Mtoto amezaliwa kwetu
1 9:1 Taz Mat 4:15
Lakini nchi ile iliyokuwa imekumbwa na huzuni haitabaki daima katika giza hilo kuu. Hapo awali Mungu alizifedhehesha nchi za Zebuluni na Naftali, lakini siku za usoni ataifanikisha sehemu hii ya baharini na nchi iliyo ngambo ya Yordani na hata Galilaya wanamoishi watu wa mataifa.
2 9:2 Taz Mat 4:16; Luka 1:79 Watu waliotembea gizani
wameona mwanga mkubwa.
Watu walioishi katika nchi ya giza kuu,
sasa mwanga umewaangazia.
3Wewe, ee Mungu, umelikuza taifa,
umeiongeza furaha yake.
Watu wanafurahi mbele yako,
wana furaha kama wakati wa mavuno,
kama wafurahivyo wanaogawana nyara.
4Maana nira nzito walizobeba,
nira walizokuwa wamefungwa,
na fimbo ya wanyapara wao,
umezivunjavunja kama wakati wa Wamidiani.
5Viatu vyote vya washambulizi vitani
na mavazi yote yenye madoa ya damu
yatateketezwa kama kuni za kuwasha moto.
6Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu,
tumepewa mtoto wa kiume.
Naye atapewa mamlaka ya kutawala.
Ataitwa: “Mshauri wa Ajabu”.
“Mungu Mwenye Nguvu”,
“Baba wa Milele”,
“Mfalme wa Amani”.
7 9:7 Taz Luka 1:32-33 Utawala wake utastawi daima,
amani ya ufalme wake haitakoma.
Atachukua wadhifa wa mfalme Daudi
na kutawala juu ya ufalme wake;
ataustawisha na kuuimarisha,
kwa haki na uadilifu,
tangu sasa na hata milele.
Hayo atayafanya Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Adhabu ya Waisraeli
8Mwenyezi-Mungu ametoa tamko dhidi ya Yakobo
nalo litampata Israeli.
9Watu wote watatambua,
ukoo wote wa Efraimu
na wakazi wa Samaria.
Kwa kiburi na majivuno wanasema:
10“Kuta za matofali zimeanguka
lakini sisi tutazijenga kwa mawe yaliyochongwa!
Nyumba za boriti za mikuyu zimeharibiwa
lakini mahali pake tutajenga za mierezi.”
11Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani
na kuwachochea maadui zao.
12Waaramu upande wa mashariki,
Wafilisti upande wa magharibi,
wamepanua vinywa vyao kuimeza Israeli.
Hata hivyo, hasira yake haijatulia,
bado ameunyosha mkono wake.
13Ingawa aliwaadhibu watu,
hawakumrudia Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
14Basi kwa muda wa siku moja tu,
Mwenyezi-Mungu atakata katika Israeli vichwa na mikia,
tawi la mtende na nyasi:
15Vichwa ndio wazee na waheshimiwa,
mikia ndio manabii wafundishao uongo.
16Wale wanaoongoza watu hawa wamewapotosha,
na hao wanaoongozwa nao wamepotoka.9:16 wamepotoka: Au wamemezwa.
17Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu hawahurumii9:17 hawahurumii: Kufuatana na hati moja ya kale. Kiebrania: Hapendezwi. vijana wao,
hana huruma juu ya yatima na wajane wao;
kwani hakuna hata mmoja amchaye Mungu,
kila mtu husema uongo.
Hata hivyo, hasira yake haijatulia,
bado ameunyosha mkono wake.
18Uovu huwaka kama moto
uteketezao mbigili na miiba;
huwaka kama moto msituni,
na kutoa moshi mzito upandao angani juu.
19Kwa ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi
nchi imechomwa moto,
na watu ni kama kuni za kuuwasha.
Hakuna mtu anayemhurumia ndugu yake;
20wananyanganya upande mmoja na hawatosheki;
wanakula upande mwingine lakini hawashibi.
Kila mmoja anamshambulia mwenzake.9:20 anamshambulia mwenzake: Kiebrania: Anakula nyama ya mwenzake.
21Manase dhidi ya Efraimu,
Efraimu dhidi ya Manase
na wote wawili dhidi ya Yuda.
Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia,
bado ameunyosha mkono wake.
Isaya9;1-21
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.