Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 20 July 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Marlaw, anakwambia -Bembeleza,Pii pii!!!!!






Waungwana; Natumaini wote wazima na Mnaendelea vyema na mambo yenu,vipi hali ya hewa huko mlipo?
 Hapa tulipo  leo jua linawaka vizuri...ni Raha na tuweza kunyoosha miguu/kutembea tembea na mambo mengine meengi ya nje yanawezekana.
Mnaofunga ndoa Leo tunawatakia Maisha mema  yenye Furaha,Amani,Upendo,Uvumilivu na mshikamano.Mnaotafuta Wachumba/wenza na mliokuwa kwenye maandalizi Mungu awasimamie.

Chaguo La Mswahili Leo Tumsikilize/angalie Marlaw.. mimi napenda  nyimbo zake hizi vipi wewe?
Maneno Mengi sina wewe pata Burudani na uwe na J'mosi njema.

"Swahili Na Waswahili" Pamoja sana.

Thursday, 18 July 2013

Jikoni Leo;Mkate wa Ufuta,Tambi za Kukaanga,Visheti,Viazi vya Karai.. Mmmhh Kazi kwenu Wapishi!!!!!














Waungwana "Jikoni Leo" kumejaa mapishi mbalimbali... kazi kwenu mkipika msiache kutushirikisha.. 
Hata wanaume mnaweza kupika wenyewe si kila siku mpikiwe tuu au kununua!!!

"Swahili na Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday, 17 July 2013

Nipo wapendwa Muwe na Ramadhani njema!!!!!

Waungwana, Ndugu,Jamaa,Marafiki na wapenzi wote.. Nashukuru kwa kunitafuta.. Nipo salama na Mungu ni Mwema...
Emu-3 [Ndugu wa mimi], da'Yasinta [kadala] na wote mlionitumia Ujumbe, Mnaondelea kupitia kibarazani Mbarikiwe sana na Tupo Pamoja.

Mliofunga nawatakia Ramadhani Njema...

Summer njema mliokuwa Nga'mbo.....

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday, 7 July 2013

Nawatakia J'Pili njema na yenye Furaha;Burudani -Sifa Voices,Enda Nasi na Nyingine!!!!!!










Wapendwa Muwe na J'Pili njema yenye Furaha,Amani,Rehema,Wema na Hekima....
N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole  wa hekima...

Neno La Leo:Waraka wa Yakobo;3:10-18..Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

"Swahili Na Waswahili"Mungu Atubariki Sote.

Saturday, 6 July 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Nyota Ndogo-Anakwambia,Kuna Watu Na Viatu na nyingine!!!!!









Waungwana; Leo tunaye "NYOTA NDOGO"  Ni ndogo inayo Nga'aa...
Mhhh...Rafiki yangu mpendwa...naja kwako siku nyingi wanipokea kwa uzuri siku zote,Wakati sina wanipa nitakachoo.....
Hivi majuzi nilipata kazi nzuri  nikaja kukueleza,Mtu wa kwanza nilifiria ni wewe rafiki yangu,Nilifurahi na kuruka na kutaja jina lake Mungu.........  Ohhh Kuna Watu Na Viatu DUNIANI!!!!!!
 Mhhh si Maneno yagu....... Endelea mwenyewe Mpenzi.....

Jee huyu  Rafiki utamuweka  kwenye Fungu Gani? 
Nyota Ndogo anakubamba/kupenda kazi zake?

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Friday, 5 July 2013

Wa-Afrika na Sherehe zao;Zambian Kitchen Party!!!!!!!








Waungwana;Wa-Afrika na Sherehe zao..hii Kitchen Party ya Wa Zambia na wanaume walikuwepo....
za Waswahili/Tanzania nyingi wanaume hawaingizwi. Nilisikia Waziri Mkuu  Mizengo Pinda aliingia kwenye K/party ya mtoto wake..jee alikosea?
Unafikiri ni kwa nini wanaume hawaingii? kuna sababu za msingi au wanaonewa na kukosa UHONDO? 
 Jee Kichen Party zina faida kwenye maisha ya ndoa au nikutaka kukusanya Zawadi ,Kupata Nafasi ya Wanawake Kujimwaga peke yao au Kuna siri zao?
 Jee kwanini Wanaume hawafanyiwi Kitchen Party/Party za Kufundwa? Au wao wanajua kila kitu kabla ya ndoa?

Swali la Kizushi;Kwanini Wanawake wanapenda Party za Peke yao kuliko Wanaume?

 Karibuni wote kwa Maoni/Ushauri,Tujifunze pamoja na Kuelimishana kwa Upendo

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Thursday, 4 July 2013

KUNDI JIPYA LA MUZIKI LAJA JIJINI, LITAKALO JULIKANA KWA JINA LA NDEGE WATATU


Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa.
Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel)na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.

Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.



"Swahili Na Waswahili" Wanawake na Maendeleo.