|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "AMOSI" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki... Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"OBADIA"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!!
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Dhoruba iliendelea kuvuma na kesho yake wakaanza kutupa nje shehena ya meli. Siku ya tatu, wakaanza pia kutupa majini vifaa vya meli kwa mikono yao wenyewe.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula, Paulo alisimama kati yao, akasema, “Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kama mngalinisikiliza na kuacha kusafiri kutoka Krete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepuka shida hii na hasara hizi zote.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Maono ya Obadia. Mambo aliyosema Bwana Mwenyezi-Mungu kuhusu taifa la Edomu.
Mwenyezi-Mungu ataadhibu Edomu
Tumepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu;
mjumbe ametumwa kati ya mataifa:
“Inukeni! Twende tukapigane na Edomu!”
2Mwenyezi-Mungu aliambia taifa la Edomu:
“Nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa,
utadharauliwa kabisa na wote.
3Kiburi chako kimekudanganya:
Kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imara
na makao yako yapo juu milimani,
hivyo wajisemea,
‘Nani awezaye kunishusha chini?’
4Hata ukiruka juu kama tai,
ukafanya makao yako kati ya nyota,
mimi nitakushusha chini tu.
Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
5“Kama wezi au wanyang'anyi wangekujia usiku,
je, wasingechukua tu kiasi cha kuwatosha?
Ikiwa wavunaji zabibu wangekujia,
je, wasingekuachia kiasi kidogo tu?
Lakini wewe, adui zako wamekuangamiza kabisa.
6Enyi wazawa wa Esau, mali zenu zimetekwa;
hazina zenu zote zimeporwa!
7Washirika wenzenu wamewadanganya,
wamewafukuza nchini mwenu.
Mliopatana nao wamewashinda vitani,
rafiki wa kutegemewa ndio waliokutegea mitego,
nawe hukuelewa yaliyokuwa yanatendeka.
8Mimi Mwenyezi-Mungu nakuuliza hivi:
Je, siku hiyo, sitawaangamiza wenye hekima kutoka Edomu
na wenye maarifa kutoka mlima Esau?
9Ewe Temani, mashujaa wako watatishika
na kila mtu atauawa mlimani Esau.
Sababu za Edomu kuadhibiwa
10“Kwa sababu ya matendo maovu
mliyowatendea ndugu zenu wazawa wa Yakobo,
mtaaibishwa na kuangamizwa milele.
11Siku ile mlisimama kando mkitazama tu,
wakati wageni walipopora utajiri wao,
naam, wageni walipoingia malango yao
na kugawana utajiri wa Yerusalemu kwa kura.
Kwa hiyo nanyi mlitenda kama wazawa wao.
12Msingalifurahia siku hiyo ndugu zenu walipokumbwa na mikasa;
msingaliwacheka Wayuda
na kuona fahari wakati walipoangamizwa;
msingalijigamba wenzenu walipokuwa wanataabika.
13Msingeliingia katika mji wa watu wangu,
siku walipokumbwa na maafa;
msingelipora mali zao, siku hiyo ya maafa yao.
14Msingelisimama kwenye njia panda
na kuwakamata wakimbizi wao;
wala msingeliwakabidhi kwa adui zao
wale waliobaki hai.
Mungu atayahukumu mataifa
15“Siku inakaribia ambapo mimi Mwenyezi-Mungu
nitayahukumu mataifa yote.
Kama mlivyowatendea wengine, ndivyo mtakavyotendewa,
mtalipwa kulingana na matendo yenu.
16Maana, kama walivyokunywa kikombe cha ghadhabu yangu
kwenye mlima wangu mtakatifu
ndivyo na mataifa jirani yatakavyokunywa;
watakunywa na kupepesuka,
wataangamia kana kwamba hawakuwahi kuwapo duniani.
Waisraeli watashinda
17“Lakini mlimani Siyoni watakuwapo wale waliosalimika
nao utakuwa mlima mtakatifu.
Wazawa wa Yakobo wataimiliki tena nchi iliyokuwa yao.
18Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto
na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto.
Watawaangamiza wazawa wa Esau
kama vile moto uteketezavyo mabua makavu,
asinusurike hata mmoja wao.
Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
19Wale wanaokaa Negebu wataumiliki mlima Esau;
wale wanaokaa Shefela wataimiliki nchi ya Wafilisti.
Waisraeli watamiliki nchi za Efraimu na Samaria
na watu wa Benyamini wataimiliki nchi ya Gileadi.
20Waisraeli walio uhamishoni Hala
wataimiliki Foinike hadi Sarepta.
Watu wa Yerusalemu walio uhamishoni Sefaradi
wataimiliki miji ya Negebu.
21Waokoaji watapanda juu ya mlima Siyoni
ili kuutawala mlima Esau;
naye Mwenyezi-Mungu atakuwa ndiye Mfalme.”
Obadia1;1-21
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe