|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "YONA" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki... Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"MIKA"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!!Tumshukuru Mungu wetu katika yote...Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Kisha Elifazi, Mtemani, akajibu: “Je, mtu wa hekima hujibu kwa maneno ya upuuzi? Je, mtu huyo amejaa maneno matupu? Je, mwenye hekima hujitetea kwa maneno yasiyofaa, au kwa maneno yasiyo na maana?
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Lakini wewe unapuuza uchaji wa Mungu; na kuzuia kutafakari mbele ya Mungu. Uovu wako ndio unaokifundisha kinywa chako, nawe wachagua kusema kama wadanganyifu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Maneno yako mwenyewe yanakuhukumu, sio mimi; matamshi yako yashuhudia dhidi yako. Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Je, wewe ulizaliwa kabla ya kuweko vilima? Je, ulipata kuweko katika halmashauri ya Mungu? au, wewe ndiwe peke yako mwenye hekima?
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Mika, mwenyeji wa Moreshethi, wakati Yothamu, Ahazi na Hezekia walipokuwa wafalme wa Yuda. Mika aliona mambo yote haya kuhusu Samaria na Yerusalemu.
Mwenyezi-Mungu aja kuhukumu
2Sikilizeni enyi watu wote;
sikiliza ewe dunia na vyote vilivyomo.
Mwenyezi-Mungu anakuja kuwashtaki,
Bwana anena kutoka hekalu lake takatifu.
3Naam! Mwenyezi-Mungu yuaja kutoka makao yake;
atashuka na kutembea juu ya vilele vya dunia.
4Milima itayeyuka chini ya nyayo zake,
kama nta karibu na moto;
mabonde yatapasuka,
kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.
5Haya yote yatatukia
kwa sababu ya makosa ya wazawa wa Yakobo,
kwa sababu ya dhambi za wazawa wa Israeli.
Je, uhalifu wa Yakobo waonekana wapi?
Katika mji wake mkuu Samaria!
Je, uhalifu wa Yuda waonekana wapi?
Katika Yerusalemu kwenyewe!
6Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Mji wa Samaria nitaufanya magofu nyikani,
shamba ambalo watu watapanda mizabibu.
Mawe yaliyoujenga nitayatupa bondeni,
na misingi yake nitaichimbuachimbua.
7Sanamu zake zote zitavunjwavunjwa,
kila kilichochumwa kitateketezwa kwa moto.
Vinyago vyake vyote nitaviharibu.
Vilirundikwa kutokana na ujira wa malaya,
navyo vitatumiwa tena kulipia umalaya.”
Nabii anaomboleza juu ya Yerusalemu na Yuda
8Kwa sababu hiyo, mimi nitalia na kuomboleza;
nitatembea uchi na bila viatu.
Nitaomboleza na kulia kama mbweha,
nitasikitika na kulia kama mbuni.
9Majeraha ya Samaria hayaponyeki,
nayo yameipata pia Yuda;
yamefikia lango la Yerusalemu,
mahali wanapokaa watu wangu.
10Msiitangaze habari hii huko Gathi,
wala msilie machozi!
Huko Beth-leafra mgaegae mavumbini kwa huzuni.
11Nendeni enyi wakazi wa Shafiri,
mkiwa uchi na wenye haya.
Wakazi wa Zaanani msitoke nje ya mji wenu.
Watu wa Beth-ezeli wanalia;
msaada wao kwenu umeondolewa.
12Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa,
lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu
karibu kabisa na lango la Yerusalemu.
13Enyi wakazi wa Lakishi,
fungeni farasi wepesi na magari ya vita.
Nyinyi mlikuwa mmeiga dhambi ya watu wa Siyoni,
makosa ya Waisraeli yalikuwa kwenu.
14Hivyo, mnapaswa kuagana na kuwaacha wakazi wa Morasheth-gathi.
Nao mji wa Akzibu hautawasaidia wafalme wa Israeli,
15Enyi wakazi wa Maresha,
Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka.
Viongozi waheshimiwa wa Israeli
watakimbilia pangoni huko Adulamu.
16Enyi watu wa Yuda, nyoeni upara
kuwaombolezea watoto wenu wapenzi;
panueni upara wenu uwe mpana kama wa tai,
maana watoto wenu watawaacha kwenda uhamishoni.
Mika1;1-16
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe