Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 21 September 2016

Kipindi cha Reggae Time Pride Fm Sept 17 2016.....Mahojiano na Innocent Galinoma


Karibu katika kipindi cha REGGAE TIME ya Pride Fm Mtwara Tanzania.

Na leo, ni mazungumzo yangu na Innocent Galinoma ambaye alikuwa mkarimu sana kufika Kilimanjaro Studios kwa mahojiano.



Ni kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, mbili kamili kwa Marekani Mashariki

Jiunge nasi kupitia 87.8 Fm kwa mikoa ya kusini, ama www.878pridefm.com ama kupitia TuneIn, bofya tun.in/seTTx.

Tuesday, 13 September 2016

Kipindi Cha Jukwaa Langu Sep 12 2016....Tetemeko Bukoba


Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo, tulizungumzia janga kuu la Tetemeko la ardhi nchini Tanzania
Wadau
Baraka Galiatano wa BukobaWadau Blog na Erick Kimasha walijiunga nasi
kwa njia ya Skype kutoka Tanzania kutupa taswira ya nini kilitokea, vipi
kilipokelewa na maendeleo tangu Sept 10 na hali ilivyo hivi sasa mjini
humo.
Pia tuliungana na mmoja wa wanaharakati ambao wameanzisha mfuko maalum kuchangia wahanga wa tetemeko hilo Agnetta .



Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093

Karibuni

Tuesday, 30 August 2016

Kipindi cha JUKWAA LANGU Aug 29 2016 (Pt 1)...Demokrasia Tanzania


Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA ya sasa na ile tuitakayo.

Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania na ukuaji wa Demokrasia ya nchi yetu.

KARIBU

Mahojiano na Prof Julius Nyang'oro katika kipindi cha JUKWAA LANGU


Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.

Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.

Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.

Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na
mwanasheria

KARIBU




Thursday, 4 August 2016

Wawakilishi wa Tanzania katika YALI 2016 wazungumza kuhusu kongamano lao Washington DC

Stanley Magesa (mjasiriamali) akifafanua jambo ndani ya studio kuhusu YALI 2016


Aug 3, 2016 tulipata fursa ya kutembelewa na kuhojiana na baadhi ya
Watanzania wanaowakilisha kwenye mkutano wa Mandela Washington
Fellowship - Young African Leaders Initiative (YALI) 2016 waliomaliza
mkutano wao hapa Washington DC

Walikuwa wakarimu sana kujiunga nasi Studio na kuzungumza nasi kuhusu mambo mbalimbali

Karibu uwasikilize



Heri Emmanuel (kati kutoka Mwanza) akieleza jambo huku Tusekile Mwakalundwa ( Mhadhiri na Mwanasheria kutoka Arusha) akisikiliza kwa makini. Kulia ni Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Vijimambo Radio
Baadhi ya wawakilishi wa YALI 2016 kutoka Tanzania, wajasiriamali Stanyey Magesa (Mwanza), Simon Malugu (Morogoro) na Lusajo Mwaisaka (Dar) wakiwa kwenye mahojiano Kilimanjaro Studio
Mshiriki wa YALI 2016 Heri Emmanuel (Mwanza) kulia akaifafanua jambo huku akisikilizwa na mshiriki mwenzake ambaye pia ni Mhadhiri na Mwanasheria Tusekile Mwakalundwa (Arusha) na mjasiriamali na Lusajo Mwaisaka (kutoka Dar)



Sunday, 24 July 2016

Muendelee na Jumapili nyema;Burudani-Bado Sijafika,Kina Cha Upendo Wako,Twaokolewa kwa Neema - Kijitonyama choir



Wapendwa/Waungwa natumaini Jumapili inaendelea vyema..
Basi muendelee kuwa na Amani,Furaha,Baraka na msipungukiwe na
kila lililojema Mungu awe nanyi daima.






Kuumbwa ulimwengu
1Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. 2Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.
3Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. 4Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza,5mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
   



    Neno La Leo;Mwanzo 1:1-31



6Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” 7Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo. 8Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili.





9Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo. 10Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.







11Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. 12Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. 13Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.
14Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka, 15na ingae angani na kuiangazia dunia.” Ikawa hivyo. 16Basi, Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; ule mkubwa utawale mchana na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17Mungu akaiweka mianga hiyo angani iiangazie dunia, 18ipate kutawala mchana na usiku, na kuutenga mwanga na giza. Mungu akaona kuwa ni vyema. 19Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya nne.


