Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 20 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 6...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona siku hii...
Si kwamba tumetenda mema sana,wala si kwamba sisi ni wazuri mno
si kwa nguvu/utashi wetu,wala si kwa akili zetu sisi kuwa hivi
tulivyo leo hii....
Ni kwa neema/rehema zake,Ni kwa mapenzi yake  Mungu wetu..


Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe. Tena watu wengi watazifuata hizo njia zao mbaya, na kwa sababu yao wengine wataipuuza njia ya ukweli. Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yuko tayari, na Mwangamizi wao yuko macho! Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea siku ile ya hukumu. Mungu hakuihurumia dunia ya hapo kale, bali alileta gharika kuu juu ya nchi ile ya watu wasiomcha Mungu; lakini Noa ambaye alihubiri uadilifu, Mungu alimwokoa pamoja na watu wengine saba. Mungu aliiadhibu miji ya Sodoma na Gomora, akaiteketeza kwa moto, akaifanya iwe mfano wa mambo yatakayowapata watu wasiomcha Mungu.
Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu...
Asante Baba wa Mbinguni kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwa uzima/pumzi,afya na kuwa tayari katika majukumu yetu..
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah,
Uabudiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..!!


Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako Yahweh...
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,
kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale
wote waliotukosea..
Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu Baba utuokoe na
yule mwovu na kazi zake zote..
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Yahweh utufunike
kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo
wa Nazareti maana yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..



Alimwokoa Loti, mtu mwema, ambaye alisikitishwa sana na mwenendo mbaya wa watu hao waasi. Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu. Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu, hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni wakaidi na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu. Lakini malaika ambao wana uwezo na nguvu kuliko hao waalimu wa uongo, hawawashtaki na kuwatukana hao mbele ya Bwana. Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na wanyama wasio na akili ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe, na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, hali wakifurahia njia zao za udanganyifu. Macho yao yamejaa uzinzi na uwezo wao wa kutenda dhambi hauna kikomo. Huwaongoza watu walio dhaifu mpaka mitegoni. Mioyo yao imezoea kuwa na tamaa ya mali. Wapo chini ya laana ya Mungu! Wameiacha njia iliyonyoka, wakapotoka na kuifuata njia aliyofuata Balaamu, mwana wa Beori ambaye alipendelea kupata faida kwa kufanya udanganyifu, akakaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi, alinena kwa sauti ya binadamu, akaukomesha wazimu wa huyo nabii.




Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu..
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu,maarifa katika ufanyaji/utendaji
Baba nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako....
Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji


Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Jehovah ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu
na wote wanaotuzunguka,Baba wa Mbinguni tunaomba ulinzi wako kwetu
na kwa vyote tunavyovimiliki,Yahweh ukatamalaki na kutuatamia,Mungu wetu ukatupe neema ya kufuata njia zako,Kusimamia Neno lako amri
na sheria zako siku zote za maisha yetu..Baba wa Mbinguni ukatupe
amani moyoni, utu wema,fadhili,unyenyekevu,hekima,busara,upendo,
tukaonyane/kuelimishana kwa upole na amani,tuakchuliane na kusamehena,Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu,tupate kutambua/kujitambua,ukatufanye barua njema nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu. Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu. Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu – maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala. Watu waliokwisha ponyoka katika upotovu wa ulimwengu kwa kupata kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kisha wakakubali kunaswa na kutawaliwa tena na upotovu huo, hali yao itakuwa mbaya zaidi kuliko awali. Ingalikuwa afadhali kwao kama wasingalijua kamwe njia hiyo ya uadilifu kuliko kuijua na kisha kuiacha na kupoteza amri takatifu waliyopokea. Ipo methali isemayo: “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika matope!” Ndivyo ilivyo kwao sasa.


Tazama wenye shida/tabu Mungu wetu,wagonjwa,wenye njaa,wanaopitia
magumu/majaribu mbalimbali,walio katika vifungo vya yule mwovu,
waliokataliwa,waliokata tamaa,wenye hofu na mashaka,waliopotea/kuanguka na wote walio katika mapito mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,Yahweh tunaomba ukawaponye kiroho na kimwili pia,Baba ukawape neema ya
kujiombea,kufuata njia zako,Yahweh ukawape chakula na ukabariki mashamba yao,Mungu wetu tunaomba ukawarudishe na kuwasimamisha tena,Baba wa Mbinguni wakapate tumaini na Nuru yako ikaangaze
katika maisha yao,Baba wa Mbinguni ukaonekane katika shida zao
Mungu wetu ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe
Baba ukasikie kulia kwao na ukawafute machozi ya watoto wako
wanaokutafuta,kukuomba kwa imani na bidii,Ee Baba tunaomba upokee
sala/maombi yetu na ukawatendee sawasawa na mapenzi yako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele....
Amina..!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwa kuwa nami..
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake
Amani,upendo,furaha na baraka ziwe nanyi...
Nawapenda.

Gideoni

1Waisraeli walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akawatia mikononi mwa Wamidiani kwa muda wa miaka saba. 2Wamidiani waliwakandamiza sana Waisraeli, mpaka wakajichimbia mashimo na mapango milimani kuwa ngome zao. 3Kila mara Waisraeli walipopanda mbegu mashambani, Wamidiani, Waamaleki na watu wengine wa huko mashariki walikuja kuwashambulia. 4Mataifa hayo yaliweka kambi nchini, yakawashambulia na kuharibu mazao yote nchini hadi mpakani mwa Gaza, wasiwaachie Waisraeli chochote, awe kondoo, ng'ombe au punda. 5Adui waliozoea kuja kwa wingi kama nzige, pamoja na ng'ombe na ngamia wao na kufanya makao yao nchini Israeli, waliharibu nchi ya Israeli kwa vile walikuwa wengi mno wasiohesabika. 6Waisraeli walidhoofishwa sana na Wamidiani hata wakamlilia Mwenyezi-Mungu awasaidie.
7Waisraeli walipomlilia Mwenyezi-Mungu awaondolee taabu walizopata kwa Wamidiani, 8Mwenyezi-Mungu aliwapelekea nabii, naye akawaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: ‘Niliwatoa nchini Misri ambako mlikuwa watumwa, 9nikawakomboa mikononi mwa Wamisri wote waliowakandamiza. Nikawafukuza watu mbele yenu na kuwapa nyinyi nchi yao. 10Kisha nikawakumbusheni kuwa mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; na kwamba msiiheshimu miungu ya Waamori, ambao nchi yao mmeichukua, lakini hamkuisikiliza sauti yangu.’”

Mungu anamwamuru Gideoni awaokoe Waisraeli

11Malaika wa Mwenyezi-Mungu akaenda, akaketi chini ya mwaloni wa Yoashi, Mwabiezeri, huko Ofra. Gideoni mwana wa Yoashi, alikuwa anapura ngano ndani ya shinikizo la kusindikia zabibu ili Wamidiani wasimwone. 12Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamtokea, akamwambia, “Mwenyezi-Mungu yuko pamoja nawe, ewe shujaa.”
13Gideoni akamwambia, “Ee Bwana wangu, ikiwa Mwenyezi-Mungu yuko pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu ambayo wazee wetu walitusimulia, wakisema: ‘Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetutoa nchini Misri.’ Lakini sasa Mwenyezi-Mungu ametutupa na kututia mikononi mwa Wamidiani!”
14Mwenyezi-Mungu akamgeukia, akamwambia, “Nenda kwa uwezo ulio nao, ukaikomboe Israeli kutoka Wamidiani. Ni mimi ninayekutuma.”
15Gideoni akamjibu, “Tafadhali Bwana, nitawezaje kuikomboa Israeli? Ukoo wangu ndio dhaifu zaidi katika kabila la Manase, na mimi mwenyewe ni mdogo kabisa katika jamaa yetu!”
16Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nitakuwa pamoja nawe; nawe utawaangamiza Wamidiani kana kwamba wangekuwa mtu mmoja.”
17Gideoni akamwambia, “Basi, ikiwa nimepata fadhili kwako, nioneshe ishara ili nijue kuwa ni wewe kweli uliyezungumza nami. 18Nakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea zawadi yangu na kuiweka mbele yako.”
Naye akamjibu, “Nitakaa hapa mpaka utakaporudi.” 19Gideoni akaenda nyumbani mwake, akatayarisha mwanambuzi na mikate isiyotiwa chachu kutoka debe la unga; akatia nyama ndani ya kikapu na mchuzi ndani ya chungu, kisha akampelekea chini ya mwaloni, akampa. 20Malaika wa Mungu akamwambia, “Chukua nyama na mikate isiyotiwa chachu uviweke juu ya mwamba huu. Halafu tia mchuzi juu ya mikate na nyama.” Naye akafanya hivyo. 21Malaika wa Mwenyezi-Mungu akanyosha fimbo yake, akagusa nyama na mikate kwa ncha ya fimbo. Ghafla, moto ukatoka mwambani, ukateketeza nyama na mikate. Mara malaika wa Mwenyezi-Mungu akatoweka mbele yake.
22Ndipo Gideoni akatambua kwamba huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi-Mungu; akasema, “Ole wangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu, maana nimemwona malaika wako uso kwa uso.”
23Lakini Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Amani iwe nawe! Usiogope, hutakufa.” 24Gideoni akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu huko na kuyaita, “Mwenyezi-Mungu ni Amani.” Madhabahu hiyo iko huko Ofra, mji wa Wabiezeri, mpaka leo.

Gideoni anaibomoa madhabahu ya Baali

25Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo. 26Halafu, unijengee mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, madhabahu nzuri juu ya mwinuko huu. Kisha unitolee sadaka ya kuteketezwa ya yule fahali wa pili ukitumia kuni za ile sanamu ya Ashera uliyoivunja.” 27Basi, Gideoni akachukua watumishi wake kumi, akafanya kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Lakini kwa kuwa aliiogopa jamaa yake na watu wa mjini, badala ya kufanya hayo mchana, alifanya wakati wa usiku.
28Wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema waliona madhabahu ya Baali na sanamu ya Ashera iliyokuwa karibu nayo vimeharibiwa. Yule fahali wa pili alikuwa ameteketezwa juu ya madhabahu iliyokuwa imejengwa mahali hapo. 29Wakaulizana, “Nani amefanya jambo hili?” Walipofanya uchunguzi wakagundua kwamba Gideoni mwana wa Yoashi ndiye aliyekuwa amefanya hayo. 30Wakazi wa mji wakamjia Yoashi, wakamwambia, “Mtoe mwanao tumuue, maana ameharibu madhabahu ya Baali na kuivunja sanamu ya Ashera iliyokuwa karibu nayo.”
31Yoashi akawaambia wale wote waliomkabili, “Je, mnamtetea Baali? Je, mtamwokoa? Yeyote atakayemtetea atauawa kabla ya mapambazuko. Kama Baali ni mungu, basi, na ajitetee mwenyewe maana madhabahu yake imebomolewa.” 32Siku hiyo wakamwita Gideoni “Yerubaali” maana yake, “Baali na ajitetee mbele yake”, maana aliibomoa madhabahu ya Baali.
33Wamidiani, Waamaleki na watu wote wanaokaa kando ya mto Yordani wakapiga kambi zao katika bonde la Yezreeli. 34Lakini roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Gideoni. Gideoni akapiga tarumbeta kuwaita Wabiezeri waje kumfuata. 35Akatuma wajumbe katika nchi yote ya Manase waje kumfuata. Wajumbe wengine akawatuma kuwaita watu wa makabila ya Asheri, Zebuluni na Naftali, nao wakaja kujiunga naye.
36Gideoni akamwambia Mungu, “Ikiwa utaikomboa Israeli kwa mkono wangu kama ulivyosema, 37sasa naweka ngozi ya kondoo kwenye sakafu ya kupuria ngano. Ikiwa kutakuwa na umande juu ya ngozi tu, na sakafu inayoizunguka ikawa kavu, basi, nitajua kuwa utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu kama ulivyosema.” 38Ikawa hivyo, kwa maana alipoamka asubuhi kesho yake, alikamua umande uliokuwa juu ya ile ngozi, akajaza bakuli. 39Gideoni akamwambia Mungu, “Tafadhali usinikasirikie. Nakuomba niseme mara moja tena. Nakuomba uniruhusu nitumie ngozi hii kufanya jaribio lingine. Nakuomba juu ya ngozi kuwe kukavu, lakini kwenye sakafu kuwe na umande.” 40Mungu akafanya hivyo usiku huo, maana, juu ya ngozi kulikuwa kukavu na kwenye sakafu kulikuwa na umande.


Waamuzi 6;1-40

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday, 17 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 5...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba wa Nchi na Mbingu,
Muumba wa vyote vinavyoonekana na visivyoonekana,Muweza wa yote
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mungu mwenye nguvu,Mfalme wa amani,Alfa na Omega,wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Hakuna kama wewe,Unatosha Baba wa Mbinguni...!

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..

Sifa na utukufu tunakurudishia wewe..!!



Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.” Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na
kujiachilia mikononi mwako Jehovah..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza
kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu
Baba utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah
utufunike kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi
wetu Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..




Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na kutetemeka; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo. Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu nyinyi ni watumishi wa Kristo. Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu. Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana. Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba nyinyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, naye hatendi kwa ubaguzi.
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Mungu wetu ukatupe ubunifu,maarifa katika ufanyaji/utendaji
Yahweh tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji,Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Yahweh ukatupe kama inavyokupendeza wewe..


Mungu wetu tunaomba ukabariki Nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi
wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka,Mfalme wa amani
tunaomba amani yako itawale katika maisha yetu,Mungu wetu tunaomba
ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki,Yahweh ukatamalaki
na kutuatamia,Baba wa Mbinguni ukatupe neema ya kufuata njia zako,kusimamia Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Jehovah ukatufanye chombo chema nasi tukatumike
 kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote tupate kutambua/kujitambua
na tukawe na kiasi..



Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara. Basi, kaeni tayari. Ukweli na uwe kama mkanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu. Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Injili kwa uthabiti. Mimi ni balozi kwa ajili ya Injili hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
wote wanaopitia magumu/majaribu,wagonjwa,wenye shida/tabu,
waliokatika vifungo vya yule mwovu  Baba ukawape uponyaji wa mwili na
roho,ukawape neema ya kujiombea na kufuata njia zako,wenye njaa
Mungu wetu ukawatendee na kubariki mashamba yao,wafiwa ukawe
mafariji wao,Mungu wetu ukafute machozi ya watoto wako na ukasikie
kuomba kwao,Nuru yako ikaangaze katika maisha yao..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!



Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya. Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo. Ninawatakieni nyinyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho.

Wapendwa katika Bwana asanteni sana kwakuwa nami
Mungu wa rehema/neema aendelee kuwabariki na kuwatendea
sawasawa na mapenzi yake, Amani ya Kristo Yesu iwe nanyi Daima..
Nawapenda.

Wimbo wa Debora

1Siku hiyo, Debora na Baraki, mwana wa Abinoamu, wakaimba wimbo huu:
2“Viongozi walijitokeza kuongoza Israeli,
watu walijitolea kwa hiari yao.
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu!
3“Sikilizeni, enyi wafalme!
Tegeni sikio, enyi wakuu!
Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
4“Ee Mwenyezi-Mungu, ulipotoka huko Seiri,
ulipoteremka mlimani Edomu,
nchi ilitetemeka,
mbingu zilidondosha maji,
naam, mawingu yakaiangusha mvua.
5Milima ilitikisika mbele yako Mwenyezi-Mungu,
naam, mlima Sinai mbele yako Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
6“Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi,
katika wakati wa Yaeli,
misafara ilikoma kupita nchini,
wasafiri walipitia vichochoroni.
7Wakulima walikoma kuwako,
walikoma kuwako katika Israeli,
mpaka nilipotokea mimi Debora,
mimi niliye kama mama wa Israeli.
8Walijichagulia miungu mipya,
kukawa na vita katika nchi.
Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngao
kati ya watu 40,000 wa Israeli.
9Nawapa heshima makamanda wa Israeli
waliojitoa kwa hiari yao kati ya watu.
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu!
10“Tangazeni, enyi wapandapunda weupe,
enyi mnaokalia mazulia ya fahari,
nyinyi mnaotembea njiani, tangazeni jambo hilo.
11Imbeni kupita wanamuziki kwenye visima vya maji,
tangazeni ushindi wa Mwenyezi-Mungu,
ushindi kwa wakulima wake katika Israeli.
Ndipo watu wa Mwenyezi-Mungu waliposhuka malangoni.
12“Amka, amka, Debora!
Amka! Amka uimbe wimbo!
Amka, Baraki mwana wa Abinoamu,
uwachukue mateka wako.
13Mashujaa waliobaki waliteremka,
watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania
dhidi ya wenye nguvu.
14Kutoka Efraimu waliteremka bondeni,5:14 bondeni: Makala ya Kiebrania; katika Maaleki.
wakafuata ndugu zao watu wa Benyamini;
kutoka Makiri walishuka makamanda,
kutoka Zebuluni maofisa wakuu.
15Wakuu wa Isakari wakafuatana na Debora,
watu wa Isakari waaminifu kwa Baraki;
wakamfuata mbio mpaka bondeni.
Lakini miongoni mwa koo za Reubeni
kulikuwamo kusitasita kwingi.
16Kwa nini walibaki mazizini?
Ili kusikiliza milio ya kondoo?
Miongoni mwa koo za Reubeni
kulikuwamo kusitasita kwingi.
17Kabila la Gileadi lilibaki ngambo ya Yordani.
Kabila la Dani, kwa nini mlibaki merikebuni?
Kabila la Asheri lilitulia huko pwani ya bahari,
lilikaa bandarini mwake.
18Watu wa Zebuluni ni watu
waliohatarisha maisha yao katika kifo.
Hata wa Naftali walikikabili kifo
kwenye miinuko ya mashamba.
19“Huko Taanaki, kando ya chemchemi za Megido,
wafalme walikuja, wakapigana;
wafalme wa Kanaani walipigana,
lakini hawakupata nyara za fedha.
20Nyota kutoka mbinguni zilishiriki vita,
zilifuata njia zao, zilipigana na Sisera.
21Mafuriko ya mto Kishoni yaliwachukua mbali,
naam, mafuriko makali ya mto Kishoni.
Songa mbele kwa nguvu, ee nafsi yangu!
22“Farasi walipita wakipiga shoti;,
walikwenda shoti na kishindo cha kwato zao.
23Malaika wa Mwenyezi-Mungu asema hivi:
‘Uapizeni mji wa Merosi,
waapizeni vikali wakazi wake;
maana hawakuja kumsaidia Mwenyezi-Mungu
hawakumsaidia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wenye nguvu’.
24“Abarikiwe kuliko wanawake wote
Yaeli, mke wa Heberi, Mkeni.
Naam, amebarikiwa kuliko wanawake wote
wanaokaa mahemani.
25Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa;
alimletea siagi katika bakuli ya heshima.
26Kwa mkono mmoja alishika kigingi cha hema,
na kwa mkono wake wa kulia nyundo ya fundi;
alimponda Sisera kichwa,
alivunja na kupasuapasua paji lake.
27Sisera aliinama, akaanguka;
alilala kimya miguuni pake.
Hapo alipoinama ndipo alipoanguka, amekufa!
28“Mama yake Sisera alitazama dirishani
alichungulia katika viunzi vyake, akalalamika:
‘Kwa nini gari lake limechelewa?
Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa kusikika?’
29Jibu akalipata kwa wanawake wenye hekima:
Akajituliza tena na tena kwa jibu hilo:
30‘Bila shaka wanatafuta na kugawana nyara;
msichana mmoja au wawili kwa kila askari,
vazi la sufu ya rangi kwa ajili ya Sisera.
Vazi la sufu iliyotariziwa,
na mikufu miwili ya nakshi kwa ajili ya shingo yangu!’
31“Ee Mwenyezi-Mungu, waangamie adui zako wote!
Lakini rafiki zako na wawe kama jua,
wakati linapochomoza kwa mwanga mkubwa!”
Nayo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arubaini.


