Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 8 June 2014

Natumaini JumaPili hii inaendelea Vyema;Burudani-Kinondoni Revival Choir,Ninakushukuru,Mtu wa Nne!!!!!!


Wapendwa Natumaini JumaPili inaendelea vyema....
Iwe yenye Imani,Tumaini,Kusifu/Kuabudu na Kushukuru....

Basi,mfalme Nebukadneza akashangaa,akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake,"Je,hatukuwafunga watu watatu na kuwatupa motoni?Nao wakamjibu mfalme,"Naam,mfalme!Ndiyo!"


Neno La Leo;Kitabu Cha Danieli;3:1-30

Nebukadneza anasimamisha sanamu;1-7
Marafiki wa Danieli;8-18
Wenzake Danieli wanahukumiwa;19-25

Vijana wanaachwa huru;26-30

Kisha akauliza,"Lakini  sasa mbona ninaona watu wanne wakitembeatembea humo motoni bila kufungwa na wala hawadhuriki, na mtu wa  nne anaonekana kama  mwana wa MUNGU?"



"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Wote.

Saturday, 7 June 2014

Mahojiano ya Dekula Kahanga "Vumbi" na Kwanza Production‏


Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Dekula Kahanga "Vumbi"
Vumbi ambaye anamiliki Dekula Band nchini Sweden

Amezungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa albamu yake mpya ya Shujaa Mamadou Ndala iliyozinduliwa Aprili 23 na 24 huko Sweden.

Pia, ametoa ushauri kwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaotaka kufanya muziki nchi za Scandinavia

KARIBU UUNGANE NASI

Kwa maoni na ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Sunday, 1 June 2014

Tumalizie JumaPili Hii Hivi;Burudani-Mbele "sala sikoyo " na Nyingine..!!!!!


Wapendwa tumalizie JumaPili hii kwa Hekima,Busara,Amani,Upendo na Furaha....

Mwenyezi-MUNGU akujibu uwapo taabuni;Jina la MUNGU wa Yakobo likulinde.

Neno La Leo;Zaburi;20:1-9
Wengine hujigamba kwa magari ya vita;
Wengine hujigamba kwa farasi wao.
Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-MUNGU,MUNGU wetu.
 





"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima

Wednesday, 28 May 2014

Amina's Baby Shower,Coventry,UK.!!!!!!

Mapokezi/Twasubiri Mgeni...

Michezo......
Mawilimatatu,Kutakiana kheri,kucheka/Furaha.....


Kucheza tulicheza....

Baadhi ya wanakamati ikiongozwa na Zayana[Mwasu]



Ilkuwa  Shughuli ndogo ya[Suprise] Baby Shower ya Amina[Emmy].
Iliandaliwa na Dada yake Zayana[Mwasu] mwenye nguo Nyekundu,Akishirikiana na Baadhi ya Ndugu,Jamaa na Marafiki.
Ilifanyika Coventry,UK.
Pia wageni mbalimbali kutoka Birmingham na Vitongoji vingine walijumuika pamoja.

Da'Zayana[Mwasu] Anawashukuru sana Wote kwa,Zawadi,kutoa Muda,Upendo na Mengineyo.
MUNGU awabariki na Kuwaongezea pale mlipopunguza na zaidii.
Anawapenda Wote.

Burudani/Muziki na kaka Paul....
Muongozaji wa Shughuli/MC;Da'Rachel siwa[Kachiki]
Picha na Mpiga Picha wetu wa Swahili Na Waswahili;Da'Neema[Nyanyile]



"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.