Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 14 August 2012

Siku kama ya Leo da'Leyla Kiwinga Alizaliwa;Burudani-Lady Jaydee - Shamba!!!!!




 Siku kama ya Leo,Familia ya Bibi na Bwana M.S.Kiwinga Walipata Mtoto wa kike na Wakamwita LEYLA.
Naye ndiye Funga Dimba[Mtoto wa Mwisho] wa Familia hiyo.
Da'Leyla Tunakutakia kila lililo Jema Maishani.MUNGU Azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo Leo.Akupe sawaswa na Mapenzi Yake,Uwe baraka kwa Watu Woote.

Pamoja Sana. MUNGU NI PENDO



Sunday, 12 August 2012

Nawatakia J'Pili Njema,Burudani;Usinipite Mwokozi -Lydiah Joy Kaimuri;Sarah k-Niinue;Unibariki-Hellen Ken!!!!

Wapendwa Nawatakia J'Pili yenye Upendo,Amani na Furaha.

Nanyi mkiwa katika kusali,msipayuke-payuke,kama watu wa mataifa,maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa Mengi.

Neno la Leo;Mathayo Mtakatifu:6;7-13.

MUNGU Atubariki Sote.

Saturday, 11 August 2012

Chaguo la Mswahili Leo;[Mambo ya Pwani]Top in Town -Khadija Koppa,Omar Koppa;Nifagilieni na Kitchen Party!!!


Malkia wa Mipasho,Khadija Koppa.

Waungwana;
 "Chaguo la Mswahili Leo"Mambo ya Pwani,Taarab/Rusha Roho!!Mmmmhh lakini usitoe Roho.Sina Maneno Meeengi Sikiliza mwenye mambo yao.
Mnasema ToT Kimeo Mbona Mnachezaaa?Pisha Njia pisha Njiaaa....Tarararar eehh Tararaa Wacha weeeeh...tehthetheteh

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Thursday, 9 August 2012

Mapishi ya Chicken and pinneaple salad with pink sauce na Mapishi ya Chicken with avocado Sauce- Recipe of (Swahili]!!

Waungwana "JIKONI LEO" SI Wengine ni "da'SOPHI" na "Tupike Pamojaa".
Leo Mapishi ni kuku kwa Nananasi NA Kuku kwa Parachichi.Mmmmmhhh Tamu Saaaana.

Hivi vitu tunavyo sana Nyumbani lakin jee wote tulikuwa tunajua jinsi ya Matumizi Tofauti  AU Ulikuwa unajua ni MaTunda tuu?

Una Swali au Maoni?Usisite kumuuliza. Kujua Zaidi usiache kutembelea.Tupike Pamoja.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daimaaaa!!!!!!

Tuesday, 7 August 2012

Ubatizo wa da'Charmaine Mungai;Ulifanyika St .Patrick Church Coventry!!!!!!!!

                    da'Farajika [mama mtoto] na da'Charmaine.
             wazazi wa mtoto na wazazi wa kiroho,Mtoto abatizwa!!!!
       Wazazi  na Charmaine Akishangaa duh jamani sinita unguaaa. 
Baba, Mama na Mwana
Wapendwa walioungana na Familia kwenye ibada ya Ubatizo
Zawadi ya Rosary kutoka kwa ma'Mkubwa Stellah
                             Ma'mkubwa Stellah na Charmaine
Da'Tecla[mama wa Ubatizo] da'Farajika[mama mazazi] na Binti yao.MUNGU Awabariki saaaana.
mama na baba wa Ubatizo na Familia ya Mungai
Familia
Kaka Richad na kaka Isaac, watoto kwa mbalii nao walikuwepo
da'Joyce,da'Farajika,da'Stellah ,da'Tecla na mtoto wao!!

Shangazi, da'Tracey,da'Farajika.


Mamazzzz Pamoja sana.
mama totoo na baba totoo na shangazi walikuwepo!!
                                dada Rose na da'Farajika Mbarikiwe sana!!!!
            dada Rose mwenyeweeee, yeye alikuwa anashughulika na misosi[Chakula] Mmmm tulishiba mamaaa,Asante sana.




  Mmmm hizi zinatosha, Jamani mweehh Shughuli za Waswahili kama una Diet usisogee!!!Mmmm Tamu saaana.

Waungwana J'Pili ya tarehe 05/08/12.Familia ya Mungai na da'FarajikaWalimbatiza mtoto wao Charmaine Mungai.

Ubatizo ulifanyika St.Patrick Catholic Church.Coventry U.K.
Baada ya hapo waliungana na Wageni wao Nyumbani kwao kwa Chakula cha Mchana.

Wazazi hao wa Charmaine Wanawashukuru sana Baba na Mama wa Ubatizo. Ndugu, Jamaa, Marafiki woote kwa kuungana nao kwenye siku hii muhimu ya mtoto wao.
Hawana cha kuwalipa bali Wanawaombea kila lililo jema.

Nasi; "Swahili NA Waswahli" Tunamtakia maisha mema na baraka mtoto Charmaine na Wazazi pia.
                                          "Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Monday, 6 August 2012

Jikoni leo;Somali Rice Cake (Mkate wa Maashara)na Cilantro Rice!!!!!

Waungwana "JIKONI LEO"Ngoja niwapeleke kwa jarani zetu Wasoli.
Vyakula vyao si vigeni saaana naona tunatofautiana majina na uandaaji labda.Waswahili wanasema MCHELE MMOJA..........."

Kujua Zaidi ingia.SomaliFoodBlog
Shukrani saana.
Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday, 5 August 2012

Nawatakia J'Pili yenye Furaha;Burudani- PARAPANDA VOICE CHOIR!!!!!!!

Taa ya Mwili ni Jicho;basi jicho lako likiwa safi,Mwili wako wote utakuwa na Nuru.
Lakini jicho lako likiwa bovu,Mwili wako wote utakuwa na giza.Basi ile Nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza;Si giza hilo!!!!!


Neno la Leo;Mathayo Mtakatifu:6:22-23.
MUNGU NA AZIDI  KUTUBARI SOOOTE!!!