|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki/Mwezi mwingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!
Kisha, nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu. Njoni mkaitafune miili ya wafalme, ya majemadari, ya watu wenye nguvu, ya farasi na wapandafarasi wao; njoni mkaitafune miili ya watu wote: Walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.” Ufunuo 19:17-18 |
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....
Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake.
Ufunuo 19:19
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake). Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti. Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.
Ufunuo 19:20-21
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimamie Neno lako nalo likawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.
Mungu anaahidi ukombozi 1Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika.
Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua;
ndiye awapaye watu mvua za rasharasha,
na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.
2Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu,
na waaguzi wao wanaagua uongo;
watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu,
na kuwapa watu faraja tupu.
Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo;
wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.
3Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji,
nami nitawaadhibu hao viongozi.10:3 viongozi: Kiebrania: Beberu.
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,
nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.
Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
4Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:
Watawala wa kila namna,
viongozi imara kama jiwe kuu la msingi,
walio thabiti kama kigingi cha hema,
wenye nguvu kama upinde wa vita.
5Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitani
watawakanyaga maadui zao katika tope njiani.
Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao;
nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
6“Watu wa Yuda nitawaimarisha;
nitawaokoa wazawa wa Yosefu.
Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma,
nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa.
Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao,
nami nitayasikiliza maombi yao.
7Watu wa Efraimu watakuwa kama mashujaa vitani;
watajaa furaha kama waliokunywa divai.
Watoto wao wataona hayo na kufurahi,
watajaa furaha mioyoni kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu.
8“Nitawaita watu wangu
na kuwakusanya pamoja;
nimekusudia kuwakomboa,
nao watakuwa wengi kama hapo awali.
9Japo niliwatawanya kati ya mataifa,
hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo.
Nao pamoja na watoto wao wataishi
na kurudi majumbani mwao.
10Nitawarudisha kutoka nchini Misri,
nitawakusanya kutoka Ashuru;
nitawaleta nchini Gileadi na Lebanoni,
nao watajaa kila mahali nchini.
11Watapitia katika bahari ya mateso,10:11 mateso: Au Misri.
nami nitayapiga mawimbi yake,
na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka.
Kiburi cha Ashuru kitavunjwa
na nguvu za Misri zitatoweka.
12Mimi nitawaimarisha watu wangu,
nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Zekaria10;1-12
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe