|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Mfalme Dario aliamua kuteua wakuu 120 kusimamia mambo ya utawala. Aliwateua pia wakuu watatu, Danieli akiwa mmojawapo, wawasimamie wale wakuu wengine na maslahi ya mfalme, asije akapata hasara.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Muda si muda, Danieli akadhihirika kuwa bora kuliko wale wasimamizi wengine na wakuu wote kwa kuwa alikuwa na roho njema. Hivyo mfalme akanuia kumpa uongozi wa ufalme wote.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Wale wakuu pamoja na maliwali wakatafuta kisingizio cha kumshtaki Danieli kuhusu mambo ya ufalme, lakini hawakuweza kupata sababu ya kumlaumu, wala kosa lolote, kwani Danieli alikuwa mwaminifu. Hakupatikana na kosa, wala hatia yoyote.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
1Laiti ungekuwa kaka yangu,
ambaye amenyonyeshwa na mama yangu!
Hivyo, hata kama ningekutana nawe nje,
ningekubusu na hakuna ambaye angenidharau.
2Ningekuongoza na kukufikisha nyumbani kwa mama mzazi,
mahali ambapo ungenifundisha upendo.
Ningekupa divai nzuri iliyokolezwa,
ningekupa divai yangu ya makomamanga yangu.
3Mkono wako wa kushoto u chini ya kichwa changu,
na mkono wako wa kulia wanikumbatia.
4Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu,
msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,
hadi hapo wakati wake utakapofika.
Shairi la sita
Wanawake
5Ni nani huyu ajaye kutoka mbugani,
huku anamwegemea mpenzi wake?
Bibi arusi
Chini ya mtofaa, mimi nilikuamsha,
pale ambapo mama yako aliona uchungu,
naam, pale ambapo mama yako alikuzaa.
6Nipige kama mhuri moyoni mwako,
naam, kama mhuri mikononi mwako.
Maana pendo lina nguvu kama kifo,
wivu nao ni mkatili kama kaburi.
Mlipuko wake ni kama mlipuko wa moto,
huwaka kama mwali wa moto.
7Maji mengi hayawezi kamwe kulizima,
mafuriko hayawezi kulizamisha.
Mtu akijaribu kununua pendo,
akalitolea mali yake yote,
atakachopata ni dharau tupu.
Ndugu za Bibi arusi
8Tunaye dada mdogo,
ambaye bado hajaota matiti.
Je, tumfanyie nini dada yetu
siku atakapoposwa?
9Kama angalikuwa ukuta,
tungalimjengea mnara wa fedha;
na kama angalikuwa mlango,
tungalimhifadhi kwa mbao za mierezi.
Bibi arusi
10Mimi nalikuwa ukuta,
na matiti yangu kama minara yake.
Machoni pake nalikuwa
kama mwenye kuleta amani.
Bwana arusi
11Solomoni alikuwa ana shamba la mizabibu,
mahali paitwapo Baal-hamoni.
Alilikodisha kwa walinzi;
kila mmoja wao alilipa vipande elfu vya fedha.
12Shamba langu la mizabibu ni shamba langu mwenyewe,
naam, ni shamba langu binafsi!
Basi, Solomoni, wewe ukae na elfu zako za fedha,
na kila mlinzi wa matunda akae na mia mbili zake.
13Ewe uliye shambani,
rafiki zangu wanasikiliza sauti yako;
hebu nami niisikie tafadhali!
Bibi arusi
14Njoo haraka ewe mpenzi wangu,
kama paa au mwanapaa dume juu ya milima ya manukato.
Wimbo Ulio Bora8;1-14
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.