Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 29 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 14...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni
Uhimidiwe Jehovah,Uabudiwe Yahweh..
Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu
Matendo yako yatisha,Hakuna kama wewe Mungu wetu
wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Alfa na omega..!!
Neema yako yatutosha ee Mungu wetu..!!


Kauli ya Mungu aliyoiona nabii Habakuki. “Ee Mwenyezi-Mungu, nitakulilia mpaka lini, nawe usinisikilize na kunisaidia? Kwa nini nalia: ‘Dhuluma’ nawe hutuokoi? Kwa nini wanifanya nishuhudie mabaya na taabu? Uharibifu na ukatili vinanizunguka, ugomvi na mashindano yanazuka. Hivyo sheria haina nguvu, wala haki haitekelezwi. Waovu wanawazunguka waadilifu, hivyo hukumu hutolewa ikiwa imepotoshwa.”

Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kwakupigwa kwake sisi tumepona...!!


Mungu akasema: “Yaangalie mataifa, uone! Utastaajabu na kushangaa. Maana ninatenda kitu ukiwa bado unaishi, kitu ambacho ungeambiwa hungesadiki. Maana ninawachochea Wakaldayo, taifa lile kali na lenye hamaki! Taifa lipitalo katika nchi yote, ili kunyakua makao ya watu wengine. Wao ni watu wa kuchukiza na kutisha; wao hujiamulia wenyewe nini haki na adhama. “Farasi wao ni wepesi kuliko chui; wakali kuliko mbwamwitu wenye njaa. Wapandafarasi wao wanatoka mbali, wanaruka kasi kama tai arukiavyo mawindo. “Wote wanakuja kufanya ukatili; kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele, wanakusanya mateka wengi kama mchanga. Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka. Kisha wanasonga mbele kama upepo, wafanya makosa na kuwa na hatia, maana, nguvu zao ndizo mungu wao!”

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
ukatupe kama inavyokupendeza wewe....



Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,
Familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Yahweh tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya
Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia
Mungu wetu tukawe salama rohoni
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu
popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni
Ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni
tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe
Roho Matakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....


“Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu, tangu kale na kale? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu; Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu! Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu, huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya. Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao? “Umewafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe vitambaavyo visivyo na kiongozi! Wakaldayo huwavua watu kwa ndoana, huwavutia nje kwa wavu wao, huwakusanya wote katika jarife lao, kisha hufurahi na kushangilia. Kwa hiyo, wanazitambikia nyavu zao, na kuzifukizia ubani; maana kwa hizo huweza kuishi kwa anasa, na kula chakula cha fahari. “Je, hawataacha kamwe kuvuta upinde wao? Je, wataendelea tu kuwanasa watu, na kuyaangamiza mataifa bila huruma?

Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.





Shughuli za Daudi Yerusalemu

(2Sam 5:11-16)

1Kisha mfalme Hiramu wa Tiro alituma wajumbe kwa Daudi, pia alimpelekea mierezi, waashi na maseremala, ili wamjengee Daudi ikulu. 2Hivyo, Daudi akatambua kwamba Mwenyezi-Mungu amemwimarisha awe mfalme wa Israeli, na kwamba ufalme wake umekuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.
3Huko Yerusalemu, Daudi alioa wake wengi zaidi, naye akazaa wana na mabinti wengine. 4Yafuatayo ndio majina ya watoto aliozaa huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 5Ibhari, Elishua, Elpeleti, 6Noga, Nefegi, Yafia, 7Elishama, Beeliada na Elifeleti.

Ushindi dhidi ya Wafilisti

(2Sam 25:17-25)

8Wafilisti waliposikia kwamba Daudi amepakwa mafuta kuwa mfalme wa nchi nzima ya Israeli, wote walitoka kwa wingi kwenda kumtafuta. Daudi alipopata habari, alitoka kwenda kuwakabili. 9Wafilisti walifika wakaanza mashambulizi katika bonde la Refaimu. 10Ndipo Daudi alipomwuliza Mungu shauri, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Naye Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”
11Basi, Daudi akaenda huko Baal-perasimu, akawashinda; halafu akasema, “Mungu amepita katikati ya adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo panaitwa Baal-perasimu.14:11 Baal-perasimu: Kiebrania maana yake “Bwana apitaye katikati.” 12Wafilisti walipokimbia, waliziacha sanamu za miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri zote zichomwe moto.
13Kisha Wafilisti walifanya mashambulizi katika bonde hilo kwa mara ya pili. 14Safari hii, Daudi alipoomba shauri kwa Mungu, Mungu akamwambia, “Usiwashambulie kutoka hapa, ila zunguka na kuwashambulia kutoka mkabala na miti ya miforosadi, halafu washambulie kutoka huko. 15Na mara utakaposikia vishindo vya gwaride kwenye vilele vya hiyo miforosadi, haya, toka uende vitani. Nitakuwa nimekwisha kukutangulia kulipiga jeshi la Wafilisti.” 16Daudi alifanya kama alivyoamriwa na Mungu. Alilipiga jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni hadi Gezeri. 17Daudi akawa maarufu kote nchini, naye Mwenyezi-Mungu akayatia hofu mataifa yote, nayo yakamwogopa sana.



1Mambo ya Nyakati14;1-17


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday, 28 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 13...





Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua
na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!



Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya taabu zitakazowajieni. Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Nyinyi mmejirundikia mali katika siku hizi za mwisho! Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. Mmemhukumu na kumuua mtu asiye na hatia, naye hakuwapingeni!


Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tuaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya 
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza
 kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi
wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza 
ili sisi tupate kupona...




Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli. Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia. Ndugu zangu, msinung'unikiane nyinyi kwa nyinyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia. Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana. Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.



Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi



Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu. Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa. Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa. Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi. Elia alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua isinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa mazao yake. Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine akamrudisha, fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.

Mungu Baba tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu
wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.


Sanduku la agano lasimamishwa Kiriath-yearimu

(2Sam 6:1-11)

1Daudi alishauriana na makamanda wa vikosi vya maelfu na vikosi vya mamia, pamoja na viongozi wote. 2Kisha akawaambia Waisraeli wote waliokusanyika, “Ikiwa mtakubaliana nami, na ikiwa ni mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na tufanye hivi: Tutume wajumbe waende wakawaite ndugu zetu waliobaki nchini Israeli, pamoja na makuhani na Walawi walioko katika miji yao na malisho yao, waje wajumuike pamoja nasi. 3Kisha twende tukalichukue sanduku la agano la Mungu wetu, maana hatukulijali wakati wa utawala wa mfalme Shauli.” 4Watu wote walikubaliana na pendekezo hilo kwani waliliona kuwa jambo jema.
5Hivyo, Daudi aliwakusanya Waisraeli wote nchini; toka kijito cha Shihori kilichoko Misri, hadi maingilio ya Hamathi ili kulileta sanduku la Mungu toka Kiriath-yearimu. 6Daudi, akiandamana na Waisraeli wote, akaenda hadi mjini Baala, yaani Kiriath-yearimu, nchini Yudea, ili kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe vyenye mabawa. 7Basi, wakalichukua sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Abinadabu kwa gari jipya. Uza na Ahio waliliendesha gari hilo. 8Daudi na Waisraeli wote wakawa wanacheza kwa nguvu zao zote, mbele ya Mungu. Waliimba huku wanapiga ala za muziki zilizotengenezwa kwa mvinje: Vinubi, vinanda, matari, matoazi na tarumbeta.
9Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Kidoni, Uza aliunyosha mkono wake kulishikilia sanduku la agano kwa sababu ng'ombe walijikwaa. 10Mara Mwenyezi-Mungu akamkasirikia Uza kwa kulishika sanduku, akamuua. Uza akafa papo hapo mbele ya Mungu. 11Daudi alikasirika kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimuua Uza akiwa na hasira. Kwa sababu hiyo, mahali hapo huitwa Peres-uza13:11 Peres-uza: Kiebrania maana yake “Pigo la Uza”. hadi leo. 12Siku hiyo Daudi akamwogopa Mungu, akasema, “Sasa, nitawezaje kulichukua sanduku la Mungu nyumbani mwangu?” 13Basi, Daudi hakulichukua sanduku mpaka mji wa Daudi,13:13 mji wa Daudi: Yaani: Yerusalemu. bali alilipeleka nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. 14Sanduku hilo la Mungu lilikaa huko kwa Obed-edomu kwa muda wa miezi mitatu, naye Mwenyezi-Mungu akaibariki nyumba ya Obed-edomu na mali yake yote.


1Mambo ya Nyakati13;1-14


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday, 27 May 2018

Natumai Jumapili ilikuwa/inaendelea Vyema;Burudani-NAKUSHUKURU MUNGU,AUNGURUMAPO SIMBA,KWA NEEMA - UKOMBOZI KKKT MSASANI






Wapendwa/waungwana  Nimatumaini yangu mmekuwa na jumapili njema
Hapa kwetu ni salama kabisa na Mungu ametupa kibali cha kushiriki ibada na wapendwa 
wengine kanisani...
Basi muendelee luwa na wakati mwema na Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea
sawasawa na mapenzi yake.....


Neno La leo;Yakobo 4;1-17


Mapigano na ugomvi wote kati yenu vinatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu. Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani sana kupata vitu, lakini hamvipati; hivyo mnagombana na kupigana. Hampati kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mungu. Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu. Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure, yanaposema: “Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa.” Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.” Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni. Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki! Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa. Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni. Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu. Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako? Basi, sasa sikilizeni nyinyi mnaosema: “Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na kupata faida.” Nyinyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Nyinyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena. Mngalipaswa kusema: “Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au kile.” Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya. Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi.














"Sawahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Friday, 25 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 12...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye huruma,Mungu mwenye upendo
Mungu wa walio hai,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo
Mungu wa baraka,Mungu unaye jibu,Mungu unayesikia,Mungu wetu
ni Mungu wa haki.....
Unatosha ee Baba wa Mbinguni,Utukuzwe ee Mungu  wetu
Hakuna kama wewe Jehovah Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shalom...!
Emanuel-Mungu pamoja nasi...!!!

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudishia ee Baba wa Mbinguni....!!


Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Mwenye mwenendo mnyofu humcha Mwenyezi-Mungu, lakini mpotovu humdharau Mungu. Mpumbavu hujiadhibu mwenyewe kwa kuropoka kwake, lakini mwenye hekima hulindwa na maneno yake. Bila ng'ombe wa kulima ghala za mtu ni tupu, mavuno mengi hupatikana kwa nguvu ya ng'ombe wa kulima. Shahidi mwaminifu hasemi uongo, lakini asiyeaminika hububujika uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima bure, lakini mwenye busara hupata maarifa kwa urahisi. Ondoka mahali alipo mpumbavu, maana hapo alipo hamna maneno ya hekima. Hekima ya mwenye busara humwonesha njia yake, lakini upumbavu wa wapumbavu huwadanganya wenyewe. Wapumbavu huchekelea dhambi, bali wanyofu hupata fadhili kwa Mungu.

Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....




Moyo waujua uchungu wake wenyewe, wala mgeni hawezi kushiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa, lakini hema ya wanyofu itaimarishwa. Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo. Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi. Mtu mpotovu atavuna matunda ya mwenendo wake, naye mtu mwema atapata tuzo la matendo yake. Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari. Mwenye hekima ni mwangalifu na huepa uovu, lakini mpumbavu hajizuii wala hana uangalifu. Mwenye kuwaka hasira haraka hutenda kipumbavu, lakini mwenye busara ana uvumilivu. Wajinga hurithi upumbavu, lakini wenye busara hutuzwa taji ya maarifa. Waovu watapiga magoti mbele ya watu wema, watu wabaya mlangoni mwa waadilifu. Maskini huchukiwa hata na jirani yake, lakini tajiri ana marafiki wengi. Anayemdharau jirani yake ni mwenye dhambi, bali ana heri aliye mwema kwa maskini. Anayepanga maovu kweli anakosea! Wanaopanga kutenda mema hufadhiliwa.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
ukatupe kama inavyokupendeza wewe....

Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,
Familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Yahweh tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya
Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na kwavyote tunavyo vimiliki
Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia
Mungu wetu tukawe salama rohoni
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu
popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni
Ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni
tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe
Roho Matakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...





Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini. Mali ni taji ya fahari ya wenye hekima, lakini ujinga ni shada la wapumbavu. Shahidi wa kweli huokoa maisha, lakini msema uongo ni msaliti. Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni chemchemi ya uhai; humwezesha mtu kuepa mitego ya kifo. Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake, lakini bila watu mtawala huangamia. Mtu asiye mwepesi wa hasira ana busara kubwa, lakini akasirikaye upesi hukuza upumbavu. Amani rohoni humpa mtu afya, lakini tamaa huozesha mifupa. Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu. Mwovu huangamizwa kwa matendo yake maovu, lakini mwadilifu hupata usalama kwa unyofu wake. Hekima imo moyoni mwa mtu mwenye busara; haipatikani kamwe mioyoni mwa wapumbavu. Uadilifu hukuza taifa, lakini dhambi ni balaa kwa taifa lolote. Mfalme humfadhili mtumishi atendaye kwa hekima, lakini hasira yake huwakumba watendao yasiyofaa.


Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
wenye shida/tabu,wagonjwa,wenye njaa na kila mmoja
na mahitaji yake..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawaokoe na kuwavusha salama
Yahweh tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Mungu wetu tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
Baba wa Mbinguni ukawape macho ya rohoni na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,amani ikatawale..
Ee Baba tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.


Wafuasi wa kwanza wa Daudi kutoka Benyamini

1Hawa ni wanaume ambao walijiunga na Daudi huko Siklagi, alipokuwa hana uhuru wowote wa kutembea kwa sababu ya mfalme Shauli mwana wa Kishi; walikuwa miongoni mwa askari mashujaa waliomsaidia vitani. 2Hao walikuwa watu wa kabila la Benyamini kama alivyokuwa Shauli. Walikuwa wapiga upinde hodari, na warusha mawe kwa kombeo kwa kutumia mikono yote, wa kulia na kushoto. 3Kiongozi wao alikuwa Ahiezeri, aliyesaidiwa na Yoashi, wote wana wa Shemaa kutoka Gibea; wengineo ni: Yezieli na Peleti, wana wa Azmawethi, Beraka, Yehu kutoka Anathothi, 4Ishmaya kutoka Gibeoni, mtu shujaa miongoni mwa wale thelathini na kiongozi wao pia pamoja na Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi kutoka Gedera, 5Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi, 6Elkana, Ishia, Azareli, Yoezeri, Yashobeamu kutoka ukoo wa Kora 7na Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.

Wafuasi wa Daudi kutoka kabila la Gadi

8Tena, watu kutoka kabila la Gadi walijiunga na Daudi akiwa ngomeni kule nyikani. Hawa walikuwa askari wenye nguvu na uzoefu, hodari wa kutumia ngao na mkuki; wenye nyuso za kutisha kama simba na wepesi kama swala milimani. 9Kiongozi wao mkuu alikuwa Ezeri, wa pili Obadia, wa tatu Eliabu, 10wa nne Mishmana, wa tano Yeremia, 11wa sita Atai, wa saba Elieli, 12wa nane Yohanani, wa tisa Elsabadi, 13wa kumi Yeremia, na wa kumi na moja Makbanai. 14Wagadi hao, walikuwa maofisa wa jeshi. Kulingana na vyeo vyao, mdogo alisimamia kikosi cha wanajeshi 100, na mkubwa alisimamia kikosi cha wanajeshi 1,000. 15Hawa ndio watu waliovuka mto Yordani mnamo mwezi wa kwanza, mto ulipokuwa umefurika pande zote na kuwatawanya watu mashariki na magharibi ya mto.

Wafuasi kutoka Benyamini na Yuda

16Baadhi ya watu kutoka makabila ya Benyamini na Yuda walifika ngomeni alipokuwa Daudi. 17Daudi akatoka nje kuwalaki, akawaambia, “Ikiwa mmekuja kwangu kama marafiki ili kunisaidia basi nawapokea kwa moyo wote, lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa maadui zangu, ingawa sijatenda ovu lolote, Mungu wa baba zetu awaone na awakemee.” 18Hapo Roho akamjia Abishai, mkuu wa hao watu thelathini, naye akasema,
“Sisi tu watu wako, ee Daudi,
tuko upande wako, ee mwana wa Yese!
Amani, amani iwe kwako,
na amani iwe kwa yeyote akusaidiaye!
Maana akusaidiaye ndiye Mungu wako.”
Ndipo Daudi akawapokea na kuwafanya maofisa katika jeshi lake.

Wafuasi toka Manase

19Askari wengine wa kabila la Manase, walitoroka na kujiunga na Daudi, wakati alipoondoka pamoja na Wafilisti kwenda kupigana na mfalme Shauli. (Lakini hata hivyo, hakuwasaidia maana watawala wa Wafilisti walifanya shauri wamfukuze arudi Siklagi wakisema, “Tutayahatarisha maisha yetu kwa sababu atatutoroka arudi kwa bwana wake Shauli.”) 20Basi, Daudi alipokuwa Siklagi, watu wafuatao wa kabila la Manase walimwendea: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai. Kila mmoja wao alikuwa kiongozi wa kikosi cha watu 1,000 katika kabila la Manase. 21Walimsaidia Daudi kupigana na magenge ya washambuliaji,12:21 kupigana … washambuliaji: Au Kama maofisa wa jeshi lake. kwani wote walikuwa askari mashujaa na makamanda jeshini. 22Siku hata siku, watu walijiunga na Daudi kumsaidia, hatimaye akawa na jeshi kubwa sana, kama jeshi la Mungu.

Orodha ya majeshi ya Daudi

23Hii ndio idadi ya vikosi vya askari wenye silaha waliojiunga na Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Shauli, kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu: 24Watu wa kabila la Yuda waliokuwa na mikuki na ngao, walikuwa 6,800. Wote walikuwa na silaha zao. 25Kutoka kabila la Simeoni, watu 7,100 mashujaa na wenye ujuzi mwingi wa vita. 26Kutoka kabila la Lawi: Watu 4,600. 27Yehoyada, wa uzao wa Aroni na wenzake: Watu 3,700. 28Jamaa ya Sadoki, kijana hodari vitani, yeye pamoja na makamanda ishirini na wawili kutoka ukoo wa baba yake mwenyewe. 29Kutoka kabila la Benyamini, (kabila la Shauli): Watu 3,000. Wengi wao walibaki waaminifu kwa jamaa ya Shauli; 30Kutoka kabila la Efraimu: Watu 20,800, watu mashujaa sana tena mashuhuri katika koo zao; 31Kutoka nusu ya kabila la Manase: Watu 18,000, waliotajwa majina ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme. 32Kutoka kabila la Isakari: Wakuu 200 pamoja na ndugu zao wote waliokuwa chini ya amri yao. Wakuu hao walikuwa na elimu ya kujua mambo ya nyakati na walijua kilichowapasa Waisraeli kufanya. 33Kutoka kabila la Zebuluni: Watu 50,000; waaminifu na wazoefu wa vita. Walijiandaa na zana za vita za kila namna, lengo lao likiwa ni kumsaidia Daudi tu. 34Kutoka kabila la Naftali: Makamanda 1,000 pamoja na watu 37,000 wenye ngao na mikuki. 35Kutoka kabila la Dani: Watu 28,600 wenye silaha tayari kwa vita. 36Kutoka kabila la Asheri: Watu 40,000 wazoefu wa vita, tayari kwa mapigano. 37Kutoka kabila la Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kutoka ngambo ya mto Yordani: Watu 120,000 wenye kila aina ya silaha za vita.
38Wanajeshi hao wote, waliojiandaa tayari kabisa kwa vita, walikwenda Hebroni na nia yao kubwa ikiwa ni kumtawaza Daudi awe mfalme wa Israeli yote. Nao watu wote wa Israeli, pia waliungana wakiwa na nia moja ya kumtawaza Daudi awe mfalme.
39Basi, walikaa na Daudi kwa muda wa siku tatu, wakila na kunywa kwani ndugu zao walikuwa wamekwisha waandalia vyakula. 40Zaidi ya hayo, majirani zao wa karibu na hata wa mbali kama huko Isakari, Zebuluni na Naftali, waliwaletea vyakula walivyobeba kwa punda, ngamia, nyumbu na ng'ombe. Waliwaletea unga, mikate ya tini, vichala vya zabibu kavu, divai na mafuta, ng'ombe na kondoo wengi, kukawa na vyakula tele, kwani kulikuwa na furaha katika Israeli.



1Mambo ya Nyakati12;1-40


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.