Waamuzi 5;1-31

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday, 16 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 4...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..!Baba wa Mbinguni..
Mungu wetu,Muumba wetu,Muumba wa Vyote vilivyopo..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mungu wa wote walio hai..
Baba wa Yatima,Mume wa wajane,Baba wa Upendo,Mungu wa huruma Muweza wa yote,Mponyaji wetu,Jehovah..!Yahweh..!Adonai..!
El Shadai..!Elohim..!El Elyon..!El Olam..!El Qanna..!Emanueli..!Mungu pamoja nasi..!

Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,
Unatosha Mungu wetu,Hakuna kama wewe..!




Laiti mngenivumilia kidogo, hata kama mimi ni mjinga kiasi! Naam, nivumilieni kidogo. Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana nyinyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo. Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo. Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, nyinyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au Injili tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu! Sidhani kwamba mimi ni mdogo kuliko hao “mitume wakuu.” Labda sina ufasaha wa lugha, lakini elimu ninayo; jambo hili tumelionesha wazi kwenu, kila mahali na kila wakati.

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba tumetenda mema sana,si kwa nguvu/utashi wetu,si kwa akili zetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Mungu wetu,Ni kwa Neema/rehema zako
Ni kwa mapenzi yako Mungu wetu kuwa hivi tulivyo..

Tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya na Kesho ni siku
Nyingine Baba wa Mbinguni..
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia
mikononi mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Mungu wetu
nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Jehovah tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule
mwovu na kazi zake zote..
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Yahweh utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo
wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..





Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya? Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia nyinyi. Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo. Naahidi kwa ule ukweli wa Kristo ulio ndani yangu, kwamba hakuna kitakachoweza kunizuia kujivunia jambo hilo popote katika Akaya. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu eti siwapendi nyinyi? Mungu anajua kwamba nawapenda! Nitaendelea kufanya kama ninavyofanya sasa, ili nisiwape nafasi wale wanaotafuta nafasi, nafasi ya kujivuna kwamba eti wanafanya kazi kama sisi. Maana, hao ni mitume wa uongo, wafanyakazi wadanganyifu wanaojisingizia kuwa mitume wa Kristo. Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga! Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.


Jehovah tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu,Mungu wetu ukatupe
Ubunifu,Maarifa katika ufanyaji/utendaji nasi tukatende
sawasawa na mapenzi yako..
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu
nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..



Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako..
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika
nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na
kwa vyote tunavyovimiliki,Baba wa Mbinguni ukatawale,ukatamalaki na
kutuatamia,Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu,Baba ukatuokoe
katika majivuno,masengenyo,ugomvi,makwazo na vyote vinavyokwenda
kinyume nawe,Mungu wetu ukatupe neema ya kusaidiana,kupendana na tukafurahi pamoja na tukalie pamoja inapobidi..
Baba tukafuate njia zako,Tukasimamie Neno lako amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu,Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ee.. Baba ..!tunaomba upokee maombi/sala zetu..





Tena nasema: Mtu asinifikirie kuwa mpumbavu. Lakini kama mkifikiri hivyo, basi, nichukueni kama mpumbavu ili nami nipate kuwa na cha kujivunia angaa kidogo. Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu. Maadamu wengi hujivuna kwa sababu za kidunia, nami pia nitajivuna. Nyinyi ni wenye busara, ndiyo maana hata mnawavumilia wapumbavu! Mnamvumilia hata mtu anayewafanya nyinyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni! Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu – nasema kama mtu mpumbavu – mimi nathubutu pia. Je, wao ni Waebrania? Hata mimi. Je, wao ni Waisraeli? Hata mimi. Wao ni wazawa wa Abrahamu? Hata mimi. Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi – nanena hayo kiwazimu – ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi. Mara tano nilichapwa vile viboko arubaini kasoro kimoja vya Wayahudi. Nilipigwa fimbo mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa. Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo. Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote. Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi. Ikinilazimu kujivuna, basi, nitajivunia udhaifu wangu. Mungu na Baba wa Bwana Yesu – jina lake litukuzwe milele – yeye anajua kwamba sisemi uongo. Nilipokuwa Damasko, mkuu wa mkoa, aliyekuwa chini ya mfalme Areta, alikuwa akiulinda mji wa Damasko ili anikamate. Lakini, ndani ya kapu kubwa, niliteremshwa nje kupitia katika nafasi ukutani, nikachopoka mikononi mwake.



Mungu wetu ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu wagonjwa
wakapate uponyaji wako,wenye njaa ukawapatie chakula na ukabariki
mashamba yao wapate mavuno ya kutosha na kuweka akiba,
wanaopitia magumu/majaribu Mungu wetu ukawavushe,walio magerezani pasipo na hatia Baba ukawatete na kuwatendea,waliokatika vifungo vya
yule mwovu Mungu wetu ukawafungue na ukawaweke huru,Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako na Nuru yako
ikaangaze katika maisha yao..
Kwa imani tunayaweka haya yote mikononi mwako,tukiamini
wewe ni Mungu wetu Jana leo kesho na hata Milele..
Sifa na Utukufu ni wako Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!


Asanteni sana wapendwa kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee
kuwa nanyi,Amani,Upendo na Baraka zisipungue katika maisha yenu..
Nawapenda.

Debora na Baraki

1Baada ya kifo cha Ehudi, Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu. 2Mwenyezi-Mungu akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, ambaye aliishi huko Hazori. Kamanda wa jeshi lake alikuwa Sisera, mwenyeji wa Harosheth-hagoimu. 3Mfalme Yabini alikuwa na magari ya vita 900 ya chuma. Aliwakandamiza sana Waisraeli kwa miaka ishirini; nao wakamlilia Mwenyezi-Mungu awasaidie.
4Wakati huo, kulikuwa na nabii mwanamke aliyeitwa Debora, mke wa Lapidothi, aliyekuwa mwamuzi wa Waisraeli wakati huo. 5Debora alikuwa na mazoea ya kuketi chini ya mtende uliokuwa kati ya mji wa Rama na mji wa Betheli katika nchi ya milima ya Efraimu. Watu wa Israeli walimjia ili awaamulie mashauri yao. 6Siku moja alimwita Baraki mwana wa Abinoamu wa Kedeshi katika nchi ya Naftali. Alipokuja alimwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anakuamuru hivi: ‘Nenda ukusanye watu wako mlimani Tabori, uchague watu 10,000 kutoka makabila ya Naftali na Zebuluni. 7Mimi nitamchochea Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, aje na majeshi na magari yake kupigana nawe kwenye mto Kishoni, na kumtia mikononi mwako.’” 8Baraki akamwambia Debora, “Kama utakwenda pamoja nami, nitakwenda. Lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.” 9Debora akamjibu, “Sawa. Nitakwenda pamoja nawe; lakini hutapata heshima yoyote ya ushindi, maana Mwenyezi-Mungu, atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Basi, Debora akafuatana na Baraki kwenda Kedeshi. 10Baraki akayaita makabila ya Naftali na Zebuluni huko Kedeshi; watu 10,000 wakamfuata. Debora akaenda pamoja naye.
11Wakati huo, Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni wenzake ambao ni wazawa wa Hobabu, baba mkwe wa Mose. Alikuwa amepiga hema lake mbali huko kwenye mwaloni wa Zaananimu, karibu na Kedeshi.
12Sisera alipopata habari kwamba Baraki mwana wa Abinoamu amekwenda mlimani Tabori, 13alikusanya jeshi lake lote na magari yake mia tisa ya chuma, akaondoka Harosheth-hagoimu, akaenda kwenye mto Kishoni. 14Debora akamwambia Baraki, “Inuka! Leo ni siku ambayo Mwenyezi-Mungu atamtia Sisera mikononi mwako. Mwenyezi-Mungu anakwenda mbele yako.” Basi, Baraki akashuka kutoka mlimani Tabori akiwaongoza watu wake 10,000. 15Baraki akafanya mashambulizi, naye Mwenyezi-Mungu akamtimua Sisera na jeshi lake lote mbele ya Baraki kwa upanga. Sisera akatoka katika gari lake, akakimbia kwa miguu. 16Baraki akalifuatia jeshi hilo na magari mpaka Harosheth-hagoimu na kuwaua wanajeshi wote wa Sisera kwa mapanga; hakubaki hata mtu mmoja.
17Lakini Sisera alikimbia kwa miguu mpaka hemani kwa Yaeli, mke wa Heberi, Mkeni. Alifanya hivyo kwa sababu kulikuwa na amani kati ya mfalme Yabini wa Hazori na jamaa ya Heberi. 18Yaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, “Bwana wangu, karibu kwangu, wala usiogope.” Akaingia hemani mwake, akamfunika kwa blanketi. 19Sisera akamwambia Yaeli, “Tafadhali, nipe maji kidogo ninywe, maana nina kiu.” Akampa maziwa badala ya maji, kisha akamfunika tena. 20Sisera akamwambia, “Simama mlangoni mwa hema. Mtu yeyote akija kukuuliza kama kuna mtu yeyote hapa, mwambie hakuna.” 21Lakini Yaeli, mke wa Heberi, akachukua kigingi cha hema na nyundo, akamwendea polepole akakipigilia kile kigingi cha hema katika paji la uso wake kikapenya mpaka udongoni, kwa maana alikuwa amelala fofofo kwa uchovu. Basi, Sisera akafa papo hapo. 22Naye Baraki alipokuwa anamfuatilia Sisera, Yaeli akatoka nje kumlaki akamwambia, “Njoo nami nitakuonesha yule unayemtafuta.” Baraki akaingia ndani ya hema la Yaeli na kumkuta Sisera chini, amekufa, na kigingi cha hema pajini mwake.
23Hivyo, siku hiyo Mungu akawapa Waisraeli ushindi juu ya mfalme Yabini wa Kanaani. 24Waisraeli wakaendelea kumwandama Yabini, mfalme wa Kanaani, mpaka walipomwangamiza.


Waamuzi 4;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday, 15 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 3...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu Mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu..

Asante Baba wa Mbinguni kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa mpumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Utukuzwe Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhihidiwe Jehovah,
Uabudiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu sana,Matendo yako ni ya ajabu
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..!!


Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako Yahweh...
Mungu wetu tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua...
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea....
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu
 Baba  utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah
utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Wastahili sifa, ee Mungu, huko Siyoni, watu watakutimizia wewe ahadi zao, maana wewe wajibu sala zetu. Binadamu wote watakujia wewe. Tunapolemewa na makosa yetu, wewe mwenyewe watusamehe. Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu, waishi katika maskani yako. Sisi tutatoshelezwa na mema ya nyumba yako; mema ya hekalu lako takatifu. Kwa matendo yako makuu watuitikia na kutuokoa, ewe Mungu wa wokovu wetu; wewe ndiwe tumaini la viumbe vyote, duniani kote na mbali baharini. Kwa nguvu yako uliisimika milima mahali pake. Wewe una nguvu mno! Watuliza mshindo wa bahari na wa mawimbi yake, wakomesha ghasia za watu. Ulimwengu wote washangazwa na matendo yako. Wasababisha furaha kila mahali, toka mashariki hata magharibi. Wewe waitunza nchi kwa kuinyeshea mvua, waijalia rutuba na kuistawisha; mto wako umejaa maji tele, waifanikisha nchi na kuipatia mavuno. Hivi ndivyo uitengenezavyo nchi: Mashamba wayanyeshea mvua kwa wingi, na kuyalowanisha kwa maji; ardhi wailainisha kwa manyunyu, na kuibariki mimea ichipue. Wautunukia mwaka wote mema yako, kila ulipopitia pamejaa fanaka. Mbuga za majani zimejaa mifugo, milima nayo imejaa furaha. Malisho yamejaa kondoo, mabonde yamefunikwa kwa ngano. Kila kitu kinashangilia kwa furaha.




Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Mungu wetu ukatupe ubunifu,maarifa katika ufanyaji/utendeji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Yahweh
nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Baba wa Mbinguni tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu
ukatupe kama inavyokupendeza wewe..



Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu; kwake naliweka tumaini langu. Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika. Wokovu na fahari yangu vyatoka kwa Mungu; mwamba wangu mkuu na kimbilio langu ni Mungu. Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu. Binadamu wote ni kama pumzi tu; wote, wakubwa kwa wadogo, hawafai kitu. Tena ukiwapima uzito hawafikii kilo, wote pamoja ni wepesi kuliko pumzi. Msitegemee dhuluma, msijisifie mali ya wizi; kama mali zikiongezeka, msizitegemee. Mungu ametamka mara moja, nami nimesikia tena na tena: Kwamba enzi ni mali yake Mungu; naam, nazo fadhili ni zake Bwana; humlipa kila mtu kadiri ya matendo yake.

Mtalme wa amani tunayaweka maisha yetu mikononi mwako..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatawale,ukatamalaki na kutuatamia
Yahweh tunaomba ulinzi wako wakati wote kwetu na kwa vyote
tunavyovimiliki,Mungu wetu ukatupe neema ya kutambua/kujitambu,
kufuata njia zako,kusimamia Neno lako amri na sheria zako siku zote
za maisha yetu,Yahweh tukawe wanyenyekevu kwa watu wote,
wepesi wa kusamehe Baba ukatupe amani ya moyo,upendo wa kweli,
kusaidiana,kuchukuliana,kuonyana/kuelimishana kwa amani na upendo
Mungu wetu ukatufanye barua njema nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..




Tunakushukuru, ee Mungu, tunakushukuru! Tunatangaza ukuu wa jina lako na kusimulia juu ya matendo yako makuu. Mungu asema: “Mimi nimeweka wakati maalumu! Wakati huo nitahukumu kwa haki. Nchi ikitetemeka na vyote vilivyomo, mimi ndiye ninayeitegemeza misingi yake. Nawaambia wenye kiburi: ‘Acheni kujigamba’; na waovu: ‘Msioteshe pembe za kiburi! Msijione kuwa watu wa maana sana, wala kusema maneno ya majivuno.’” Hukumu haitoki mashariki au magharibi; wala haitoki nyikani au mlimani. Mungu mwenyewe ndiye hakimu; humshusha mmoja na kumkweza mwingine. Mwenyezi-Mungu, anashika kikombe mkononi, kimejaa divai kali ya hasira yake; anaimimina na waovu wote wanainywa; naam, wanainywa mpaka tone la mwisho. Lakini mimi nitafurahi milele, nitamwimbia sifa Mungu wa Yakobo. Atavunja nguvu zote za watu waovu; lakini nguvu za waadilifu ataziimarisha.

Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
wote wataabikao na kuelemewa na mizigo,Mungu wetu tunaomba ukawaponye wagonjwa ,wenye njaa ukawapatie chakula,waliokataliwa na kukata tamaa Mungu wetu ukawape tumaini,wanaopita katika magumu/majaribu
Mungu wetu ukawavushe salama,waliokatika vifungo vya yule mwovu
Baba wa Mbinguni ukawafungue na kuwaweka huru,Yahweh ukawape
neema ya kujiombea,kufuata njia zako,ukawape macho ya kuona
na masikio ya kusikia sauti yako na kutii,Baba tunaomba ukapokee
sala/maombi yetu na ukawafute machozi ya watoto wako
wanaokutafuta kwa bidii na imani,Ee Baba utusikie..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa katika Bwana kwakuwa nami
Mungu awe nanyi daima na msipungukiwe katika mahitaji yenu
Baba wa Mbinguni akawape sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.

