Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 29 June 2014

Tumalize JumaPili hii Kwa Amani Na Shukrani;Burudani,Solomon Mukubwa - Mungu Mwenye Nguvu,Ni Kwa Neema Na Rehema - Edson Mwasabwite. Na Siku Kama Ya Leo,Kaka Lusungu Ndondole Alizaliwa!!!

Wapendwa,Tumalizie/Tuendelee na JumaPili Hii kwa,Amani Shukrani,Furaha,Upendo na Matumaini.....
Basi, tuseme nini juu ya hayo?MUNGU akiwa upande wetu,ni nani aliye juu yetu?

Neno La Leo;Warumi:8:31-39
Wala yaliyo juu,Wala yaliyo chini,Wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika Kristo YESU BWANA wetu.

Siku Kama Ya Leo;Bibi Na Bwana I.Ndondole Walipata Mtoto wa Kiume.
Hongera Sana kwa Kutimiza Miaka Kadhaa, Mwl. Lusungu Ndondole
MUNGU azidi kukubariki kila iitwapo Leo,Uendelee kuwa Baraka kwa Wazazi,Familia na Jamii pia.
MUNGU akupe Miaka Mingi na Ufanikishe Ndoto zako.


Mhhhhh Ni Kwa Neema Na Rehema.......




"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Friday, 27 June 2014

JESCA KIPLAGAT ELECTRIFYS THE HALL WINNING FACE OF KENYA UK 2014


Jesca won because of her unique story. She was educated by charity, Educated in University using HELB loans and is now in UK on a sponsorship program. In her own words, she says she has received so much its time to give back. Jesca raised £560 for her charity of choice Kapchaselewes childrens home in Marakwet district.

Other contestants had a beautiful English ascent but Jesca proudly pulled a Kalenjin English accent and just really portrayed the pride of Kenya. During the talents, most contestants choose to sing and dance but Jesca chose to have a motivational speech as her talent, this was unique, moving and melting the hall away, she won the audiences hearts
"I must say this was a worthy course to have participated in. I had a wonderful experience, enjoyed myself and as well it has given me a platform to give back to my community. I have attended photo shoots, fundraisers, networking dinner among other initiatives that I have thoroughly enjoyed. I am honoured and humbled by this wonderful experience, It has inculcated in me a sense of nationalism-proud Kenyan and yes giving back to the community which is the ultimate thing that have really made it a worthy course and I promise to lead other youths in the national building exercise as The Face of Kenya UK 2014 BRAND AMBASSODOR".


FUNDS: £ 560 KAPSCHELEWES CHILDREN HOME MARAKWET.




Kwa picha zaidi;http://www.ukentv.com/faceofkenyauk.html
 Video; Africanacts


congratulations sister Janet, great job!

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Wednesday, 25 June 2014

Katika "HUYU NA YULE" ya NJE-NDANI wiki hii......‏


Photo Credits: Bongo Celebrity 
Katika NJE NDANI wiki hii, mbali na habari kutoka Afrika, utasikia mahojiano yangu na NURU THE LIGHT.

Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nami kutoka Stockholm Sweden

Kazungumza mengi mema

Jiunge nami, MUBELWA BANDIO Jumamosi (June 28) katika NJE NDANI ya Kwanza Production na Border Radio kuanzia saa sita mpaka saa nane mchana kwa saa za Marekani ya mashariki kupitia www.kwanzaproduction.com ama www.bordermediagroup.com


Monday, 23 June 2014

Mahojiano ya Kwanza Production na Haika Lawere. Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel‏




Haika Lawere akizungumza na wanawake kwenye tukio la wanawake waTanzania Washington DC
Photo Credits: IskaJojo Studios 
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Haika Lawere.

Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mbezi Garden Hotel ya Dar Es Salaam Tanzania.

Amezungumzia mengi kuhusu maisha yake, kazi yake, changamoto anazokumbana nazo katika kazi, ziara yake hapa Marekani na hata ushauri wake kwa wasikilizaji

Amezungumza mengi mema

Karibu uungane nasi



Kwa maoni ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail dot com

Sunday, 22 June 2014

Nawatakia JumaPili Njema na Yenye Amani;Burudani-Ambassador of Christ Choir Rwanda - Kaeni macho,Tuwe Na Upendo,Ng'ambo Ya Mto...!!!!!

Wapendwa Nawatakia JumaPili njema,Yenye,Amani,Upendo na Furaha..........
Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa;Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa;Achilieni, nanyi mtaachiliwa;Wapeni watu vitu,nanyi mtapewa;kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.Kwa kuwa kipimo kile kile  mpimacho ndicho mtakachopimiwa............

Neno La Leo;Luka Mtakatifu:6:1-49

43.Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya,Wala mti mbaya uzaao matunda mazuri;44.Kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake;Maana,katika miiba hawachumi tini,wala katika michongoma hawachumi zabibu.45.Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, Na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu;Kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Suala juu Ya Siku Ya Sabato;1-5
Mtu mwenye mkono Uliopooza;6-11
Yesu anateuwa Mitume kumi na wawili;12-16
Yesu anafundisha na Kuwaponya watu;17-19
Heri Na Ole;20-26
Kuwapenda Maadui;27-36
Juu Ya Kuwahukumu Wengine;37-42

Mtu Hujulikana kwa Matunda Yake;43-45
Wajenzi wa NamnaMbili;46-49








Mhhhhmmmm;Tuache Maneno Yesu yu karibu tena yukaribu sana siyo mbaliiii,Hatujui siku wala saa Ndugu....Lakini dalili zinaonyeshaaa....
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Tuesday, 17 June 2014

Mahojiano ya moja kwa moja na msanii Anna Mwalagho kuhusu Tamasha lijalo‏


Anna Mwalagho.
Photo Credits Anna Mwalagho Facebook page
 Karibu katika mahojiano mafupi na ya moja kwa moja kati ya msanii Anna Mwalagho na Kwanza Production kwenye kipindi cha NJE-NDANI Jumamosi Juni 14, 2014

Amezungumzia tamasha kubwa linaloendelea ambalo atatumbuiza pamoja na kikundi chake kwa siku tatu

Tamasha hilo linaandaliwa kwa ushirikiano wa watu wa Oman na maktaba ya sanaa za waAfrika hapa Washington DC
Karibu usikilize