenye kifo, nami sisemi kwamba mnapaswa kumwomba Mungu kwa ajili ya hiyo. Kila tendo lisilo adilifu ni dhambi, lakini kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo. Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda salama, na yule Mwovu hawezi kumdhuru. Tunajua kwamba sisi ni wake Mungu ingawa ulimwengu wote unatawaliwa na yule Mwovu. Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli – katika muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio uhai wa milele. Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu!

Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Baba wa Mbinguni..
Tunayaweka haya  yote mikononi mwako Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana
 kwakuwanami/kunisoma
Baba wa Upendo akadumishe upendo wenu..
Msipungukiwe katika mahitaji yenu..
Mungu mwenye nguvu akawape kama itakavyompendeza yeye..
Nawapenda.

Sadaka za kila siku

(Kut 29:38-46)

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waamuru Waisraeli ifuatavyo: Nyinyi mtanitolea kwa wakati wake tambiko zitakiwazo: Vyakula vya kuteketezwa kwa moto, vyenye harufu nzuri ya kupendeza. 3Waambie kwamba sadaka watakayonitolea ya kuteketezwa kwa moto, itakuwa ifuatavyo: Wanakondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari yoyote, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. 4Mwanakondoo mmoja atatolewa asubuhi na wa pili jioni; 5kila mmoja atatolewa pamoja na sadaka ya nafaka ya kilo moja ya unga uliochanganywa pamoja na lita moja ya mafuta bora yaliyopondwa. 6Hii ni sadaka ya kutolewa kila siku inayoteketezwa kabisa motoni, ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza mlimani Sinai kama sadaka ya chakula, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. 7Sadaka ya kinywaji itakayotolewa na kila mwanakondoo ni lita moja ya divai. Utaimimina sadaka hii ya kinywaji kikali mahali patakatifu. 8Wakati wa jioni utamtoa yule mwanakondoo mwingine kama sadaka ya nafaka na kama sadaka ya kinywaji utaitoa kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, sadaka yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.

Dhabihu za Sabato

9“Siku ya Sabato, mtatoa sadaka ya wanakondoo wawili wa kiume wa mwaka mmoja wasio na dosari, sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji. 10Sadaka hii ya kuteketezwa itatolewa kila siku ya Sabato licha ya ile sadaka ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

Sadaka za kila mwezi

11“Mwanzoni mwa kila mwezi, mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa: Fahali wadogo wawili, kondoo dume mmoja na, wanakondoo saba madume wa mwaka mmoja, wasio na dosari. 12Mtatoa sadaka ya nafaka ya unga laini kilo tatu, uliochanganywa na mafuta kwa kila fahali mmoja; mtatoa kilo mbili za unga kwa kila kondoo dume, 13na kilo moja ya unga kwa kila mwanakondoo. Sadaka hizi za kuteketezwa ni sadaka za chakula zenye harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. 14Kipimo cha sadaka ya kinywaji kinachohitajika ni lita 2 za divai kwa kila fahali; lita moja u nusu kwa kila kondoo dume, na lita moja kwa kila mwanakondoo. Hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika mwaka mzima. 15Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.


Sadaka ya Pasaka

(Lawi 23:5-14)

16 Taz Kut 12:1-13; Kumb 16:1-2 “Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza ni Pasaka ya Mwenyezi-Mungu. 17Taz Kut 12:14-20; 23:15; 34:18; Kumb 16:3-8 Siku ya kumi na tano ya mwezi huohuo ni sikukuu. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. 18Katika siku ya kwanza kutakuwa na mkutano mtakatifu. Siku hiyo hamtafanya kazi. 19Mtatoa sadaka ya kuteketezwa kama sadaka ya chakula kwa Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga wawili, kondoo dume mmoja, wanakondoo madume saba wa mwaka mmoja, wote wawe bila dosari. 20Sadaka ya nafaka itakayoandamana nazo itakuwa ya unga safi uliochanganywa na mafuta, kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo dume, 21na kilo moja kwa kila mmoja wa wale wanakondoo saba. 22Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi ili kuwafanyia upatanisho. 23Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kawaida inayotolewa kila siku asubuhi. 24Vivyo hivyo, kwa muda wa siku saba, mtatoa sadaka ya kuteketezwa ya kawaida ya chakula kwa kuteketezwa, ambayo ni harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. Hii mtaitoa licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji. 25Katika siku ya saba mtafanya mkutano mtakatifu; msifanye kazi.

