Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 3 August 2015

Mkutano wa Injili Washington DC [Aug 14 - 16 2015]


Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries linapenda kuwaalika katika siku tatu za mkutano wa uamsho utakaofanyika hapa Washington DC.

Ni kati ya Agosti 14-16 2015




Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ama Masanja Mkandamizaji alipohudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya Jumapili 07/07/2013 katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES

Sunday, 2 August 2015

Muendelee Vyema na Jumapili Hii;Namshukuru Sana Mungu kwa mema Mengi,Burudani-Kinondoni Revival Choir Ninakushukuru na ....

Namshukuru sana Mungu baba muumba wa vyote,
Kwa mema yote aliyonitendea na ayonitendea..
Nimrudishie nini Mungu wangu?
Nasema Asante Mungu...
Jana tarehe 01/08 ilikuwa Siku ya kumbukumbu yangu ya Mimi kuja katika Dunia hii/Kuzaliwa.

Mungu yu mwema Sana!!!
Asante kwa Wazazi/Walezi kwa yote mliyoweza kufanikisha
Kwa nafasi yenu ili mimi niendelee.
Asante kwa Mume wangu kwa Nafasi yako pia.
Asante Watoto wangu, Dada/kaka,Ma Wifi/Ma Shemeji,Ndugu,Jamaa naMarafiki zangu pia kwa Nafasi zenu.
Asante kwa wote mlionitumia ujumbe,Maombi,Dua/Sala na mengine mengi..
Mungu azidi kuwabariki Sana katika yote.

Asante pia kwa wewe unayepita hapa...


"Sasa baba naja kwako najimimina maisha yangu niguseeeee!!!!!!!"""
Pendo Lako Calvary...!!!!!
Lanivutaaaa nipate Kuabuduuuu...!!!
Neno La Leo;Waebrania:11:1-40
Imani






"Swahili na Waswahili" Mbarikiwe wote.

Saturday, 1 August 2015

WATANZANIA CALIFORNIA WAMUAGA BALOZI LIBERATA MULAMULA


 Watanzania California wakiongozwa na Balozi wa Heshima Mhe. Ahmed Issa walijumuika pamoja siku ya Ijumaa na kumuaga Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na kurudi nyumbani kwenda kulitumikia taifa kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Watanzania wa California wakipiga picha ya pamoja na Mhe. Balozi Libarata Mulamula (wapili toka kushoto) siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomuaga rasmi.
 Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi yake Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme mara tu baada ya kukabidhiwa na Watanzania California siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomualika rasmi kwa ajili ya kumuaga.
 Balozi Liberata Mulamula akicheza na kuburudika kwenye moja ya nyimbo zilizopigwa kwenye tafrija hiyo.
 Balozi Liberata akipiga makofi
Moja wa kikundi maarufu cha ngomma ya asili kikitoa burudani

Wednesday, 29 July 2015

Mazungumzo na mtangazaji Rose Chitallah kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU


Mubelwa Bandio na Rose Chitallah studioni
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania

Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na mtangazaji Rose Chitallah

Karibu

Mahojiano na Balozi Amina Salum Ali kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU


Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifafanua jambo ndani ya Kilimanjaro Studio
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania

Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali

Karibu

Sunday, 26 July 2015

Mahojiano na Charles Magali ndani ya Washington DMV


Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media
Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini
Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo
Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi

Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio

Wednesday, 15 July 2015

Siku kama ya Leo da'Sandra-Neema Alizaliwa....!!!


Siku miezi miaka sasa.. Ni Furaha isiyo na kikomo kwetu kwa zawadi hii kubwa Mungu aliyotupatia
Mtoto kwa wazazi hakui atabaki kuwa mtoto tuu mpaka mwisho...

Hongera Sana da'Sandra-Neema(Dide)kwa kuongezeka mwaka mwingine..
Mungu azidi kukubariki,kukutendea,Kukulinda,Kukuongoza.
Akupe miaka Mingi ufanikishe ndoto Zako na Kazi aliyokutuma hapa Duniani...
Uendelee kuwa Baraka,Faraja kwetu kama wazazi na kwa Ndugu,Jamaa,Marafiki na Jamii pia.

Tunamshukuru Sana Mungu katika yote aliyokutendea na Anayoendelea kukutendea.
Mkono wake tumeuona/tunaendelea kuuona juu yako.
Tumejifunza mengi mno na tunaendelea kujifunza.

Shukrani kwa wazazi wetu kwa muongozo na mengine mengi..
Shukrani kwa ndugu/jamaa na Marafiki wote kwa kushirikiana nasi katika Maombi,Sala/Dua na malezi kwa ujumla..
Tunaamini mtoto halelewi na wazazi tuu..
Mungu azidi kuwabariki na kuwaongezea zaidi ya mnavyojitoa kwetu.

Mungu yu mwema sana..
Tunawapenda wote...
Happy birthday binti yetu Mpendwa Sandra-Neema(Didee)
Isaac family.