1Mwenyezi-Mungu aliyaacha nchini mataifa yafuatayo ili kuwajaribu Waisraeli ambao walikuwa hawajapigana vita katika nchi ya Kanaani 2(alifanya hivyo ili awape watu wa vizazi hivyo ujuzi wa kupigana kwani hawakuwa wameona vita): 3Wakuu watano wa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni na Wahivi waliohamia katika milima ya Lebanoni kutoka mlima Baal-hermoni mpaka kufikia Hamathi. 4Mwenyezi-Mungu alikusudia kuwatumia hao ili awajaribu Waisraeli, aone kama watatii amri zake alizowaamuru wazee wao kwa njia ya Mose. 5Basi, Waisraeli waliishi pamoja na Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 6Wakaoa binti zao na kuoza binti zao kwa vijana wa mataifa hayo na kuiabudu miungu yao.
Othnieli
7Waisraeli walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; wakamsahau Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaabudu Mabaali na Maashera. 8Basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia, nao wakamtumikia kwa muda wa miaka minane. 9Waisraeli wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawapelekea mtu wa kuwakomboa yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu. 10Basi, roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Othnieli, naye akawa mwamuzi wa Waisraeli. Othnieli alikwenda vitani naye Mwenyezi-Mungu akamtia Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwake. 11Hivyo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arubaini. Kisha Othnieli mwana wa Kenazi, akafariki.
Ehudi
12Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akampa nguvu mfalme Egloni wa Moabu awashambulie Waisraeli, kwa sababu walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu. 13Egloni akawakusanya Waamoni na Waamaleki, akaenda kupigana na Waisraeli, akawashinda. Akauteka Mji wa Mitende yaani Yeriko. 14Waisraeli wakamtumikia Egloni mfalme wa Moabu, kwa muda wa miaka kumi na minane.
15Lakini Waisraeli walipomlilia Mwenyezi-Mungu, yeye aliwapelekea mtu wa kuwakomboa, yaani Ehudi mwana wa Gera, mwenye mkono wa shoto, wa kabila la Benyamini.
Waisraeli walimtuma apeleke zawadi zao kwa Egloni mfalme wa Moabu. 16Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake. 17Kisha akampelekea Egloni zile zawadi. Egloni alikuwa mtu mnene sana. 18Ehudi alipomaliza kutoa zawadi, akawaambia watu waliobeba zawadi, waondoke. 19Lakini yeye alipofika kwenye sanamu za mawe yaliyochongwa karibu na Gilgali, alimrudia Egloni akasema, “Nina ujumbe wa siri kwako, ee mfalme.” Mfalme akawaamuru watumishi wakae kimya, nao wakatoka nje. 20Naye Ehudi akamkaribia pale alipokaa katika chumba chake chenye baridi barazani, akamwambia “Nina ujumbe wako kutoka kwa Mungu.” Mfalme akainuka kitini mwake na kusimama. 21Ehudi akauchomoa upanga wake kwa mkono wake wa kushoto kutoka paja lake la kulia, akamchoma nao tumboni mwake. 22Upanga ukaingia ndani pamoja na mpini wake, mafuta yakaufunika upanga huo kwani Ehudi hakuutoa tena; ukawa umetokea kwa nyuma.3:22 ukawa umetokea kwa nyuma: Maana ya neno la Kiebrania si dhahiri. 23Kisha, Ehudi akatoka nje barazani baada ya kuifunga milango ya chumba hicho kwa ufunguo.
24Ehudi alipoondoka, watumishi wa mfalme wakarudi. Walipoona milango yote ya chumba imefungwa, walifikiri amekwenda kujisaidia chooni humo ndani ya nyumba. 25Wakangojea mpaka wakaanza kuwa na wasiwasi. Walipoona hafungui, wakachukua ufunguo na kufungua mlango. Wakamwona mfalme wao sakafuni, naye amekufa.
26Walipokuwa wanangoja, Ehudi alitoroka akipitia kwenye sanamu za mawe, akaenda Seira. 27Alipofika huko alipiga tarumbeta katika nchi ya milima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani naye akawatangulia. 28Akawaambia, “Mnifuate, maana Mwenyezi-Mungu amewatia adui zenu Wamoabu mikononi mwenu.” Wakamfuata mpaka kivuko cha Yordani na kukiteka toka mikononi mwa Wamoabu, wakazuia mtu yeyote kupita. 29Siku hiyo, wakawaua Wamoabu wapatao 10,000; watu wote wenye afya na nguvu, wala hakuna hata mmoja aliyenusurika. 30Siku hiyo Waisraeli wakawashinda Wamoabu. Nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka themanini.
Shamgari
31Baada ya Ehudi mwana wa Anati, Shamgari alishika nafasi yake. Yeye aliwaua Wafilisti 600 kwa fimbo ya kuchungia ng'ombe. Naye pia aliwakomboa Waisraeli.


Waamuzi 3;1-31

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday, 14 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 2...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu.!Baba wa Mbinguni..
Mungu wetu,Muumba wetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Mungu wa Wajane,Baba wa Yatima,Muweza wa yote,Mponyaji wetu,
Utukuzwe Yahweh,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uabudiwe Jehovah,
Uhimidiwe Mungu wetu,Unatosha Baba wa Mbinguni,Hakuna kama wewe
wewe ni alfa na Omega,wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho..!

Ndugu zangu, ninataka na kutazamia kwa moyo wangu wote hao wananchi wenzangu wakombolewe. Tena nawaombea kwa Mungu daima. Maana naweza kuthibitisha kwa niaba yao kwamba wanayo bidii ya kumtafuta Mungu; lakini bidii hiyo haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli. Maana hawakufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu wawe waadilifu, na wamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe na hivyo hawakuikubali njia hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu. Maana kwa kuja kwake Kristo, sheria imefikia kikomo chake, ili wote wanaoamini wafanywe waadilifu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na
kujiachilia mikononi mwako Yahweh..
Tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya kwakuwaza,
kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Mungu wetu..
Tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote
waliotukosea..
Jehovah tunaomba utuepushe katika majaribu Baba utuokoe na yule
mwovu na kazi zake zote..
Mungu wetu tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Yahweh utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu
 Yesu Kristo wa Nazareti..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..



Kuhusu kuwa mwadilifu kwa kuitii sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya sheria ataishi.” Lakini kuhusu kuwa mwadilifu kwa njia ya imani, yasemwa hivi: “Usiseme moyoni mwako: ‘Nani atapanda mpaka mbinguni?’ (yaani, kumleta Kristo chini); wala usiseme: ‘Nani atashuka mpaka kuzimu?’ (yaani, kumleta Kristo kutoka kwa wafu).” Maandiko Matakatifu yasema hivi: “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri. Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Maana mtu huamini kwa moyo akafanywa mwadilifu; na hukiri kwa kinywa akaokolewa. Maandiko Matakatifu yasema: “Kila anayemwamini hataaibishwa.” Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao. Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.”

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu,Jehovah
ukatupe ubunifu,maarifa katika ufanyaji/utendaji Yahweh
nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji,Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Yahweh ukatupe sawasawa na mapenzi yako...

Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa
zetu,watoto/wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Mungu wetu ukatubariki,ukatamalaki na kutuatamia,Jehovah ukatupe
neema ya kufuata njia zako,kusimamia Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu,Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Baba ukatuepushe na roho za kiburi,kujiona kujisifu,Mungu wetu na vyote vinavyokwenda kinyume nawe..
Jehovah ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupenda wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Basi, watamwombaje yeye ambaye hawamwamini? Tena, watamwaminije kama hawajapata kusikia habari zake? Na watasikiaje habari zake kama hakuna mhubiri? Na watu watahubirije kama hawakutumwa? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari Njema!” Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” Hivyo basi, imani inatokana na kuusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo. Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.” Tena nauliza: Je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu: “Nitawafanyeni muwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu.” Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.” Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”


Tazama wenye shida/tabu Mungu wetu, Tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,wagonjwa wakapate uponyaji wako,wenye njaa ukawapatie chakula,wanaopitia magumu/majaribu ukawavushe Mungu wetu,walio katika vifungo vya yule mwovu ukawafungue Jehovah ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako,Nuru ikaangaze katika
maisha yao,wakapate uponyaji wa mwili na roho pia...

Sifa na utukufu tunakurudishia Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakunisoma
Mungu aendelee kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Amani,Upendo na Baraka ziwe nanyi siku zote..
Nawapenda.

Mwenyezi-Mungu anawagombeza watu wake

1Malaika wa Mwenyezi-Mungu aliondoka Gilgali, akaenda Bokimu, akawaambia Waisraeli, “Niliwatoa nchini Misri na kuwaleta katika nchi ambayo niliwaahidi kwa kiapo babu zenu. Nilisema kwamba sitalivunja agano langu nanyi kamwe. 2Na kwa upande wenu niliwaamuru msifanye agano na wenyeji wa nchi hii na kwamba madhabahu zao mtazibomoa. Lakini nyinyi hamkuitii amri yangu. Kwa nini mambo haya? 3Kwa hiyo sasa nasema: Sitawafukuza tena wakazi wa nchi hii bali watawataabisha, nayo miungu yao itakuwa mtego kwenu.” 4Malaika wa Mwenyezi-Mungu alipowaambia watu wote wa Israeli maneno haya, walipaza sauti zao na kulia. 5Wakapaita mahali hapo Bokimu.2:5 Bokimu: Jina hili katika Kiebrania linamaanisha “Wanaolia”. Hapo wakamtolea sadaka Mwenyezi-Mungu.

Kifo cha Yoshua

6Baada ya Yoshua kuwaaga Waisraeli, kila mmoja alikwenda kwenye eneo lake alilogawiwa ili kuimiliki nchi. 7Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu siku zote za maisha ya Yoshua na baada ya kifo chake muda wote walioishi wale wazee waliosalia ambao waliyaona matendo makuu ambayo Mwenyezi-Mungu aliwatendea Waisraeli. 8Yoshua mwana wa Nuni na mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alifariki akiwa na umri wa miaka 110. 9Wakamzika katika sehemu aliyogawiwa iwe yake huko Timnath-heresi, katika nchi ya milima ya Efraimu kaskazini ya mlima Gaashi. 10Kisha watu wote wa kizazi chake walifariki, kikafuata kizazi kingine ambacho hakikumjua Mwenyezi-Mungu wala matendo aliyowatendea watu wa Israeli.

Waisraeli wanamwasi Mwenyezi-Mungu

11Basi, Waisraeli walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuabudu Mabaali. 12Walimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wao, ambaye aliwatoa katika nchi ya Misri, wakaifuata miungu mingine, miungu iliyoabudiwa na watu walioishi kandokando yao. Waliisujudia miungu hiyo, wakamkasirisha sana Mwenyezi-Mungu. 13Walimwacha Mwenyezi-Mungu, wakatumikia Mabaali na Maashtarothi. 14Basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwaka dhidi ya Israeli, naye akawaacha wanyanganyi wapore mali zao. Aliwakabidhi kwa adui zao waliowazunguka hata wasiweze tena kuwapinga. 15Kila walipokwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi-Mungu uliwakabili kuwaletea balaa, kama alivyokuwa amewaonya na kuapa. Nao wakawa katika huzuni kubwa.
16Ndipo Mwenyezi-Mungu akawapa waamuzi ambao waliwaokoa mikononi mwa watu waliopora mali zao. 17Hata hivyo, Waisraeli hawakuwasikiliza waamuzi wao, maana walifanya kama wazinzi kwa kufuata miungu mingine na kuisujudia. Waliacha upesi nyayo walizofuata babu zao ambao walitii amri za Mwenyezi-Mungu; bali wao hawakufanya hivyo. 18Kila mara Mwenyezi-Mungu alipowapelekea mwamuzi, yeye mwenyewe alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa mikononi mwa adui zao muda wote wa uhai wa mwamuzi huyo. Aghalabu, Mwenyezi-Mungu aliwaonea huruma aliposikia kilio chao kutokana na mateso na dhuluma walizofanyiwa. 19Lakini kila mara mwamuzi alipofariki walirudia mienendo yao ya zamani, wakaishi vibaya kuliko babu zao. Waliifuata miungu mingine, wakaitumikia na kuisujudia, wala hawakuyaacha matendo yao wala ukaidi wao. 20Kwa hiyo Mwenyezi-Mungu akawaka hasira dhidi ya Waisraeli, akasema, “Kwa kuwa watu hawa wamevunja agano nililofanya na babu zao, wakakataa kutii sauti yangu, 21sitayafukuza tena mataifa ambayo Yoshua aliyabakiza, wakati alipofariki. 22Nitayatumia mataifa hayo kuwajaribu Waisraeli nione kama watairudia njia yangu kama babu zao au sivyo.” 23Basi, Mwenyezi-Mungu akayaacha mataifa hayo, wala hakuyafukuza mara moja, wala hakumpa Yoshua ushindi juu ya mataifa hayo!

Waamuzi 2;1-23

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.