Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 22 April 2015

BALOZI MPYA WA ANGOLA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.



 Mhe, balozi wa Angola Agostinho Tavares akipokelewa na afisa wa ubalozi  Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi .
 Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwa na furaha baada ya mgeni wake kufika ofisini .
 Mhe balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Angola Agostinho Tavares.
 Mhe Balozi wa Angola nchini Marekani Agostinho Tavares akiweka sahihi  kitabu cha wageni.
 Mhe balozi wa Angola chini Marekani Agostinho Tavares akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha .
Mhe balozi Libarata Mulamula na balozi wa Angola nchini marekani Agostinho Tavares pamoja na afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme walipokua wakibadilishana mawazo.
               PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI

RAIS MSTAAFU MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI AWASILI JIJINI WASHINGTON DC.


 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiambata na mama Sitti Mwinyi wawasili jijini Washington DC tayari kwa tamasha maalum la Chama cha Ukuzaji wa RaisiKiswahili Duniani.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa utawala Lilly Munanka wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, mara alipowasili hotelini.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi Edward Taji.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme.
  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Emmanuel Swere.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi John Anbiah
     Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiwa ameongozana na mama Sitti   Mwinyi na baadhi ya msafara wake katika hoteli waliyofikia.
                                  PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI

BALOZI WA RWANDA NCHINI MAREKANI MHE. MATHILDA MUKANTABANA ATEMBELEAAFISI ZA UMOJA WA AFRIKA WASHINGTON, DC.




Mhe Balozi wa Rwanda Profesa Mathilda Mukantabana akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa AU Mhe. Amina Salum Ali alipotembelea ofisi za Umoja wa Afrika uliopo Washington, DC nchini Marekani .Balozi Profesa Mathilda anachukua uongozi wa mikutano wa mabalozi wa Afrika katika kipindi cha mwezi April hadi July 2015 akiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.

Monday, 20 April 2015

Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) Pt I


Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout
Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo
Nani alimfanya ashawishike na fani hii?
Maisha yake kimahusiano je?
Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake?
KARIBU

Sunday, 19 April 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA WASABATO WAISHIO NCHINI MAREKANI




Mchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.
 Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.


Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake  Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.  


Nchungaji Herry Mhando akifanya mamombi maalum kabla ya kumkaribisha mchungaji Wilbert Nfubhusa kutoa mahubiri,


Mshereheshaji Magoma akifafanua jambo


Mhahubiri yakiendelea
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Tuendelee na Jumapi hii kwa Kusifu Na Kuabu;Burudani-KGC WORSHIP SERVICE...!!!

Wapendwa;Muendelee na Jumapili hii Vyema,Baraka,Amani, Furaha vitawale juu yenu.
Utukufu Tumrudishie BWANA.
1 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema, “Tazama, namtuma mjumbe wangu anitangulie kunitayarishia njia. Bwana mnayemtafuta atalijia hekalu lake ghafla. Mjumbe mnayemtazamia kwa hamu kubwa atakuja na kutangaza agano langu.” 2 Lakini ni nani atakayestahimili siku hiyo atakapokuja? Ni nani atakayesimama kustahimili atakapotokea? Yeye ni kama moto mkali usafishao chuma; ni kama sabuni ya dobi.
 3Yeye atakuja kuhukumu kama mtu asafishaye na kutakasa fedha. Atawasafisha wazawa wa Lawi, kama mtu afuavyo dhahabu au fedha, mpaka wamtolee Mwenyezi-Mungu tambiko zinazokubalika. 4Hivyo, tambiko za watu wa Yuda na wa Yerusalemu zitampendeza Mwenyezi-Mungu kama za watu wa kale; kama katika miaka ya zamani. 5Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Kisha nitawakaribia ili kuwahukumu. Sitasita kutoa ushahidi dhidi ya wachawi, wazinzi, watoa ushahidi wa uongo, wanaowapunja waajiriwa, wanaowadhulumu wageni na wale wasionicha mimi.













WELCOME TO KENYAN GLOBAL CHURCH
Sunday Worship services are as follows:
Prayer Service: 10:30am. Please Use Glass Door Entrance for this service. 
Main Service: 11:30am
Children Service: 11:30am
Teens Service: 11:30am
WORSHIP VENUE: 1900 DAVENPORT ROAD, TORONTO, ON M6N 1B7, CANADA
www.kgcministry.org
Shukrani;REV ANN MUHIA

6“Mimi ni Mwenyezi-Mungu, mimi sibadiliki. Lakini nyinyi, nyinyi wazawa wa Yakobo hamjatoweka bado. 7Tangu wakati wa wazee wenu, mmezidharau kanuni zangu wala hamkuzifuata. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu nasema: Nirudieni, nami nitawageukieni. Lakini nyinyi mnauliza, ‘Tutakurudia namna gani?’ Nami nawaulizeni, 8Je, ni sawa mtu kumdanganya Mungu? La! Lakini nyinyi mnanidanganya! Walakini nyinyi mwauliza: ‘Tunakudanganya kwa namna gani?’ Naam! Mnanidanganya kuhusu zaka na tambiko zenu

Neno La Leo:Malaki 3:1-18

Zaka na tambiko
 9Nyinyi na taifa lenu lote mmelaaniwa kwa sababu ya kunidanganya. 10 Leteni ghalani mwangu zaka yote, ili nyumbani mwangu kuwe na chakula cha kutosha. Kisha mwaweza kunijaribu. Nijaribuni namna hiyo nanyi mtaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele. 11Wadudu waharibifu nitawakemea wasiyaharibu tena mazao yenu. Mizabibu yenu mashambani haitaacha kuzaa matunda. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema. 12Ndipo mataifa yote yatawaita nyinyi watu waliobarikiwa, maana nchi yenu itakuwa nchi ya furaha. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu nimesema.” 13Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Maneno yenu yamekuwa mzigo kwangu. Hata hivyo mnasema, ‘Tumesema nini dhidi yako?’ 14Nyinyi mmesema, ‘Kumtumikia Mungu hakuna faida. Kuna faida gani kuyatii maagizo ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, au kujaribu kumwonesha kuwa tumekosa mbele yake kwa kutembea kama watu wanaoomboleza? 15Tuonavyo sisi, ni kwamba, wenye kiburi ndio wenye furaha daima. Watu waovu, licha ya kustawi, hata wanapomjaribu Mungu, hawapati adhabu.’” 16Ndipo watu wanaomcha Mwenyezi-Mungu walipozungumza wao kwa wao, naye Mwenyezi-Mungu akasikia mazungumzo yao. Mbele yake kikawekwa kitabu ambamo iliandikwa kumbukumbu ya wale wanaomcha na kumheshimu. 17Iliandikwa hivi: Mwenyezi-Mungu asema: “Hao watakuwa watu wangu. Watakuwa urithi wangu maalumu siku ile nitakapoinuka kufanya ninalokusudia. Sitawadhuru kama vile baba asivyomdhuru mwanawe anayemtumikia. 18Hapo ndipo mtakapotambua tena tofauti iliyopo kati ya waadilifu na waovu; naam, kati ya mtu anayemtumikia Mungu na asiyemtumikia.”

Bible Society of Tanzania
"Swahili Na Waswahili"Nawapenda Wote.

Katika kipindi cha "HUYU NA YULE" kesho (Jumatatu), usikose kujua UNDANI wa maisha ya Linda‏


NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Kesho Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda


Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho