Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 27 April 2016

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete na Mama Salma Kikwete wakaribishwa nyumbani kwa Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi


Wiki iliyopita Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC, alimkaribisha Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake kwa chakula cha jioni na kujumuika pamoja na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao walikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia (World Bank Group) na International Monetary Fund (IMF) tarehe 12 - 17 Aprili 2016. Kwenye ziara yake jijini Washington, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Afya (World Health Congress) na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani (International Commission on Financing Global Education Opportunity).


DSC_0447.JPG
Mhe. Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wao, Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Mama Marystella Masilingi


Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akibadiliashana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile (kushoto), Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu nyumbani kwa Mhe. Balozi , Tanzania House Bethesda, MD.









Tuesday, 26 April 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu. Mjadala wa DICOTA Convention 2016 April 25


Kongamano la kila mwaka la waTanzania waishio Marekani (DICOTA) litafanyika mwishoni mwa juma hili jijini Dallas Texas.
Katika kipindi cha Jukwaa Langu jumatatu hii, tulipata fursa ya kuzungumza na viongozi waandamizi wa DICOTA, Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini Lunda Asmani na Mwenyekiti wa DICOTA Dr Ndaga Mwakabuta.

Pia wachangiaji mbalimbali

KARIBU


Sunday, 24 April 2016

CLOUDS MEDIA GROUP IKIONGOZWA NA MD JOE KUSAGA YATEMBELEA NYUMBANI KWA BALOZI MANONGI, NEW YORK


Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tovako Manongi akimkaribisha Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga nyumbani kwake siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi huyo alitembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakzi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika jijini Las Vegas. Picha na Vijimambo New York.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akiwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn, Joseph Kusaga (hayupo pichani) siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwn. Joseph Kusaga akitambulisha timu yake kwa Mhe. Balozi Tuvako Manongi.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn. Joseph Kusaga.
Mkurugenzi wa Clouds Medea Group, Bwn. Joseph Kusaga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Timu nzima ya Clouds Media Group iliyohudhuria Tamasha la Radio nchini Marekani ikiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Kutoka kushoto ni Saleh Mohammed, Daudu Lembuya, Dj Venture, Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Mkurugenzi Joseph Kusaga, Mama Manongi, Dj Peter Moe na Jackson Joseph.
Kushoto ni Brightus Titus, Getrude Clement na NY Ebra wakiwa katika picha ya pamoja.

Siku hiyo pia lilifanyika kusanyiko la maDJ mbalimbali wa zamani waishio nchini Marekani ambao walikutana kwa nyama choma na kubadilishana mawazo. MaDj hawa ni wachache miongoni mwa wengi wanaounda kundi la Tanzania Djs Worldwide ambalo limeanza miezi mitatu iliyopita, na mpaka sasa lina wanachama wapatao 70. Kusanyiko lao la kwanza lilifanyika Escape One March 24 (lirejee hapa)