Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 24 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi Kumbukumbu la Sheria 2 (Kumbukumbu la Torati katika tafsiri nyingine)



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi..
Mfalme wa Amani,Mlinzi wetu,Muweza wa Yote..
Baba wa Yatima Mume wa Wajane,Alfa na Omega..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Utukuzwe Baba wa Mbinguni,Usifiwe Mungu wetu,Uhimidimiwe Baba..
Hakuna kama wewe,Matendo yako ni ya Ajabu Unatosha Mungu wetu..

Sikieni mafundisho yangu, enyi watu wangu; yategeeni sikio maneno ya kinywa changu. Nitasema nanyi kwa mafumbo, nitasema mambo yaliyofichika tangu kale; mambo tuliyoyasikia na kuyajua, mambo ambayo wazee wetu walitusimulia. Hatutawaficha watoto wetu; ila tutakisimulia kizazi kijacho matendo matukufu ya Mwenyezi-Mungu na uwezo wake; tutawaambia maajabu yake aliyotenda. Aliwapa wazawa wa Yakobo masharti, aliweka sheria katika Israeli, ambayo aliwaamuru wazee wetu wawafundishe watoto wao; ili watu wa kizazi kijacho, watoto watakaozaliwa baadaye, wazijue, nao pia wawajulishe watoto wao, ili wamwekee Mungu tumaini lao, wasije wakasahau matendo ya Mungu, bali wazingatie amri zake.


Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuchagua tena kuendelea kuiona Leo hii..
Si kwa nguvu zetu wala si kwa ujuzi/utashi wetu sisi kuwa hivi tulivyo..
Ni kwa neema /rehema zako Muumba wetu..

Tunakuja mbele zako Baba yetu tukijishusha,tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mungu wetu..
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale walio tukosea..
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu Baba utufunike na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Yahweh tunaomba utubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu wetu tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Jehovah tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba ukatupe kama inavyokupendeza wewe..

Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema Mungu wetu tukatumike kama ipasavyo.

Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu, mshangilieni Mungu wa Yakobo; vumisheni wimbo wa shangwe, pigeni ngoma, chezeni zeze na kinubi cha sauti nzuri. Pigeni tarumbeta kutangaza mwezi mwandamo, na pia mwezi mpevu, wakati wa sikukuu yetu. Hiyo ndiyo kanuni katika Israeli; hilo ndilo agizo la Mungu wa Yakobo. Aliwapa watu wa Israeli agizo hilo, alipoishambulia nchi ya Misri. Nasikia sauti nisiyoitambua ikisema: “Mimi nilikutua mizigo yako mabegani, nilikuondolea matofali uliyochukua mikononi. Ukiwa shidani uliniita, nami nikakuokoa. Nilikujibu nikiwa mafichoni katika ngurumo. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba. Enyi watu wangu, sikieni onyo langu. Laiti ungenisikiliza, ee Israeli! Asiwepo kwako mungu wa kigeni; usiabudu kamwe mungu mwingine. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri. Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha. “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitaka kabisa. Hivyo, nikawaacha wabaki na ukaidi wao; wafuate mashauri yao wenyewe. Laiti watu wangu wangenisikiliza! Laiti Israeli angefuata njia yangu! Ningewashinda maadui zao haraka; ningenyosha mkono dhidi ya wadhalimu wao. Wanichukiao wangenipigia magoti kwa hofu, na adhabu yao ingekuwa ya milele. Lakini wewe ningekulisha kwa ngano bora, ningekushibisha kwa asali ya mwambani.”


Tazama wenye shida/tabu na wote wanaopitia magumu/majaribu..
Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye kimwili na kiroho pia..
ukawape neema ya kukujua wewe na kusimamia Neno lako..
Baba wa Mbinguni ukaonekane kwenye taabu zao..

Jinsi gani yanavyopendeza makao yako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu! Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai. Hata shomoro wamepata makao yao, mbayuwayu wamejenga viota vyao, humo wameweka makinda yao, katika madhabahu zako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu! Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wakiimba daima sifa zako. Heri watu wanaopata nguvu zao kwako, wanaotamani kwenda kuhiji mlimani kwako. Wapitapo katika bonde kavu la Baka, hulifanya kuwa mahali pa chemchemi, na mvua za vuli hulijaza madimbwi. Wanaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi; watamwona Mungu wa miungu huko Siyoni. Usikie sala yangu ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi; unitegee sikio, ee Mungu wa Yakobo. Ee Mungu, umwangalie kwa wema ngao yetu mfalme, umtazame huyo uliyemweka wakfu kwa mafuta. Siku moja tu katika maskani yako, ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali kusimama mlangoni pa nyumba yako, kuliko kuishi nyumbani kwa watu waovu. Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu. Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, heri mtu yule anayekutumainia wewe!

Tumaini,Amani,Upendo,Uzima, Maarifa,Hekina na Busara vina wewe Mungu wetu..
Asante Mungu wetu,Sifa na utukufu tunakurudishia wewe..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana sana wapendwa/waumgwa kwakuwa nami
Mungu andelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye..
Nawapenda.



Miaka kadhaa jangwani

1“Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu. 2Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia, 3‘Mmetangatanga vya kutosha katika nchi hii ya milima; sasa geukeni mwelekee kaskazini. 4Mko karibu kupita katika nchi ya milima ya Seiri, nchi ya ndugu zenu wazawa wa Esau. Hao watawaogopeni, lakini muwe na tahadhari, 5msipigane nao kwa sababu sitawapeni sehemu yoyote ya nchi yao. Sitawapeni hata mahali padogo pa kukanyaga. Nchi hiyo ya milima ya Seiri nimewapa wazawa wa Esau iwe mali yao. 6Mkitaka chakula au maji kutoka kwao, lazima mnunue.’
7“Basi, kumbukeni jinsi Mwenyezi-Mungu Mungu wenu alivyowabariki katika kila jambo mlilofanya. Aliwatunza mlipokuwa mnatangatanga katika jangwa hili kubwa. Amekuwa pamoja nanyi miaka hii yote arubaini na hamkupungukiwa kitu chochote.
8“Hivyo tuliendelea na safari yetu, tukawapita ndugu zetu, wazawa wa Esau ambao waliishi Seiri, tukaiacha nyuma ile njia ya Araba na pia miji ya Elathi na Esion-geberi. Kisha tukageuka tukafuata njia ya kupitia nyika ya Moabu. 9Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Usiwasumbue watu wa Moabu, wala usipigane nao maana sitawapeni sehemu yoyote ya nchi yao. Ila eneo hilo la Ari nimewapa hao wazawa wa Loti liwe mali yao.’ 10(Hapo zamani hiyo nchi ya Ari ilikuwa imekaliwa na watu wengi, wenye nguvu na ambao walikuwa warefu kama Waanaki. 11Kama vile Waanaki, watu hawa walijulikana pia kama Warefai, lakini Wamoabu waliwaita Waemi. 12Wahori pia waliishi huko Seiri hapo awali, lakini wazawa wa Esau waliwafukuza na kuwaangamiza, kisha wao wenyewe wakakaa katika eneo hilo badala yao. Waisraeli walifanya vivyo hivyo katika nchi ile ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa iwe mali yao).
13“Mwenyezi-Mungu akatuambia: ‘Ondokeni sasa, mvuke kijito Zeredi’. Basi, tukavuka kijito cha Zeredi. 14Miaka thelathini na nane ilikuwa imepita tangu kuondoka Kadesh-barnea mpaka kuvuka kijito cha Zeredi. Wakati huo, kizazi chote cha wale watu wa umri wa kwenda vitani kilikuwa kimetoweka kulingana na jinsi Mwenyezi-Mungu alivyowaapia. 15Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwakabili ili kuwaangamiza huko kambini, hata wote wakaisha.
16“Basi, watu hao wote wenye umri wa kwenda vitani walipokwisha aga dunia, 17Mwenyezi-Mungu aliniambia, 18‘Leo hii mtauvuka mpaka wa Moabu kwa kupitia nchi ya Ari. 19Mtaifikia nchi ya Waamoni. Msiwasumbue wala msipigane nao kwa kuwa sitawapeni sehemu yoyote ya hao wazawa wa Amoni; iwe mali yenu. La! Hao ni wazawa wa Loti, na nimewapa hiyo nchi iwe mali yao.’”
20(Nchi hiyo inajulikana pia kama nchi ya Warefai. Warefai walikuwa wanaishi huko hapo zamani; Waamoni waliwaita hao Wazamzumi. 21Walikuwa watu wengi, wenye nguvu na warefu kama Waanaki. Lakini Mwenyezi-Mungu aliwaangamiza walipofika Waamori ambao walichukua nchi yao wakaishi humo badala yao. 22Mwenyezi-Mungu alifanya kama alivyowafanyia wazawa wa Esau, Waedomu, ambao wanaishi katika nchi ya Seiri. Aliwaangamiza Wahori wakati Waedomu walipofika huko, wakainyakua nchi yao na kuishi humo hadi leo. 23Waavi walikuwa hapo awali wakiishi katika vijiji vya mwambao wa Mediteranea mpaka Gaza. Wakaftori kutoka kisiwa cha Kaptori wakawaangamiza, wakaishi humo badala yao).
24“Kisha Mwenyezi-Mungu alituamuru: ‘Haya! Anzeni safari. Vukeni bonde la Arnoni. Mimi nimemtia mikononi mwenu Sihoni, mfalme wa Waamori wa Heshboni na nchi yake. Mshambulieni na kuanza kuimiliki nchi yake. 25Leo nitaanza kuwafanya watu wote duniani wawe na woga na hofu juu yenu; watasikia habari zenu nao watatetemeka na kufadhaika.’

Waisraeli wamshinda mfalme Sihoni

(Hes 21:21-30)

26“Basi, nikatuma watu kutoka jangwa la Kedemothi waende kwa mfalme Sihoni wa Heshboni na ujumbe ufuatao wa amani: 27‘Turuhusu tupite katika nchi yako. Tutapitia barabarani na kwenda moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto. 28Chakula chetu tutakinunua kwako na maji ya kunywa pia. Tunachoomba tu ni ruhusa ya kupita kwa miguu nchini mwako, 29tuvuke mto Yordani na kuingia katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu anatupatia. Wazawa wa Esau wanaoishi Seiri na Wamoabu waishio Ari walituruhusu pia kupita katika nchi yao’.
30“Lakini Sihoni, mfalme wa Heshboni, hakuturuhusu tupite nchini mwake. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimfanya awe na kichwa kigumu na mkaidi wa moyo, ili tumshinde na kuchukua nchi yake ambayo tunaimiliki hadi leo.
31“Halafu Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Tazama, nimeanza kumtia mfalme Sihoni na nchi yake mikononi mwenu; anzeni kuichukua nchi yake na kuimiliki’. 32Kisha Sihoni alitoka na watu wake wote kupigana nasi karibu na mji wa Yahasa. 33Naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, akamtoa, tukamshinda yeye, watoto wake na watu wake wote. 34Tukaiteka na kuiharibu miji yake yote, tukaua wanaume na wanawake na watoto; hatukumwacha mtu yeyote hai. 35Nyara zetu zilikuwa tu mifugo na mali yote tuliyokuta mijini. 36Kuanzia Aroeri, mji ulio ukingoni mwa bonde la Arnoni na mji ulio ndani ya bonde hili mpaka Gileadi, hakuna mji wowote uliokuwa imara hata tukashindwa kuuteka. Mwenyezi-Mungu aliitia yote mikononi mwetu. 37Lakini hatukukaribia nchi ya Waamoni au ukingoni mwa mto Yaboki wala katika miji ya nchi ya milima wala sehemu yoyote ile ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alitukataza.


Kumbukumbu la Sheria 2:1-37

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday, 23 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi; Leo tunaanza kitabu cha- Kumbukumbu la Sheria 1 (Kumbukumbu la Torati katika tafsiri nyingine)




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyha Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru na kumsifu Daima..
Tunamshukuru Mungu wetu kwa kutuongoza na kutupa neema ya kuweza kujifunza katika kitabu cha Hesabu,Nimatumaini yangu wewe unayepitia hapa kuna kitu umejifunza..
Tunamuomba Mungu atupe neema ya kuweza kujifunza kitabu hiki
Kitabu hiki kinaitwa Kumbukumbu la Sheria (Kumbukumbu la Torati katika tafsiri nyingine)

Mungu wetu akatupe macho ya rohoni,Masikio ya kusikia sauti yake..
Tukasome na kumaanisha tukafaidike sisi na kuwafaidisha wengine..
Akatupe Shauku/hamu,kiu ya kupenda kujifunza zaidi..
Tupate kuelewa na kusimamia Neno lake Amri na Sheria zake..
Ee Baba utuongoze..

Basi, kwa vile ahadi ya kuingia mahali pa pumziko bado ipo, na tuogope ili yeyote kati yenu asije akashindwa kupata pumziko hilo. Maana Habari Njema imehubiriwa kwetu kama vile ilivyohubiriwa kwa hao watu wa kale. Lakini ujumbe huo haukuwafaa chochote, maana waliusikia lakini hawakuupokea kwa imani. Basi, sisi tunaoamini tunapata pumziko hilo aliloahidi Mungu. Kama alivyosema: “Nilikasirika, nikaapa: ‘Hawataingia mahali pangu pa pumziko.’” Mungu alisema hayo ingawa kazi yake ilikuwa imekwisha malizika tangu alipoumba ulimwengu. Maana Maandiko yasema mahali fulani kuhusu siku ya saba: “Mungu alipumzika siku ya saba, akaacha kazi zake zote.” Tena jambo hili lasemwa pia: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko.” Basi, hiyo ahadi ya kuingia bado ipo, maana wale waliohubiriwa Habari Njema pale awali walishindwa kuingia humo kwa sababu walikosa kutii. Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.” Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine. Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Maana, kila aingiaye mahali pa pumziko la Mungu atapumzika kutoka katika kazi yake kama vile pia Mungu alivyopumzika kutoka kazi yake. Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao. Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu. Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu. Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu. Huyu Kuhani Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi. Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.

Tunakushuru Ee Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba wa Mbingu na  Nchi na vyote vilivyomo Baba ni mali yako..
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe,Uabudiwe Milele na Milele..
Tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Baba wa Upendo..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijishusha,tukijinyeyekeza na kujiachiliamikononi mwako Jehovah..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya..
Kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi  utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..

Ee Mwenyezi-Mungu, utusikie; utusamehe ee Mwenyezi-Mungu. Ee Mwenyezi-Mungu, kwa hisani yako utusikie na kuchukua hatua, wala usikawie, ee Mungu wangu, kwa ajili ya mji huu na watu hawa wanaoitwa kwa jina lako!
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu,Utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu na mpinga Kristo zishindwe katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo..

Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba mpinzani wa Kristo anakuja, na sasa wapinzani wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu. Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu. Nyinyi, lakini, mlipata kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo, na hivyo mnaujua ukweli. Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli. Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Kristo. Mtu wa namna hiyo ni mpinzani wa Kristo – anamkana Baba na Mwana. Maana yeyote anayemkana Mwana, anamkana pia Baba; na yeyote anayemkubali Mwana, anampata Baba pia. Basi, ujumbe ule mliousikia tangu mwanzo na ukae mioyoni mwenu. Kama ujumbe huo mliousikia tangu mwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtaishi daima katika umoja na Mwana na Baba. Na ahadi aliyotuahidia sisi ndiyo hii: Uhai wa milele. Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha nyinyi. Lakini, kwa upande wenu nyinyi, Kristo aliwatia mafuta kwa Roho wake. Na kama Roho huyo akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana yeye anawafundisheni kila kitu, na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi, shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo. Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu siku ya kuja kwake. Mnajua kwamba Kristo ni mwadilifu kabisa; basi, mnapaswa kujua pia kwamba kila mtu atendaye mambo adili ni mtoto wa Mungu.

Yahweh tunaomba ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..

Taabu na mateso
(Marko 13:3-13; Luka 21:7-19)



Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?” Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi. Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado. Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi. Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto. “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu. Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana. Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi. Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa. Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.

Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupatekupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Jehovah tunaomba ukatubariki na ukabariki kazi za mikono yetu..
ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwabariki wenyekuhitaji..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Mungu wetu tunaweka mikononi mwako Nyumba zetu/Ndoa,watoto/familia ,ndugu na wote wanaotuzunguka..
Baba wa mbinguni ukawatunze na kuwalinda,ukawafunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Mfalme wa Amani tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu wote wataabikao,wenye shida/tabu ,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,walio katika vifungo vya yule mwovu...
Mungu wetu ukawaponye kimwili na kiroho pia,ukawaokoe na kuwapa neema ya kukujua wewe,wakasimamie Neno lako wakati wote..


Neema,Baraka,Uponyaji,Upendo,Tumaini,Amani na vyote vinavyoponya mwili na roho vina wewe Mungu wetu..


Asante kwa pendo lako kwetu,Ulinzi wako wakati wote..
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa kwa kuwa nami..
Baba wa upendo akawe nayi daima..
Nawapenda.


Utangulizi

1Kitabu hiki kina maneno ambayo Mose aliwaambia watu wote wa Israeli wakati walipokuwa nyikani mashariki ya mto Yordani. Walikuwa katika bonde la Yordani karibu na Sufu, kati ya mji wa Parani upande mmoja na mji wa Tofeli, Labani, Hazerothi na Dizahabu, upande mwingine. 2(Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka mlima Horebu hadi Kadesh-barnea kwa njia ya mlima Seiri.) 3Siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja, mwaka wa arubaini, baada ya kutoka Misri, Mose aliwaambia watu kila kitu ambacho Mwenyezi-Mungu alimwamuru awaambie. 4Taz Hes 2:21-35 Alifanya hivyo baada ya kumshinda mfalme Sihoni wa Waamori ambaye alikuwa anakaa mjini Heshboni, na mfalme Ogu wa Bashani ambaye alikuwa anakaa mjini Ashtarothi na Edrei. 5Mose alichukua jukumu la kuwaelezea watu sheria ya Mungu wakati walipokuwa ngambo ya pili ya mto Yordani.
Aliwaambia hivi: 6“Tulipokuwa mlimani Sinai, Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu alituambia hivi: ‘Mmekaa muda wa kutosha kwenye mlima huu; 7sasa vunjeni kambi yenu mwendelee na safari. Nendeni kwenye nchi ya milima ya Waamori na maeneo ya nchi jirani katika Araba, kwenye milima na mabonde, huko Negebu na sehemu za pwani; naam, nendeni mpaka nchi ya Kanaani, na nchi ya Lebanoni, hadi kwenye ule mto mkubwa wa Eufrate. 8Nchi hii yote nimeiweka mbele yenu. Basi, nendeni mkaimiliki nchi hiyo ambayo mimi Mwenyezi-Mungu niliapa kuwapa wazee wenu Abrahamu, Isaka, Yakobo na wazawa wao.’”

Mose ateua waamuzi

(Kut 18:13-27)

9Mose akawaambia watu, “Tulipokuwa bado mlimani Sinai, mimi niliwaambieni hivi: ‘Jukumu la kuwaongozeni ni kubwa mno kwangu mimi peke yangu. 10Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewafanya muwe wengi; leo mmekuwa wengi kama nyota za mbinguni. 11Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi! 12Lakini mimi peke yangu nitawezaje kuchukua jukumu hilo zito la kusuluhisha ugomvi wenu? 13Chagueni kutoka katika kila kabila watu wenye hekima, busara na ujuzi ili niwateue wawe viongozi wenu.’ 14Nyinyi mlikubali, mkanijibu hivi: ‘Jambo ulilosema ni la busara’. 15Hivyo niliwachukua wale viongozi wenye hekima, busara na ujuzi ambao mliwachagua kutoka katika makabila yenu, nikawaweka kuwa viongozi wenu. Niliwaweka wengine kuwa makamanda wa makundi ya watu elfuelfu, ya watu miamia, ya watu hamsinihamsini na ya watu kumikumi. Nilichagua pia maofisa wengine wa kuchunga kila kabila.
16“Wakati huohuo niliwapa waamuzi wenu maagizo yafuatayo: ‘Sikilizeni kesi za watu wenu. Toeni hukumu za haki katika visa vya watu wenu, kadhalika na mizozo ya wageni waishio pamoja nanyi. 17Msimpendelee mtu yeyote katika kutoa hukumu; mtawasikiliza bila upendeleo, wakubwa kwa wadogo. Msitishwe na mtu yeyote, maana hukumu mnayotoa inatoka kwa Mungu. Kesi yoyote ikiwa ngumu zaidi kwenu, ileteni kwangu, nami nitaisikiliza.’ 18Wakati huohuo, niliwaagizeni mambo yote mnayopaswa kufanya.

Uasi wa Israeli kuhusu nchi ya ahadi

(Hes 13:1-33)

19“Basi, kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru, tulianza safari yetu kutoka mlima Horebu, tukapita katika lile jangwa kubwa la kutisha mnalolijua, kwa kufuata njia inayoelekea nchi ya milima ya Waamori. Tulipofika Kadesh-barnea, 20mimi niliwaambieni: ‘Sasa mmefika katika nchi ya milima ya Waamori ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupatia. 21Tazameni, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ameiweka nchi hii mbele yenu. Haya! Ingieni, mkaimiliki kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wenu alivyowaambia. Msiogope wala msifadhaike!’
22“Kisha nyote mlikuja karibu nami mkaniambia, ‘Tutume watu watutangulie, waipeleleze nchi, halafu warudi kutujulisha njia bora ya kufuata na miji ipi tutaikuta huko.’ 23Jambo hilo lilionekana kuwa jema kwangu, nikawateua watu kumi na wawili, mtu mmoja kutoka katika kila kabila. 24Watu hao walikwenda katika nchi ile ya milima, wakafika kwenye bonde la Eshkoli na kulipeleleza. 25Waliporudi, walituletea baadhi ya matunda ya nchi hiyo na wakatuarifu kwamba nchi hiyo anayotupatia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni nzuri.
26“Lakini nyinyi hamkufuata agizo la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kukataa kwenda katika nchi hiyo. 27Mlinungunika ndani ya mahema yenu mkisema, ‘Mwenyezi-Mungu anatuchukia na ndiyo maana alitutoa nchini Misri. Alitaka kututia mikononi mwa Waamori, atuangamize. 28Kwa nini tuende huko hali tumevunjika moyo kwa hofu? Wametuambia kuwa watu wa huko ni wakubwa na warefu kuliko sisi, na kwamba miji yao ni mikubwa na yenye kuta zifikazo mawinguni. Tena wamesema kwamba waliwaona wale wazawa wa Anaki!’1:28 Anaki: Taz Hes 13:22.
29“Lakini mimi niliwaambieni hivi: ‘Msiwe na hofu wala msiwaogope watu hao.’ 30Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambaye huwatangulia, yeye mwenyewe atapigana kwa ajili yenu kama alivyofanya mbele yenu kule Misri na 31kule jangwani ambako mliona jinsi alivyowabeba safari hiyo yote kama vile baba amchukuavyo mwanawe mpaka mkafika hapa. 32Lakini japo nilisema hayo yote, nyinyi hamkumwamini Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, 33ambaye aliwatangulia njiani na kuwatafutia mahali pa kupiga kambi zenu. Usiku aliwatangulieni kwa moto na mchana kwa wingu, ili kuwaonesha njia.
34“Mwenyezi-Mungu aliyasikia manunguniko yenu, akakasirika, akaapa akisema: 35‘Hakuna hata mmoja wenu katika kizazi hiki kiovu atakayeingia katika nchi ile nzuri niliyoahidi kuwapa wazee wenu. 36Kalebu mwana wa Yefune, ndiye tu atakayeiona; nami nitampatia nchi hiyo aliyoikanyaga iwe yake yeye na wazawa wake kwa kuwa amekuwa mwaminifu kabisa kwangu.’ 37Mwenyezi-Mungu alinikasirikia mimi pia kwa sababu yenu, akasema, ‘Hata wewe Mose hutaingia katika nchi hiyo. 38Lakini msaidizi wako Yoshua mwana wa Nuni, ataingia humo. Basi, mtie moyo kwani yeye atawaongoza watu wa Israeli waimiliki nchi hiyo’. 39Kisha Mwenyezi-Mungu akatuambia sisi sote, ‘Hao watoto wenu mnaoogopa kwamba watakuwa nyara za adui zenu, naam hao walio wadogo ambao hawajui bado kupambanua kati ya mema na mabaya, hao ndio watakaoingia huko, nami nitawapa wao nchi hiyo iwe yao. 40Lakini nyinyi, geukeni na kurudi jangwani kuelekea Bahari ya Shamu.’
41“Kisha mkanijibu, ‘Sisi tumemtendea dhambi Mwenyezi-Mungu, lakini sasa tutakwenda na kupigana kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru’. Hivyo, kila mmoja wenu akajitayarisha kupigana vita; maana mlifikiri kwamba lingekuwa jambo rahisi kuivamia nchi hiyo ya milima. 42Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Waambie hao watu wasiende kupigana kwa sababu sipo pamoja nao; wasiende, wasije wakashindwa na adui zao’. 43Basi, mimi niliwaambieni hivyo, lakini nyinyi hamkusikia. Badala yake mlikataa kufuata agizo la Mwenyezi-Mungu, bila kujali mkaingia katika nchi hiyo ya milima. 44Hapo, Waamori waliokuwa wanaishi katika eneo hilo la milimani wakateremka kuwashambulia na kama wafanyavyo nyuki wakawapiga huko Seiri mpaka Horma. 45Ndipo mliporudi, mkamlilia Mwenyezi-Mungu, lakini Mwenyezi-Mungu hakuwasikiliza wala hakuwajali. 46Basi, mkabaki huko Kadeshi kwa muda mrefu ambao mlikaa huko.

Kumbukumbu la Sheria 1:1-46


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday, 22 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..36-Mwisho wa kitabu cha Hesabu,Mungu wetu yu Mwema..




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Mungu wetu yu mwema sana..Tumshukuru Mungu katika yote..
Mtakatifu..Mtakatifu..Mtakatifu..!!
Baba wa Mbinguni,Mungu wetu na Muumba wetu..
Kimbilio letu na Mponyaji wetu,Mungu wa Wajane na Yatima..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Muweza wa yote,Baba wa Upendo,Baba wa Rehema..
Unastahili sifa Baba wa Mbinguni,Unastahili kuabudiwa Mungu wetu..
Hakuna kama wewe,wewe ni Alfa na Omega..

Jehovah..!Jehovah Nissi..!Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Jireh..!Jehovah Shalom..!

Yahweh..!El Shaddai..!El Olam..!El him..!Adonai..!!!!!!!
Emanueli...Mungu pamoja nasi..!Unatosha Baba wa Mbinguni..!


Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu. Kwa hiyo hatutaogopa chochote, dunia ijapoyeyuka na milima kutikisika kutoka baharini; hata kama bahari ikichafuka na kutisha, na milima ikatetemeka kwa machafuko yake. Kuna mto ambao maji yake hufurahisha mji wa Mungu, makao matakatifu ya Mungu Mkuu. Mungu yumo mjini humo, nao hauwezi kutikiswa; Mungu ataupa msaada alfajiri na mapema. Mataifa yaghadhibika na tawala zatikisika; Mungu anguruma nayo dunia yayeyuka. Mwenyezi-Mungu wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu. Njoni mwone matendo ya Mwenyezi-Mungu; oneni maajabu aliyoyafanya duniani. Hukomesha vita popote duniani, huvunjavunja pinde na mikuki, nazo ngao huziteketeza. Asema: “Nyamazeni na kujua kuwa mimi ni Mungu! Mimi natukuka katika mataifa yote; mimi natukuzwa ulimwenguni kote!” Mwenyezi-Mungu wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..

Si kwa uwezo wetu wala si kwanguvu zetu Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo..
Ni kwa Neema/rehema zako Jehovah..
Tunajishusha mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni..tunaomba utusamehe dhambi zetu zote ..
Tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mfalme wa Amani ukatamalaki na kutuatamia katika Nyumba zetu/Ndoa,watoto/familia,Ndugu/jamaa na wote wanaotuzunguka..
Baba wa Mbingu ukatuguse na mkono wako wenye nguvu..
Ukatutakase Miili yetu na Akili zetu na ukatufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atautwaa upanga wake mkubwa, mkali na imara, na kuliadhibu dude Lewiyathani joka lirukalo na danganyifu; Mwenyezi-Mungu ataliua joka liishilo baharini. Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atasema hivi: “Imbeni utenzi wa shamba langu zuri la mizabibu! Mimi, Mwenyezi-Mungu, ni mkulima wake; nalimwagilia maji kila wakati, ninalilinda usiku na mchana, lisije likaharibiwa na mtu yeyote. Silikasirikii tena shamba hili; kama miiba na mbigili ingelilivamia, mimi ningepambana nayo na kuichoma moto. Maadui za watu wangu wakitaka ulinzi wangu, basi, na wafanye amani nami; naam, wafanye amani nami.” Itakuja siku wazawa wa Yakobo watashika mizizi; naam, watu wa Israeli watachanua na kuchipua, na kuijaza dunia yote kwa matunda. Mungu hakuwaadhibu Waisraeli vikali kama alivyowaadhibu maadui wake; Waisraeli waliopotea vitani, ni wachache kuliko wale wa maadui zake. Aliwaadhibu watu wake kwa kuwapeleka uhamishoni. Wakati wa upepo mkali wa mashariki, aliwaondoa kwa kipigo kikali. Hivi ndivyo uovu wa wazawa wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo dhambi yake itakavyofutwa kabisa: Ataziharibu madhabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa; Ashera, wala madhabahu za kufukizia ubani hazitabaki. Mji ule wa ngome sasa umekuwa mtupu, umeachwa na kuhamwa kama jangwa, humo ndama wanalisha na kupumzika. Matawi ya miti yamekauka na kuvunjika; kina mama huyaokota wakawashia moto. Watu hawa hawajaelewa kitu, kwa hiyo Mungu, Muumba wao, hatawahurumia, yeye aliyewafanya, hatawafadhili. Siku hiyo, kutoka mto Eufrate hadi mpakani mwa Misri, Mwenyezi-Mungu ataipura nafaka yake, nanyi Waisraeli mtakusanywa mmojammoja. Siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa na watu wote wa Israeli waliopotea nchini Ashuru au waliotawanywa nchini Misri watarudi na kumwabudu Mwenyezi-Mungu juu ya mlima mtakatifu huko Yerusalemu.


Roho Mtakatifu akatuongoze katika maisha yetu,tupate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Mungu wetu tunaomba Ukatubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Baba wa Mbinguni tukatende sawasawa na mapezni yako..

Vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Mungu wetu ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Yahweh nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji....


Tazama wenye Shida/tabu,Mungu wetu na wote wanaopitia magumu/majaribu,walio katika vifungo mbalimbali Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,wakapate kupona kimwili na kiroho pia..

wakaijue kweli yako na kusimamia Neno lako,Amri na sheria zako..nazo ziwaweke huru..



Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia. Enyi watu wa Siyoni, enyi watu wa Yerusalemu, hakika nyinyi hamtaomboleza tena. Kweli Mungu atawahurumia; mara tu atakaposikia kilio chenu atawaitikeni. Ingawa Bwana atawalisha taabu na kuwanywesha dhiki, yeye ndiye Mwalimu wenu na hatajificha tena; nanyi mtamwona kwa macho yenu wenyewe. Mkienda kulia au kushoto, mtasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Njia ni hii; ifuateni.” Mtavifanya haramu vinyago vyenu vya miungu vilivyopakwa fedha na sanamu zenu zilizopakwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitu najisi, mkisema, “Poteleeni mbali!” Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi. Mafahali na punda wenu wa kulimia watapata malisho yaliyochambuliwa vizuri na kutiwa chumvi. Wakati utakapofika ambapo maadui watauawa na ngome zao kubomolewa, vijito vya maji vitatiririka kutoka kila mlima na kilima. Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwanga wa jua utakuwa mara saba ya mwanga wake wa kawaida, kana kwamba mwanga wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Mwenyezi-Mungu atakapoyafunga na kuyaponya majeraha aliyowaletea watu wake.


Mungu wetu ukaonekane popote tulipo,tupitapo,tunenapo Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..

Asante Mungu wetu kwa neema hii yakujifunza Neno lako..
Mungu wetu likakae nasi na likawe faida kwetu na kwa wengine..
Tukafuate na kiusimamia Neno lako na si maneno ya Dunia hii..
Ukatupe Neema ya kuendelea kujifunza zaidi..Tukawe na kiu na shauku ya kukujua zaidi..Ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako Mungu wetu..



Tegeni sikio msikilize ninayowaambieni; sikilizeni kwa makini hotuba yangu. Je, alimaye ili kupanda hulima tu? Je, huendelea kulima na kusawazisha shamba lake? La! Akisha lisawazisha shamba lake, hupanda mbegu za bizari na jira, akapanda ngano na shayiri katika safu, na mipakani mwa shamba mimea mingineyo. Mtu huyo huwa anajua la kufanya, kwa sababu Mungu wake humfundisha. Bizari haipurwi kwa mtarimbo wala jira kwa gari la ng'ombe! Ila bizari hupurwa kwa kijiti na jira kwa fimbo. Mkulima apurapo ngano yake, haendelei kuipura mpaka kuvunja punje zake. Anajua jinsi ya kuipura kwa gurudumu, bila kuziharibu punje za ngano. Ujuzi huu nao watoka kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mipango yake Mungu ni ya ajabu, hekima yake ni kamilifu kabisa.
Mungu wetu ukatuongoze vyema tunapoanza kitabu kingine..
Asante Mungu wetu kwa Neema ya kuweza kupitia/kusoma kitabu hiki tulichomaliza leo cha Hesabu Mungu wetu  na isiwe Mwisho utupe neema ya kukirudia mara nyingi na kuendelea kujifunza zaidi..


Baba wa Mbinguni ukawaguse na wengine wanaozongwa na kukosa muda wa kusoma Neno lako..Ukawape Neema ya kukutafuta na ukawape macho ya kuona na masikio ya kusikia..




Bado kidogo tu, msitu wa Lebanoni utageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa msitu. Siku hiyo viziwi watasikia ujumbe ukisomwa kitabuni na kutoka gizani vipofu wataanza kuona. Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu, na maskini wa watu watashangilia kwa furaha kwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli. Majitu makatili yataangamizwa, wenye kumdhihaki Mungu watakwisha, wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa. Watatoweka wale wanaopotosha kesi ya mtu mahakamani, watu wanaowafanyia hila mahakimu na wasemao uongo kuwanyima haki yao wasio na hatia. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu, asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo: “Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena, hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu. Watakapowaona watoto wao, watoto niliowajalia mimi mwenyewe, watalitukuza jina langu mimi Mtakatifu wa Yakobo; watakuwa na uchaji kwangu mimi Mungu wa Israeli. Waliopotoka rohoni watapata maarifa na wenye kununa watakubali kufunzwa.”


Si kwa nguvu zetu wala utashi wetu ni kwa neema zako Mungu  wetu..
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!

Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakua pamoja..
Mungu wetu yu mwema sana ..!

Je wewe unayesoma hapa leo umefaidika/umejifunza chochote?
Kuna tulieanza naye Mwanzo mpaka sasa tunaenda pamoja?
kama siyo unaweza kutenga muda wako ukaanzia nyuma ili tuweze kwenda vyema..

ikikupendeza na Muombe Mungu akupe neema hiyo..

Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea katika maisha yenu
Msipungukiwe katika mahitaji yenu Baba wa Mbinguni akawape kama inavyompendeza yeye..
Nawapenda.

Urithi wa wanawake walioolewa

1Viongozi wa jamaa katika ukoo wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, mwana wa Yosefu, walikwenda kuzungumza na Mose na viongozi wengine wa koo za Waisraeli. 2Taz Hes 27:7 Wakasema, “Bwana wetu, Mwenyezi-Mungu alikuamuru kuwagawia watu wa Israeli nchi kwa kura, kuwa urithi wao; alikuamuru pia uwape binti za Selofehadi ndugu yetu urithi wa baba yao. 3Lakini wao wakiolewa na Waisraeli wa makabila mengine, urithi wao utatoka kwetu na kuwaendea watu wa kabila watakamoolewa; kwa hiyo urithi wetu sisi utapungua. 4Katika sikukuu ya ukumbusho urithi wao utahesabiwa pamoja na ule wa kabila watakamoolewa na hivyo kabila letu halitapata urithi huo tena.”
5Basi, Mose akawapa Waisraeli agizo lifuatalo kutoka kwa Mwenyezi-Mungu, akawaambia, “Watu wa ukoo wa kabila la Yosefu,36:5 kabila la Yosefu: Yaani ukoo wa Manase, Taz Hes 36:12. wamesema ukweli. 6Na hivi ndivyo anavyoamuru Mwenyezi-Mungu kuhusu binti za Selofehadi; wako huru kuolewa na mtu yeyote wampendaye, lakini waolewe katika kabila lao, 7ili urithi wa Waisraeli usihamishiwe kwa kabila lingine; kila Mwisraeli atazingatia urithi wa kabila lake. 8Mwanamke yeyote mwenye urithi katika kabila mojawapo la Israeli ni lazima aolewe na mtu wa kabila lake, ili kila Mwisraeli achukue urithi wa babu zake. 9Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaohamishwa kutoka kabila moja hadi jingine. Kila kabila la Waisraeli litashikilia urithi wake.”
10Binti za Selofehadi walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. 11Wote: Mala, Tirza, Hogla, Milka na Noa wakaolewa na binamu zao. 12Waliolewa katika jamaa za ukoo wa Manase mwana wa Yosefu, na urithi wao ukabaki katika kabila la baba yao.
13Hizo ndizo amri na maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli kwa njia ya Mose katika tambarare za Moabu, ngambo ya Mto Yordani karibu na mji wa Yeriko

Hesabu36;1-13


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday, 21 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..35


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu, Baba yetu ametupa kibali cha kuendelea kuiona,Mfalme wa Amani tunaanza nawewe kwa kila jambo..

Asante Baba yetu Mungu wetu,Muumba wa Mbingu na Nchi..
Jehovah..!Yahweh..!Baba wa Upendo,Baba wa Rehema,Baba wa Baraka..
Muweza wa yote,Alfa na Omega..!Hakuna kama wewe Mungu wetu..
Unastahili sifa,Unastahili kuabudiwa..
Utukuzwe Mungu wetu,Uhimidiwe Baba wa Mbinguni..
Unatosha Mungu wetu..!

Tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine..Mfalme wa Amani tunaomba ukatawale katika maisha yetu..
Mungu wetu tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea.
Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunungunika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.” Yesu akawajibu kwa mfano: “Hivi, mmoja wenu akiwa na kondoo 100, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate. Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha. Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.’ Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu. “Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, ataifagia nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate. Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake na kusema, ‘Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.’ Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu.” Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu mmoja mwenye watoto wawili wa kiume. Yule mdogo alimwambia baba yake: ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Naye akawagawia mali yake. Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo. Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika. Akaomba kazi kwa mwananchi mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe. Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu. Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa? Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu. “Mwanae akamwambia: ‘Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.’ Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu! Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea! Kwa sababu huyu mwanangu; alikuwa amekufa, kumbe yu hai; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’ Wakaanza kufanya sherehe. “Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani, akasikia vifijo na ngoma. Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: ‘Kuna nini?’ Huyo mtumishi akamwambia: ‘Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.’ Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie. Lakini yeye akamjibu: ‘Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu! Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.’ Baba yake akamjibu: ‘Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako. Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’”




Ndugu zangu Mungu wetu atupe neema ya kuweza kuwasamehe wengine ili nasi atusamehe..
Haijalishi umepitia nini,umeumizwa kiasi gani,umetendwaje..
Tumuombe Mungu atupe roho ya kusamehe na kumaliza..
Atupe neema ya kuchukuliana na kuwa makini tutakapo maliza jambo hilo ili tusirudie tena makosa..
Mangapi tumekwenda kinyume na Mungu?
Mara ngapi tumeanguka na Mungu wetu ametuinua?
Mungu kama angehesabu ni mara ngapi tumekosea leo hii tungekuwa wapi? Jiulize Mungu amekuokoa na mangapi?Mungu amekutendea mangapi ambayo kwa macho au mawazo yako ulishashindwa?
Mungu wetu akatupe neema ya kuonyana kwa hekima na busara..
tukatue mizigo isiyo yetu..Tumuombe Mungu akatende leo na siku zote tukapate kupona rohoni..