Sadaka ya sikukuu ya mavuno

(Lawi 23:15-22)

26“Mnamo siku ya kwanza ya sikukuu ya majuma wakati mnapomtolea Mwenyezi-Mungu malimbuko ya nafaka zenu, mtafanya mkutano mtakatifu; msifanye kazi. 27Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga wawili, kondoo dume mmoja, na wanakondoo saba madume wa mwaka mmoja, wote hao wawe hawana dosari. 28Sadaka ya nafaka itakayoandamana nazo itakuwa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo dume, 29na kilo moja kwa kila mwanakondoo. 30Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi ili kuwafanyia upatanisho. 31Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kawaida pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

Hesabu28;1-31


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday, 9 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..27




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu...
Asante Mungu wetu Baba yetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Utukuzwe Mungu wetu wakati wote,Uabudiwe daima,
Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah..!

Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote, enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake. Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu, na kumtukuza Mwenyezi-Mungu! Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni; yeye aliyeumba mbingu na dunia.

Asante Mungu wetu  kwaulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Tunakuja mbele zako Mungu Baba tukijinyeyekeza,tukijishusha na tukijiachilia mikononi mwako Jehovah..
Mfalme wa Amani tunaomba utusamehe dhambi zetu zote..
Tulizoziwaza,tulizozinena,tulizozitenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Upendo nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Yahweh utuepushe katika majaribu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.’” Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: ‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.’” Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia: ‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’” Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake, akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.’” Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.



Ututakase Akili zetu na Miili yetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Binadamu hupanga mipango yake, lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa. Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi, kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu, huwageuza hata adui zake kuwa marafiki. Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake. Mfalme huamua kwa maongozi ya Mungu; anapotoa hukumu hakosei. Mwenyezi-Mungu hutaka kipimo na mizani halali; mawe yote mfukoni ya kupimia ni kazi yake. Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu, maana msingi wa mamlaka yao ni haki. Mfalme hupendelea mtu asemaye kwa unyofu; humpenda mtu asemaye ukweli. Hasira ya mfalme ni kama mjumbe wa kifo; mtu mwenye busara ataituliza. Uso wa mfalme ukingaa kuna uhai; wema wake ni kama wingu la masika. Kupata hekima ni bora kuliko dhahabu; kupata akili ni chaguo bora kuliko fedha. Njia ya wanyofu huepukana na uovu; anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake. Kiburi hutangulia maangamizi; majivuno hutangulia maanguko. Afadhali kuwa mnyenyekevu na kuwa maskini, kuliko kugawana nyara na wenye kiburi. Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu. Mwenye hekima moyoni huitwa mwenye akili; neno la kupendeza huwavutia watu. Hekima ni chemchemi ya uhai kwake aliye nayo, bali upumbavu ni adhabu ya wapumbavu. Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara; huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia. Maneno mazuri ni kama asali; ni matamu rohoni na yenye kuupa mwili afya. Mtu aweza kuona njia yake kuwa sawa, lakini mwishowe humwongoza kwenye kifo. Hamu ya chakula humhimiza mfanyakazi, maana njaa yake humsukuma aendelee. Mtu mwovu hupanga uovu; maneno yake ni kama moto mkali. Mtu mpotovu hueneza ugomvi, mfitini hutenganisha marafiki. Mtu mkatili humshawishi jirani yake; humwongoza katika njia mbaya. Anayekonyeza jicho kwa hila amepanga maovu; anayekaza midomo amekwisha nuia mabaya. Kuwa na mvi za uzee ni taji la utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu. Asiye mwepesi wa hasira ni bora kuliko mwenye nguvu; aitawalaye nafsi yake ni bora kuliko autekaye mji. Kura hupigwa kujua yatakayotukia, lakini uamuzi ni wake Mwenyezi-Mungu.


Tukasimamie Neno lako Amri na Sheria zako..
Mungu wetu ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Jehovah tunaomba ukatubariki na ukabariki kazi za mikono yetu
Ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda na tukatende kama itakavyokupendeza wewe..
Mungu wetu ukabariki na kuvitakase ,ukavifunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/kutumia..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Asante Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa pamoja..
Mungu aendelee kuwabariki..
Nawapenda.



Haki ya kurithi kwa wanawake

1Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirza walikuwa binti zake Selofehadi. Naye Selofehadi alikuwa mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase mwanawe Yosefu. 2Basi, hao binti wanne walimwendea Mose, wakasimama mbele yake na kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya ya Waisraeli, kwenye mlango wa hema la mkutano, wakasema, 3“Baba yetu alifia jangwani nyikani na bila mtoto yeyote wa kiume. 4Yeye hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora waliokusanyika dhidi ya Mwenyezi-Mungu, bali alikufa kutokana na dhambi yake mwenyewe. Kwa nini basi jina la baba yetu lifutwe katika ukoo wake kwa sababu hakuwa na mtoto wa kiume? Tupe urithi pamoja na ndugu zake baba yetu.”
5Mose akaleta lalamiko lao mbele ya Mwenyezi-Mungu. 6Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 7Taz Hes 36:2 “Wanachosema binti za Selofehadi ni kweli; wape urithi pamoja na ndugu za baba yao, wachukue urithi wake. 8Kisha waambie Waisraeli kwamba mtu yeyote akifa bila kuacha mtoto wa kiume, urithi wake atapewa binti yake. 9Ikiwa hana binti, basi urithi huo watapewa ndugu zake wa kiume. 10Na ikiwa hana ndugu wa kiume, basi urithi wake utawaendea baba zake, wakubwa na wadogo. 11Na ikiwa baba yake hana ndugu wa kiume, basi urithi wake utakuwa wa jamaa yake wa karibu, naye ataumiliki kama mali yake. Hii itakuwa kanuni na sheria kwa Waisraeli, kama vile mimi Mwenyezi-Mungu nilivyokuamuru.”

Yoshua ateuliwa kuwaongoza Waisraeli
(Kumb 31:1-8)
12 Taz Kumb 3:23-27; 32:48-52; Marko 6:34 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Panda juu ya Mlima huu wa miinuko ya Abarimu uitazame nchi ambayo nimewapa Waisraeli. 13Ukisha iona, nawe pia utafariki kama ndugu yako Aroni alivyofariki, 14kwa sababu hamkuitii amri yangu kule jangwani Sini. Wakati jumuiya yote ya watu walipolalamika juu yangu kule Meriba, hamkuacha utukufu wangu uonekane mbele yao walipotaka wapewe maji.” (Meriba ni chemchemi ya maji ya Kadeshi katika jangwa la Sini).
15Naye Mose akamwomba Mwenyezi-Mungu, 16“Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu uliye asili ya uhai wote,27:16 Mungu uliye asili ya uhai wote: Neno kwa neno: Mungu wa roho za wanaadamu wote. nakuomba umteue mtu wa kuisimamia jumuiya hii, 17Taz 1Fal 22:17; Eze 34:5; Mat 9:36 ambaye atawatangulia na kuwaongoza katika shughuli zao zote, ili wasije wakawa kama kondoo wasio na mchungaji.”
18 Taz Kut 24:13 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mtwae Yoshua mwana wa Nuni, mtu mwenye roho nzuri, kisha umwekee mikono, 19na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote, umkabidhi jukumu hilo. 20Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli imtii. 21Taz Kut 28:30; 1Sam 14:41; 28:6 Yeye atamtegemea kuhani Eleazari ambaye atamjulisha matakwa yangu kwa kutumia jiwe la kauli.27:21 jiwe la kauli: Kiebrania: Urimu, moja ya mawe mawili yaliyotumiwa na kuhani kujua matakwa ya Mungu. Kwa njia hii, Eleazari atamwongoza Yoshua na jumuiya yote ya Waisraeli wanapotoka na wanapoingia.” 22Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Alimtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote ya Waisraeli. 23Taz Kumb 31:23 Kisha akamwekea mikono kichwani na kumpa mamlaka kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu.


Hesabu27;1-23


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday, 8 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..26



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru  Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu  wetu Baba yetu,Muumba wa yote..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Utukuzwe ee Baba..Uinuliwe Yahweh..Usifiwe Mfalme wa Amani..Uabudiwe daima..!


Uponyaji unapatikana kwako,Upendo wa kweli upo ndani yako,Faraja inapatika nawe,Furaha ipo na wewe,wema na fadhili zipo kwako..

wewe ni Mungu wa Wajane,Wewe ni Baba wa Yatima,,
Wewe ni Alfa na Omega..!Hakuna lililogumu kwako Mungu..!
Sifa na Utukufu ni wako Jehovah...!

Ee Mwenyezi-Mungu, nitaimba fadhili zako milele; nitavitangazia vizazi vyote uaminifu wako. Natamka kuwa fadhili zako zadumu milele; uaminifu wako ni thabiti kama mbingu. Umesema: “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi: ‘Daima nitamweka mzawa wako kuwa mfalme, tena nitaudumisha ufalme wako milele.’” Mbingu na zisifu maajabu yako, ee Mwenyezi-Mungu; uaminifu wako usifiwe katika kusanyiko la watakatifu. Nani mbinguni awezaye kulinganishwa nawe ee Mwenyezi-Mungu? Nani aliye sawa nawe kati ya viumbe vya mbinguni? Wewe waogopwa katika baraza la watakatifu; wote wanaokuzunguka wanatiwa hofu kuu. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, ni nani mwenye nguvu kama wewe, ee Mwenyezi-Mungu? Uaminifu umekuzunguka pande zote. Wewe watawala machafuko ya bahari; mawimbi yake yakiinuka, wayatuliza. Uliliponda joka Rahabu na kuliua; uliwatawanya adui zako kwa nguvu yako. Mbingu ni zako na dunia ni yako pia; ulimwengu na vitu vyote vilivyomo wewe uliviumba. Wewe uliumba kaskazini na kusini; milima Tabori na Hermoni inakusifu kwa furaha. Mkono wako una nguvu, mkono wako una nguvu na umeshinda! Uadilifu na haki ni msingi wa utawala wako; fadhili na uaminifu vyakutangulia! Heri watu wanaojua kukushangilia, wanaoishi katika mwanga wa wema wako, ee Mwenyezi-Mungu. Wanafurahi mchana kutwa kwa sababu yako, na kukusifu kwa ajili ya uadilifu wako. Wewe ndiwe fahari na nguvu yao; kwa wema wako twapata ushindi. Ee Mwenyezi-Mungu, mlinzi wetu ni wako, mfalme wetu ametoka kwako ewe Mtakatifu wa Israeli.

Tunakuja Mbele zako Mungu wetu tukijishusha,tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Mungu Baba..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mungu wetu..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema yakuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Yahweh  utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..


Jehovah tunaomba ukatubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu Baba tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo na zitokazo Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwasaidia wenye kuhitaji..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mfalme wa Amani ukatupe kama inavyokupendeza wewe..

Yahweh tazama wenye shida/tabu na wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,wagonjwa na waliokata tamaa,wafiwa ukawe mfariji wao..
Jehovah tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye kimwili na kiroho pia..Ukawape neema ya kusimamia Neno lako nalo litawaweka huru..


Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi: “Kwa ajili yenu nitatuma jeshi Babuloni. Nitayavunjilia mbali malango ya mji wake, na kelele za hao Wakaldayo zitageuka maombolezo. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu; Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati mmoja nilifanya barabara baharini nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa. Nililipiga jeshi lenye nguvu, jeshi la magari na farasi wa vita, askari na mashujaa wa vita. Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena, niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa. Sasa nasema: ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya. Kinafanyika sasa hivi, nanyi mtaweza kukiona. Nitafanya njia nyikani, na kububujisha mito jangwani. Wanyama wa porini wataniheshimu, kina mbweha na kina mbuni, maana nitaweka maji nyikani, na kububujisha mito jangwani, ili kuwanywesha watu wangu wateule, watu niliowaumba kwa ajili yangu mwenyewe, ili wazitangaze sifa zangu!’

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema Mungu Baba popote tulipo tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Asante Mungu wetu..tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe  Baba wa Yote..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa katika yote..
Mungu aendelee kuonekana katika maisha yenu..
Msipungukiwe katikamahitaji  yenu Baba wa Mbinguni akawape kama itakavyompendeza yeye..

Nawapenda.


Sensa ya Pili

1 Taz Hes 1:1-46 Baada ya yale maradhi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, 2“Hesabuni jumuiya yote ya Waisraeli, kila mtu kufuatana na jamaa yake. Wahesabuni watu wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi wanaofaa kwenda jeshini.” 3Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia, 4“Hesabuni watu kuanzia na wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.” Idadi ya Waisraeli waliotoka Misri ni hii:
5Kwanza ni kabila la Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Henoki, Palu, 6Hesroni na Karmi. 7Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730. 8Wazawa wa Palu walikuwa Eliabu, 9na wanawe Nemueli, Dathani na Abiramu. (Hawa wawili: Dathani na Abiramu, ndio waliokuwa wamechaguliwa miongoni mwa jumuiya, lakini wakampinga Mose na Aroni, na kujiunga na wafuasi wa Kora wakati walipomwasi Mwenyezi-Mungu. 10Wakati huo ardhi ilifunguka ikawameza, wakafa pamoja na Kora na wafuasi wake moto ulipoangamiza watu 250; wakawa onyo kwa watu. 11Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.)
12Kabila la Simeoni. Nemueli, Yamini, Yakini, 13Zera na Shauli. 14Hizo ndizo koo za kabila la Simeoni, jumla yao wanaume 22,000.
15Kabila la Gadi lilikuwa na jamaa za Sefoni, Hagi, Shuni, 16Ozni, Eri, 17Arodi na Areli. 18Hizo ndizo koo za kabila la Gadi, jumla wanaume 40,500.
19Kabila la Yuda lilikuwa na wanawe wa Yuda Eri na Onani. Hawa walifia nchini Kanaani. 20Kabila la Yuda lilikuwa na jamaa za Shela, Peresi, na Zera. 21Kutoka kwa Peresi, familia ya Hesroni na Hamuli. 22Hizo ndizo koo za Yuda, jumla wanaume 76,500.
23Kabila la Isakari lilikuwa na jamaa za Tola, Puva, 24Yashubu na wa Shimroni. 25Hizo ndizo koo za Isakari, jumla wanaume 64,300.
26Kabila la Zebuluni lilikuwa na jamaa za Seredi, wa Eloni na wa Yaleeli. 27Hizo ndizo koo za Zebuluni, jumla wanaume 60,500.
28Kabila la Yosefu baba yao Manase na Efraimu.
29Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi. 30Yezeri, Heleki, 31Asrieli, Shekemu, 32Shemida na Heferi. 33Selofehadi, mwana wa Heferi hakupata watoto wa kiume bali wa kike tu, nao ni Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirza. 34Hizo ndizo koo za Manase, jumla wanaume 52,700.
35Kabila la Efraimu lilikuwa na jamaa za Shuthela, Bekeri na Tahani. 36Ukoo wa Erani ulikuwa na jamaa ya Shuthela. 37Hizo ndizo koo za Efraimu, jumla wanaume 32,500. Zote hizo zilitokana na Yosefu.
38Kabila la Benyamini lilikuwa na jamaa za Bela, Ashbeli, Ahiramu, 39Shufamu na Hufamu. 40Koo za Ardi na Naamani, zilitokana na Bela. 41Hizo ndizo koo za Benyamini, jumla wanaume 45,600.
42Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu; 43ukoo ulikuwa na wanaume 64,400.
44Kabila la Asheri lilikuwa na jamaa za Imna, Ishvi na Beria. 45Koo za Heberi na Malkieli zilitokana na Beria. 46Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera. 47Hizo ndizo koo za kabila la Asheri, jumla wanaume 53,400.
48Kabila la Naftali lilikuwa na jamaa za Yaseeli, Guni, 49Yeseri na Shilemu. 50Hizi ndizo koo za kabila la Naftali, jumla wanaume 45,400.
51Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730.
52 Taz Hes 34:13; Yosh 14:1-2 Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 53“Makabila haya yatagawiwa nchi iwe urithi wao, kulingana na idadi ya majina yao. 54Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake. 55Hata hivyo ugawaji wa nchi utafanywa kwa kura. Kila kabila litarithi kulingana na majina ya ukoo wao. 56Urithi wa kila kabila utagawanywa kwa kura, kila kabila litapata kulingana na ukubwa au udogo wake.”
57Hizi ndizo koo za Walawi zilizoorodheshwa na jamaa zao: Gershoni, Kohathi na Merari, 58Pamoja na jamaa za Libni, Hebroni, Mahli, Mushi na Kora. Kohathi alikuwa baba yake Amramu. 59Mkewe Amramu aliitwa Yokebedi binti yake Lawi, aliyezaliwa Misri. Huyu alimzalia Amramu watoto wawili wa kiume, Aroni na Mose, na binti mmoja, Miriamu. 60Taz Hes 3:2 Aroni alikuwa na watoto wa kiume wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 61Taz Lawi 10:1-2; Hes 3:4 Nadabu na Abihu walikufa walipomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya moto usiofaa. 62Idadi ya Walawi wanaume wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ilikuwa 23,000. Hawa hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu wao hawakupewa urithi wowote miongoni mwao.
63Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko. 64Miongoni mwao hakuwamo hata mtu mmoja aliyesalia kati ya wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni ambao walifanya sensa ya kwanza jangwani Sinai. 65Taz Hes 14:26-35 Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema kwamba wote watafia jangwani, na kweli hakuna hata mmoja wao aliyebaki hai, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.


Hesabu26;1-65


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.