(Lifestyle)Jamii,Tamaduni ,Matukio,Maisha ya Waswahili. Wapendao Kiswahili/Waswahili,Marafiki wa Swahili na Waswahili, Na Mengineyo ya Karibu, Yahitajikayo Kujuzwa Waswahili.Karibuni sana!!!!!!!
Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Waungwana;Filamu/Hadithi hizi na Nyingine ni zamuda.lakini mimi bado nazipenda na nipatapo muda huwa nazirudia... Yaani zina mafundisho na Mifano/Yaliyotokea/Yanayoendelea Kutokea katika Maisha ya kweli katika Jamii. Kuna lolote unakumbuka,kukugusa,kukutokea wewe au mtu wa karibu,Kusikia Jee? kuona Zaidi ingia;swahiliwood "Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.
Wapendwa;Natumaini J'Pili inaendelea vyema... Muwe na Amani,Baraka,Furaha na Tumaini... Upendano wa ndugu na udumu.[2]Msisahau kuwafadhili wageni;maana kwa njia hii wengine wamekaribisha malaika pasipo kujua. Neno La Leo:Waraka kwa Waebrania:13:1-6..Hata twathubutu kusema BWANA ndiye anisaidiaye,sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini? "Swahili NA Waswahili" Neema na iwe nanyi Wote.
Waungwana; Chaguo La Mswahili Leo..Mambo ya.. Boyz 2 Men.... Thank you in Advance, On Bended Knee, A song for MAMA ..................... na Nyinginee.... Mhhh palikuwa hapatoshi...Vipi wewe kuna lolote unakumbuka ukisikia/kuangalia nyimbo hizi...Wapi na Nini?
"Swahili Na Waswahili" Zilipendwa/Zinapendwa...J'Mosi Njema.
Waungwana, Walioko/Wanaoishi Nga'mbo Baadhi ya Maeneo Jua limeanzaa..watu watapungua uzito kwa Makoti..hahahhaha.. ... Vipi wewe hapo ulipo? haya niwakati wa kuzunguka zunguka Mjini , Nyama Choma, Kupeleka/Kucheza na Watoto Park na Mengine meengi..Raha tupu!!! Na Mitindo ndiyo hiyo Madukani...................
Waungwana;Mitindo mingi sasa naona inarudi, kama unavyoona Rasta kubwa sasa zimerudi tena... Jee kukumbuka zilizopendwa au Tumeishiwa Ubunifu? Mimi bado nazipenda sanaa tuu..Vipi wewe? Mitindo zaidi ingia;http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk "Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.
Fatuma Binti Baraka[Bi KIDUDE] Amefariki. Pole kwa Familia,Ndugu,Jamaa,Wasanii,Wapenzi na Wa TANZANIA Wote... Na Apumzike kwa Amani bi Kidude. "Swahili NA Waswahili" pamoja Daima.