Sheria ya Mwenyezi-Mungu ni kamilifu, humpa mtu uhai mpya; masharti ya Mwenyezi-Mungu ni thabiti, huwapa hekima wasio na makuu. Kanuni za Mwenyezi-Mungu ni sawa, huufurahisha moyo; amri ya Mwenyezi-Mungu ni safi, humwelimisha mtu. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni jambo jema, na la kudumu milele; maagizo ya Mwenyezi-Mungu ni sawa, yote ni ya haki kabisa. Yatamanika kuliko dhahabu; kuliko dhahabu safi kabisa. Ni matamu kuliko asali; kuliko asali safi kabisa. Yanifunza mimi mtumishi wako; kuyafuata kwaniletea tuzo kubwa. Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe? Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua. Unikinge mimi mtumishi wako na makosa ya makusudi, usikubali hayo yanitawale. Hapo nitakuwa mkamilifu, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa. Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu na mkombozi wangu!

Mungu wetu tunaomba ukatutakase Miili yetu na Akili zetu na ukatufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Mungu wetu ndiyo mkombozi wetu..

Mungu wetu tunaomba utubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Jehovah tukatende sawasawa na mapenzi yako..

Ukabariki Nyumba zetu/Ndoa,Watoto wetu/familia,Ndugu/jamaa na wote wanaotuzunguka Mungu wetu ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu..

Mungu wetu tusipungukiwe katika mahita yetu Baba wa Mbinguni ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Yahweh ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..

Mfalme wa Amani tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,wagonjwa,wenye shida/tabu na wote waliokatika vifungo mbalimbali Mungu wetu ukawaongoze na kuwapa neema ya kusimamia Neno lako nao wakapate kuwa huru..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ukaonekane Mungu wetu popote tupitapo,tunenapo tukanene yaliyo yako..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama ipasavyo kupitia Neno lako, Amri na sheria zako..

Sifa na utukufu  tunakurudishia Mungu wetu.
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami..
Baba wa upendo akawaongoze katika yote na upendo wenu usiwe bure..
Nawapenda.



Miji ya Walawi

1 Taz Yosh 21:1-42 Mwenyezi-Mungu aliongea na Mose katika tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko, akamwambia, 2“Waamuru Waisraeli kwamba kutokana na urithi watakaomiliki, wawape Walawi miji ya kukaa na sehemu za malisho kandokando ya miji hiyo. 3Miji hiyo itakuwa yao, nao watakaa humo na malisho yake yatakuwa kwa ajili ya ng'ombe na mifugo yao pamoja na wanyama wao wengine. 4Malisho ya maeneo mtakayowapa Walawi kandokando ya miji yataenea kila upande umbali wa mita 450 kutoka kwenye kuta za miji hiyo. 5Kwa hiyo, eneo hilo la malisho litakuwa la mita 900, na litaenea kila upande wa mji, mji wenyewe ukiwa katikati. Eneo hilo litakuwa malisho yao kandokando ya miji yao. 6Mtawapa Walawi miji sita ya makimbilio ambapo mtu akimuua mwenzake bila kukusudia ataruhusiwa kukimbilia. Pamoja na hiyo, mtawapa miji mingine arubaini na miwili. 7Jumla ya miji mtakayowapa Walawi itakuwa arubaini na minane; mtawapa miji hiyo pamoja na sehemu za malisho yake. 8Idadi ya miji mtakayowapa Walawi katika urithi wa Waisraeli itategemea ukubwa wa kabila; kabila kubwa litatoa miji mingi na kabila dogo litatoa michache. Kila kabila litatoa miji yake kwa ajili ya Walawi kulingana na eneo litakalorithi.”

Miji ya makimbilio

(Kumb 19:1-13; Yosh 20:1-9)

9Mwenyezi-Mungu akaongea na Mose, akamwambia, 10Waambie Waisraeli kwamba wakati mtakapovuka mto Yordani na kuingia nchini Kanaani, 11mtachagua miji itakayokuwa miji ya makimbilio ambamo kama mtu akimuua mwenzake bila kukusudia ataweza kukimbilia. 12Miji hiyo itakuwa mahali pa kukimbilia usalama ili huyo mwuaji asiuawe na mwenye kulipiza kisasi kabla ya kuhukumiwa na jumuiya. 13Mtajitengea miji sita kwa ajili ya makimbilio. 14Kati ya miji hiyo sita mtakayoitenga, mitatu iwe mashariki ya Yordani, na mitatu iwe katika nchi ya Kanaani. 15Miji hii itakuwa ya makimbilio kwa ajili ya Waisraeli na wageni wa kudumu au wa muda wanaokaa pamoja nao. Mtu yeyote akimuua mwingine bila kukusudia anaweza kukimbilia huko.
16“Lakini mtu akimpiga mwenzake kwa kitu cha chuma, akafa, mtu huyo ni mwuaji na ni lazima auawe. 17Mtu yeyote akimpiga mwenzake kwa jiwe, akifa, mtu huyo ni mwuaji, na lazima auawe. 18Kama akimpiga mwenzake kwa silaha ya mti ambayo yaweza kusababisha kifo, akafa, mtu huyo ni mwuaji, na ni lazima auawe. 19Jamaa wa karibu wa mtu aliyeuawa atalipiza kisasi. Huyu atakapokutana na huyo mwuaji, atatekeleza hukumu ya kifo.
20“Hali kadhalika, kama mtu anamchukia mwenzake halafu, akamsukuma au kumtupia kitu kwa kumvizia, 21au kwa kumpiga ngumi akafa, basi mtu huyo aliyempiga mwenzake ni mwuaji na ni lazima auawe. Jamaa wa karibu wa mtu aliyeuawa atalipiza kisasi atakapokutana naye.
22“Lakini kama mtu akimsukuma mwenzake kwa ghafla bila chuki au kumtupia kitu bila kumvizia 23au mtu akirusha jiwe linaloweza kusababisha kifo, akamuua mtu bila kukusudia, ingawa hakuwa adui yake wala hakutaka kumdhuru, 24basi, jumuiya itaamua kati ya huyo mwuaji na jamaa ya mtu aliyeuawa anayetaka kulipiza kisasi, kulingana na sheria hizi. 25Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu. 26Lakini huyo aliyeua akitoka nje ya mji aliokimbilia wakati wowote ule, 27halafu jamaa ya mtu aliyeuawa akampata nje ya mipaka ya mji huo wa makimbilio akamuua, huyo hatakuwa na hatia ya kuua. 28Maana huyo aliyeua ni lazima akae ndani ya mji wa makimbilio mpaka kuhani mkuu atakapofariki; lakini baada ya kifo cha kuhani mkuu anaweza kurudi nyumbani.
29“Sheria hizi zitatumika katika vizazi vyenu vyote, mahali popote mtakapokaa.
30 Taz Kumb 17:6, 19:15 “Mtu yeyote atakayeua mtu, atahukumiwa kifo kutokana na ushahidi wa mashahidi wawili au zaidi; mtu yeyote hawezi kuhukumiwa kifo kutokana na ushahidi wa mtu mmoja.
31“Msipokee fidia yoyote kuokoa maisha ya mwuaji aliyepatikana na hatia, akahukumiwa kifo; mtu huyo lazima auawe. 32Msipokee wala msikubali fidia yoyote kutoka kwa mtu aliyekimbilia mji wa makimbilio ili kumruhusu arudi kukaa nyumbani kwake kabla ya kifo cha kuhani mkuu. 33Mkifanya hivyo mtakuwa mnaitia unajisi nchi ambayo mnakaa. Umwagaji damu huitia nchi unajisi, na hakuna sadaka iwezayo kuitakasa nchi iliyofanyiwa mauaji isipokuwa kwa kumuua mwuaji huyo. 34Msiitie unajisi nchi ambayo mnakaa, nchi ambayo mimi ninakaa; maana mimi Mwenyezi-Mungu ninakaa miongoni mwenu Waisraeli.”



Hesabu35;1-34



Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday, 18 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..34



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Asante Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu na Mlinzi wetu,
Baba wa upendo,Baba wa rehema,Kimbilio letu,
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Baba wa Yatima,Mume wa Wajane,Muumba wa Mbingu na Nchi..
Utukuzwe Baba wa Mbinguni,Unastahili sifa Mungu wetu..
Uhimidiwe Mungu wetu,Unatosha Mfalme wa Amani..
Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya Ajabu..!
Hakuna kama wewe Mungu wetu..
Sifa na Utukufu ni wako..
Nakupenda, ee Mwenyezi-Mungu, nguvu yangu! Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tazama jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Mfalme wa Amani..
Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa upendo tunaomba nasi ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote ..
Tukapate kupendana kama Bwana alivyotupenda sisi..
Tukawe na upendo wa kweli na kuheshimiana,kuhurumiana,kusaidiana..
Tukaonyane kwa upendo na hekima..
Busara ikatawale na tukanene yaliyo yako Mungu wetu..

Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda yeye huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi. Nyinyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya ule ujumbe niliowaambieni. Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipobaki katika mzabibu, hali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu. “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote. Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue. Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa. Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu. Mimi nimewapenda nyinyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike. Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Nyinyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. Nyinyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita nyinyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu. Nyinyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapeni chochote mnachomwomba kwa jina langu. Basi, amri yangu kwenu ndiyo hii: Pendaneni.

Tukasimamie Neno lako,Amri na Sheria yako Mungu wetu..
Ukatuepushe na chuki,kiburi,majivuno na kufuata mambo yetu wenyewe ...
Ukatuepushe na mambo yote mabaya ya Dunia hii yaliyo kinyume nawe Mungu wetu..
Ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia..
tukapate kutambua/kujitambu na tukawe na kiasi..

“Kama ulimwengu ukiwachukia nyinyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla ya kuwachukia nyinyi. Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda nyinyi kama watu wake. Lakini kwa vile nyinyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni. Kumbukeni niliyowaambieni: Mtumishi si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na nyinyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia. Lakini hayo yote watawatendeeni nyinyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma. Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi. Anayenichukia mimi, anamchukia na Baba yangu pia. Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakanichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia. Ndiyo maana yale yaliyoandikwa katika sheria yao ni kweli: ‘Wamenichukia bure!’ “Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyo Roho wa ukweli, atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo.
Yahweh tunaomba ukatubariki na ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitikazo..
Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Jehovah ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..

Asante Baba wa Mbinguni..
Tuyaweka haya yote mikononi mwako..
Tuliyoyanena na tusiyoyanena Mungu Baba unayajua na kutujua sisi zaidi ya tujijuavyo..

Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa kwa muda wenu na kunisoma..
Mungu wa Baraka aendelee kuwabariki na kuwatendea..
Nawapenda..



Mipaka ya nchi

1Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 2“Waamuru Waisraeli ukisema: Mtakapoingia Kanaani, nchi ambayo ninawapa iwe nchi yenu, mipaka ya eneo lenu lote itakuwa kama ifuatavyo. 3Upande wa kusini mpaka wenu utakuwa kutoka jangwa la Sini kupitia upande wa Edomu. Utaanzia mashariki upande wa kusini mwisho wa Bahari ya Chumvi. 4Kisha utapinda kusini kuelekea pito la Akrabimu na kupitia Sini hadi Kadesh-barnea, upande wa kusini. Kutoka hapo, mpaka utapinda kuelekea kaskazini-magharibi hadi Hasar-adari na kupita hadi Azmoni. 5Kutoka Azmoni utapinda kuelekea kijito cha Misri kwenye mpaka wa Misri na kuishia bahari ya Mediteranea.
6“Mpaka wenu wa upande wa magharibi utakuwa bahari ya Mediteranea.
7“Mpaka wenu wa upande wa kaskazini utakuwa kama ifuatavyo: Kutoka bahari ya Mediteranea, mtatia alama hadi Mlima Hori. 8Kutoka Mlima Hori mtatia alama hadi pito la Hamathi, na kuendelea hadi Sedadi, 9na kupita hadi Zifroni na kuishia Hazar-enani; huo utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
10“Mpaka wenu wa upande wa mashariki mtauweka kutoka Hazar-enani hadi Shefamu. 11Kutoka Shefamu utaelekea kusini hadi Ribla, mashariki mwa Aini; kisha mpaka huo utakwenda chini hadi mteremko wa mashariki wa ziwa Kinerethi,34:11 Kinerethi: Ziwa Galilaya. 12halafu utateremka kufuata mto Yordani hadi Bahari ya Chumvi; hii ndiyo itakuwa nchi yako kama mpaka ulivyo.”
13 Taz Yosh 14:1-5 Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu. 14Kabila la Reubeni na la Gadi, na nusu ya kabila la Manase yamepata urithi wao kulingana na koo zao. 15Makabila hayo mawili na nusu yamepata urithi wao ngambo ya mto Yordani upande wa mashariki, mkabala wa Yeriko, mawioni.”

Viongozi watakaosimamia mgawanyo wa nchi

16Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 17“Kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni ndio watakaowagawia watu nchi kuwa mali yao. 18Utachukua pia kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia katika ugawaji wa nchi. 19Haya ndiyo majina yao:
Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
20Kabila la Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21Kabila la Benyamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
22Kabila la Dani, Buki mwana wa Yogli.
23Kabila la Manase mwanawe Yosefu, Hanieli mwana wa Efodi.
24Kabila la Efraimu, mwanawe Yosefu, Kemueli mwana wa Shiftani.
25Kabila la Zebuluni, Elisafani mwana wa Parnaki.
26Kabila la Isakari, Paltieli mwana wa Azani.
27Kabila la Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi
28Kabila la Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.
29Hawa ndio watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwaamuru wawagawie Waisraeli nchi ya Kanaani kuwa mali yao.”



Hesabu34;1-29



Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.