WAZO LA LEO:,Kumbuka ipo siku maalumu, inayotambulikana kama ya siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16 June, sijui kama upo makini na siku hii, huenda kwako ni historia tu ya Mauaji ya Soweto…kwani unaishi kwenye kisiwa cha amani, huna shida…una kazi nzuri, gari..nk. Lakini kumbuka kuna hawa watoto wa mitaani, unawakumbuka?
Je siku ya mtoto kwako inakugusaje?
Je wewe kama mzazi, unahisije ukiwaona watoto wa mitaani, au ndio huko kusema, `hawa watoto wanaomba omba tu, hawaendi shule…’ hawa kwa mateso wanayoyapata hawana tofauti na wale watoto waliouwawa kikatili,…..wewe hutumii, silaha, lakini unatumia njia nyingine, isiyoonekana, ya kutokutimiza wajibu wako kama mzazi.
Kumbuka mateso wanayopata hawa watoto, kwanza kisaikolojia pale wanapoona wenzao wakiwa kwenye sare za shule, au wakipita na magari wakiepelekwa mashuleni. Lakini pia kuwa mateso ya afya zao, kwani wengine wanaishia majalalani kuokota yale mabaki ya vyakula mliyokula na kusaza. Huyu ni mtoto wako hata kama hukumzaa wewe, kumbukeni kila mtoto ana mzazi, na mzazi wake ni mimi na wewe.
Imeandikwa na emu-three wa Diary Yangu.
Zaidi ingia kwa ndugu wa mimi,Pia kwa Visa vya kusisimua na Mambo meengi;http://miram3.blogspot.co.uk/
Kwa Habari na mambo meengi ya watoto,wazazi/walezi nifuate huku;http://www.watotonajamii.blogspot.co.uk/