Monday, 25 May 2015
Sunday, 24 May 2015
Nimatumaini Yangu Jumapili Inaendelea Vyema;Burudani-Turudi miaka ya Nyuma kidogo,[Mchanganyiko]LULU,Mimi yesu,Samson na Delila,Mapambazuko,Nishike Mkono,Kwa Viumbe Vyote.........
Neno La Leo;2 Timotheo 2:1-26.
20Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: Vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida. 21Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema. 22Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani, pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi. 23Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi. 24Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu, 25ambaye ni mpole anapowaonya wapinzani wake, kwani huenda Mungu akawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujua ukweli. 26Hapo fahamu zao zitawarudia tena, wakaponyoka katika mtego wa Ibilisi aliyewanasa na kuwafanya wayatii matakwa yake.
Bible Society of Tanzania
Askari mwaminifu wa Yesu Kristo
8Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri, 9na ambayo kwa sababu yake mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo. 10Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele. 11Usemi huu ni wa kweli:
“Ikiwa tulikufa pamoja naye,
tutaishi pia pamoja naye.
12Tukiendelea kuvumilia,
tutatawala pia pamoja naye.
Tukimkana,
naye pia atatukana.
13Tukikosa kuwa waaminifu,
yeye hubaki mwaminifu daima,
maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”
Mfanyakazi aliyekubaliwa na Mungu
14Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia. 15Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.16Jiepushe na majadiliano yasiyofaa na ya kipumbavu; kwani hayo huzidi kuwatenga watu mbali na Mungu.17Mafundisho ya aina hiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongoni mwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo na Fileto. 18Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika. 19Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
Bible Society of Tanzania
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.
TAMASHA LA GOSPEL CONCERT & CONFERENCE MEMORIAL WEEKEND, COLUMBUS, OH.
Mwimbaji mahili wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Upendo Nkone
akiimba moja ya nyimbo zilizowainua watu vitin kwenye tamasha la
Gospel linaloendelea mjini Columbus tangia siku ya Ijumaa May 22 na
kuhitimishwa leo siku ya Jumapili May 24. Tamasha lilihudhuriwa na
watu kutoka mataifa mbalimbali wengine wakiwa wamesafiri kutoka
majimbo ya mbali na Ohio.
akiimba moja ya nyimbo zilizowainua watu vitin kwenye tamasha la
Gospel linaloendelea mjini Columbus tangia siku ya Ijumaa May 22 na
kuhitimishwa leo siku ya Jumapili May 24. Tamasha lilihudhuriwa na
watu kutoka mataifa mbalimbali wengine wakiwa wamesafiri kutoka
majimbo ya mbali na Ohio.
Mwimbaji kutoka Jamhuri ya Congo akienda sambamba na mwimbaji
mahili wa nyimbo za injili Upendo Nkone kwenye tamasha la Gospel
lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 6230 Busch Blvd suit 260,
Columbus, OH 43229.
mahili wa nyimbo za injili Upendo Nkone kwenye tamasha la Gospel
lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 6230 Busch Blvd suit 260,
Columbus, OH 43229.
Mchungaji Donis Nkone ambaye ni kaka ya mwimbaji Upendo Nkone
akitoa ukifanya utambulisho kwa bendi iliyokuwa ikitumbuiza nyimbo za
injili kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23,
2015 mjini Columbus.
akitoa ukifanya utambulisho kwa bendi iliyokuwa ikitumbuiza nyimbo za
injili kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23,
2015 mjini Columbus.
Mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone wakifuatilia tamasha la
Gospel
Gospel
Bendi ikienelea kupiga moja ya nyiimbo za mwimbaji wa nyimbo za
injili kutoka Tanzania Upendo Nkone.
injili kutoka Tanzania Upendo Nkone.
Bendi ikitumbuiza.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
Friday, 22 May 2015
Siku Kama Ya Leo da'Tracey-Sarah Alizaliwa..!!!!!!!
"Rachel/Isaac/Sandra-Neema/Tracey-Sarah"Tunawapenda tunawapenda wote.
Wednesday, 20 May 2015
Monday, 18 May 2015
Sunday, 17 May 2015
Natumaini Jumapili Inaendelea Vyema;Iwe yenye Baraka Na Fanaka,Burudani- Jamaican Gospel Mix....
Natumaini Jumapili inaendelea Vyema,Iwe yenye Hekima,Busara,Heri,Fanaka,Utii,Uaminifu, Imani na Matumaini...Utukufu tumrudishie Mungu...!!! |
1Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu,
bali kwa moyo wako uzishike amri zangu.
2Maana yatakupa wingi wa siku,
maisha marefu na fanaka kwa wingi.
3Utii na uaminifu visitengane nawe.
Vifunge shingoni mwako;
viandike moyoni mwako.
Neno La Leo;Methali 3:1-35
Mawaidha kwa vijana
Mawaidha kwa vijana
4 Hivyo utakubalika na kusifika,
mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.
5Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote,
wala usitegemee akili zako mwenyewe.
6Umtambue Mungu katika kila ufanyalo,
naye atazinyosha njia zako.
7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;
mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.
8Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako,
na kiburudisho mifupani mwako.
9Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako,
na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10Hapo ghala zako zitajaa nafaka,
na mapipa yako yatafurika divai mpya.
11 Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu,
wala usiudhike kwa maonyo yake;
12 maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye,
kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.
13Heri mtu anayegundua hekima,
mtu yule anayepata ufahamu.
14Hekima ni bora kuliko fedha,
ina faida kuliko dhahabu.
15Hekima ina thamani kuliko johari,
hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.
16Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu;
kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.
17Njia zake ni za kupendeza,
zote zaelekea kwenye amani.
18Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;
wana heri wote wanaoshikamana naye.
19Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,
kwa akili aliziimarisha mbingu.
20Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,
na mawingu yakadondosha umande.
24Ukiketi hutakuwa na hofu;
ukilala utapata usingizi mtamu.
25Usiogope juu ya tishio la ghafla,
wala shambulio kutoka kwa waovu,
26Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;
atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.
27Usimnyime mtu anayehitaji msaada,
ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.
28Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho,
hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.
29Usipange maovu dhidi ya jirani yako,
anayeishi karibu nawe bila wasiwasi.
30Usigombane na mtu bila sababu
ikiwa hajakudhuru kwa lolote.
31Usimwonee wivu mtu mkatili,
wala usiige mwenendo wake.
32Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;
lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
33Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu,
lakini huyabariki makao ya waadilifu.
34 Yeye huwadharau wenye dharau,
lakini huwafadhili wanyenyekevu.
35Wenye hekima watavuna heshima,
lakini wapumbavu watapata fedheha.
Bible Society of Tanzania
"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)