|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Wastahili sifa, ee Mungu, huko Siyoni, watu watakutimizia wewe ahadi zao, maana wewe wajibu sala zetu. Binadamu wote watakujia wewe.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Tunapolemewa na makosa yetu, wewe mwenyewe watusamehe. Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu, waishi katika maskani yako. Sisi tutatoshelezwa na mema ya nyumba yako; mema ya hekalu lako takatifu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Kwa matendo yako makuu watuitikia na kutuokoa, ewe Mungu wa wokovu wetu; wewe ndiwe tumaini la viumbe vyote, duniani kote na mbali baharini.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
Njoni hata kama hamna fedha
1Haya! Kila mwenye kiu na aje kwenye maji!
Njoni, nyote hata msio na fedha;
nunueni ngano mkale,
nunueni divai na maziwa.
Bila fedha, bila gharama!
2Mbona mnatumia fedha yenu
kwa ajili ya kitu kisicho chakula?
Ya nini kutoa jasho lenu kwa kitu kisichoshibisha?
Nisikilizeni mimi kwa makini,
nanyi mtakula vilivyo bora,
na kufurahia vinono.
3Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu;
nisikilizeni, ili mpate kuishi.
Nami nitafanya nanyi agano la milele;
nitawapeni fadhili nilizomwahidi Daudi.
4Mimi nilimfanya kiongozi na kamanda wa mataifa
ili yeye anishuhudie kwa watu wa mataifa.
5Sasa utayaita mataifa usiyoyajua,
watu wa mataifa yasiyokutambua watakujia mbio,
kwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;
kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeli
niliyekufanya wewe utukuke.”
6Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana,
mwombeni msaada wakati yupo bado karibu.
7Waovu na waache njia zao mbaya,
watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya;
wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia,
wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe.
8Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Mawazo yangu si kama mawazo yenu,
wala njia zangu si kama njia zenu.
9Kama vile mbingu zilivyo mbali na dunia,
ndivyo njia zangu zilivyo mbali na zenu,
na mawazo yangu mbali na mawazo yenu.
10Kama vile mvua na theluji ishukavyo toka mbinguni,
wala hairudi huko bali huinywesha ardhi,
ikaifanya ichipue mimea ikakua,
ikampatia mpanzi mbegu na kuwapa watu chakula,
11vivyo hivyo na neno langu mimi:
Halitanirudia bila mafanikio,
bali litatekeleza matakwa yangu,
litafanikiwa lengo nililoliwekea.
12“Mtatoka Babuloni kwa furaha;
mtaongozwa mwende kwa amani.
Milima na vilima mbele yenu vitapaza sauti na kuimba,
na miti yote mashambani itawapigia makofi.
13Badala ya michongoma kutamea misonobari,
na badala ya mbigili kutamea mihadasi.
Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu
juu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu;
ishara ya milele ambayo haitafutwa.”
Isaya55;1-13
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.