Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 24 June 2015

Niambie Live Show EP7


 Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.

Na mgeni mwalikwa ni Dotto Malongo

Ni Niambie Live....

KARIBU

Saturday, 20 June 2015

Jikoni Leo na da'Miriam Rose Kinunda;Mapishi-Sweet Potatoes Futari, Tanzanian Spicy Porridge[Uji wa Pilipii Manga]


Waungwana; Nawatakia Ndugu,Jamaa na Mrafiki ,Waislam wote  Mfungo mwema.

Jikoni Leo na da'Miriam Rose mapishi haya yatawasaidia sana kwa wakati huu wa mfungo..
Kupata Mapishi yake zaidi, Nunua Kitabu chake cha mapishi,Hakika hautajutia.. 

Mimi ninacho changu na pia kinasaidia sana watoto wangu wanapotaka kujifunza zaidi kupika mapishi ya nyumbani nami ninapokuwa sina muda.
Kila mtu huwa anapenda kutambulisha kitu cha kwao..sasa wanangu wanapoalika rafiki zao ambao si Waswahili/hawafahamu radha ya chakula chetu ni rahisi sana kuandaa hata kama sipo au nipo na mambo mengine..!!!


Karibu tujifunze zaidi....





Zaidi;Taste of Tanzania


Kama unamapishi kwa mwezi huu na siku za kawaida na unapenda kushirikisha na wengine,Usisite kuwasiliana nasi/kututumia kwa Email;rasca@hotmail.co.uk.


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday, 17 June 2015

Niambie Live Show.....Father's Day Special




Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki hii mada ni SIKU YA KINABABA DUNIANI.

Na mgeni mwalikwa ni Mayor Mlima

Ni Niambie Live....

KARIBU

Sunday, 14 June 2015

Wapendwa; Jumapili iendelee kuwa Njema Kwenu,Burudani-Fanuel Sedekia...


Wapendwa/Waungwana Natumaini wote hamjambo na Mungu yu pamoja nanyi.
Na Mnaendelea vyema na Jumapili hii...
Tupo pamoja sana japo wakati mwingine muda unakuwa hautoshi wa kugawa mambo,Lakini Mungu wetu ni mwema sana.
Anazidi kututendea,Kutupigania,Kutulinda,Kutubariki na Kutupa Ushindi.!!
Kwani yeye atosha..Majaribu/Mitihani ni Mapito tuu..Lakini yeye Hashindwi na Jambo.
Basi mpendwa usife moyo kwa unayoyapitia yupo muweza wa yote,Usibebe hiyo mizigo si yako bwana...
Nyanyuka,Simama na uwe na nguvu/Imani Bwana wa Bwana yupo..!!!!


1Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.2Euodia na Suntike, nawaombeni na kuwasihi mpatane kama ndugu katika Bwana. 3Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.

Neno La Leo;Wafilipi 4;1-23
Maagizo mbalimbaliShukrani kwa zawadi za Wafilipi

4Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! 5Upole wenu ujulikane kwa watu wote. Bwana yu karibu. 6Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. 7Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.
8Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima. 9Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

10Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.11Sisemi hivyo sasa kwa sababu nahitaji kitu; maana nimejifunza kuridhika na vitu nilivyo navyo. 12Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa. 13Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu. 14Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu.
15Nyinyi Wafilipi mwafahamu wenyewe kwamba mwanzoni mwa kuhubiri Habari Njema, nilipokuwa naondoka Makedonia, nyinyi peke yenu ndio kanisa lililonisaidia; nyinyi peke yenu ndio mlioshirikiana nami katika kupokea na kuwapa wengine mahitaji. 16Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja. 17Sio kwamba napenda tu kupokea zawadi; ninachotaka ni faida iongezwe katika hazina yenu. 18Basi, nimekwisha pokea vitu vyote mlivyonipa, tena ni zaidi kuliko nilivyohitaji. Nina kila kitu kwa vile sasa Epafrodito amekwisha niletea zawadi zenu. Zawadi hizi ni kama tambiko yenye harufu nzuri, sadaka inayokubaliwa na kumpendeza Mungu. 19Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote. 20Utukufu uwe kwa Mungu wetu na Baba yetu, milele na milele. Amina.



Salamu za mwisho
21Nawasalimu watu wote wa Mungu walio wake Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami hapa wanawasalimuni.22Watu wote wa Mungu hapa, na hasa wale walio katika ikulu ya mfalme, wanawasalimuni.
23Nawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.