20Mungu akasema, “Maji na yatoe makundi ya viumbe hai na ndege waruke angani.” 21Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema.22Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni, muongezeke, muyajaze maji ya bahari; nao ndege waongezeke katika nchi.” 23Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tano.



24Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo. 25Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema.
26Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” 27 Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. 28Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”


29Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. 30Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo. 31Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya sita.


Biblia Habari Njema


"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday, 17 July 2016

Natumai Jumapili inaishia vyema;Burudani,Bwana Wa Majeshi na Nimesogea.by Paul S.Mwangosina -Sandra-Neema birthday, Shukrani na utukufu kwa Mungu wetu...


Wapendwa/Waungwana natumaini mlikuwa/mnaendelea vyema na Jumapili hii..
Mungu aendelee kuwatunza na kuwalinda, Kiroho na kimwili,Muingiapo na mtokapo,Vilaji na vinywaji, Msipungukiwe na Amani ya moyo,Baraka na Furaha kila iitwapo leo...

Kwetu kuanzia ijumaa mpaka leo tulikuwa na wakati mzuri sana,
15/7 kila mwaka tunaungana na binti yetu mpendwa kwa kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
Ni zawadi iliyo njema  kwetu kutoka kwa Mungu,Tunamshukuru sana Mungu kwa baraka hii
kwenye maisha yetu,"Sandra-Neema" alikuwa baraka tangu alipofika mikononi mwetu na anaendelea kuwa baraka kwetu,Miaka 18 ni mingi na kwa wengine ni dada mkubwa lakini kwetu sisis wazazi kila siku utakuwa mtoto kwetu.

Mungu aendelee kukulinda,kukuongoza katika masomo na maisha yako yote yawe mikononi mwake
kila hatua unayopitia umtangulize Mungu iwe mchana iwe usiku,liwe giza iwe Nuru,kunena na kutenda,Uzidi kukuwa kiroho na kimwili, Uendelee kuwa baraka kwetu kama wazazi, walezi, ndugu,Jamaa , marafiki na jamii pia.Mungu azidi kukuinua katika yote yaliyo mema.

Shukrani;Viongozi wetu katika imani,washarika wenzetu na wote tunaomba pamoja
bila kuchoka katika yote.Mungu aendelee kuwabariki sana kwa kuwa pamoja nasi.
Shukrani;kwa Ndugu,Jamaa,marafiki zetu wote kwa Zawadi na  mchongo wenu kwenye makuzi ya binti yetu na yote,
tunaamini mtoto hulelewa na wengi si wazazi tuu,Mungu awabariki sana na tunawathamini mno.

Ngoja niishie hapa kwa leo Mungu yu mwema sana na tunauona mkono wa Bwana.

"Happy birthday da'Sandra-Neema".



1Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uhai maangavu kama kioo, yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo. 2Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uhai unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa. 3Hapana kitu chochote kilicholaaniwa kitakachokuwa katika mji huo.
Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwa katika mji huo, na watumishi wake watamwabudu. 4Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao. 5Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.



Neno La Leo;Ufunuo 22: 1-21


Kuja kwa Yesu
6Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
7“Sikiliza! Naja upesi. Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabii yaliyo katika kitabu hiki.”
8Mimi Yohane, niliyaona na kusikia mambo haya. Nilipokwisha sikia na kuona, nikajitupa chini mbele ya miguu ya huyo malaika aliyenionesha mambo hayo, nikataka kumwabudu. 9Lakini yeye akaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kama wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoyatii maagizo yaliyomo katika kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”10Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia. 11Kwa sasa anayetenda mabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidi kutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu.”
12  “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. 13Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.”
14Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.15Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.
16“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”
17Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo.

Hatima
18Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: Mtu yeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katika kitabu hiki.19Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki. 20Naye anayetoa ushahidi wake juu ya mambo haya asema: “Kweli naja upesi.”
Amina. Njoo Bwana Yesu!
21Nawatakieni nyote neema ya Bwana Yesu. Amina.

Biblia Habari Njema 


"Swahili Na Waswahili"Muwe na wakati Mwema.