Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 23 April 2016

FRANK LYIMO APEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA MAREKANI, ASHINDA MR. VIRGINIA INTERNATIONAL UNIVERSITY




Frank Lyimo (mwenye vazi la kimasai) mmoja ya Watanzania wanaosoma katika chuo cha kimataifa cha Virginia, ameshinda kwenye shindano la vivazi lililofanyika siku ya Alhamisi April 21, 2016. Vazi lililompa taji hilo ni vazi la kimasai.
Frank Lyimo akiwa katika picha ya pamoja na miss District of Columbia mara tu alipovikwa taji na kuwa Mr. Virginia International University.
Frank Lyimo akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzake wa Kitanzania wakipeperusha bendera ya Tanzania chuoni hapo katika kusherehekea ushindi.
Frank Lyimo (kati) akiwa na washiriki wengine.


Monday, 18 April 2016

MWILI WA MAREHEMU HENRY KIHERILE WAAGWA HOUSTON, TEXAS


Jioni ya jana Jumamosi (16/04) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada Takatifu katika kanisa la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. Mwili wa marehemu Henry unatarajiwa kusafirishwa jioni ya leo kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.

Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake
Gari lililobeba mwili wa Henry likiingia kanisani


Wachungaji wakiwa nje ya kanisa kabla ya ibada


Jeneza lililobeba mwili wa Henry likiingizwa kanisani
Dada  Lulu  ( mdogo wa Marehemu Henry ) akimuaga kwa uchungu kaka yake
Mr. & Mrs. Tenende ( Baba na Mama mkubwa wa marehemu ) wakiwa kanisani
Waombolezaji wakilia kwa uchungu
Rafiki wa Henry kutoka Cameroon
Waombolezaji