Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima na kuwa tayari kwa majukumu yetu.
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah,Uabudiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu sana,Matendo yako ni ya ajabu,hakuna lililogumu mbele zako Mungu wetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mungu mwenye nguvu,Mungu wa walio hai
Mume wa Wajane,Baba wa Yatima,Muweza wa yote,Alfa na Omega..
neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!!
Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungu kwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima ya binadamu. Nilipokuwa kwenu niliamua kutojua chochote kile isipokuwa tu kumjua Yesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa. Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi. Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho. Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu.
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Jeohovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Baba wa Mbinguni tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu,nguvu za mpinga Kristo zishindwe kwa jina lililo kuu kuliko majina yote jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Mungu wetu tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah utufunike kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana wetu yesu Kristo
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...
Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea. Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu. Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu. Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona, wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”
Jehovah tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Mungu wetu nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji...
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa zetu,baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Mungu wetu tunaomba ukatamalaki na kutuatamia Jehovah tunaomba ukatubariki tuiingiapo/tutokapo Yahweh ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/tumia Mungu wetu tukawe salama moyoni Baba wa Mbinguni tukanene yaliyoyako Yahweh tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Mungu wetu tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu,Jehovah ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ijulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni....
Ukatupe neema ya hekima,busara,utuwema,fadhili,huruma na upendo ukadumu kati yetu...
Yahweh ukatuokoe na makwazo,unafiki,fitina,choyo,ugombanishi,kijisifu/kujikweza na yote yanayokwenda kinyume nawe...
Ukatufanye barua njema Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisa ya Mungu. Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. Sasa, sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tumepokea Roho atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu. Basi, sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho. Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada wa Roho. Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubainisha ubora wa kila kitu, naye mwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine. Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.
Baba wa Mbinguni tazama wenye shida/tabu,wagonjwa,wenye njaa,walio kata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka,wali katika vifungo vya yule mwovu,walio magereza pasipo na hatia,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,walioanguka/potea,wafiwa ukawe mfariji wao Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu Yahweh ukawaponye kimwili na kiroho pia,Baba wa Mbinguni tunaomba ukawape chakula na ukabariki mashamba/vyanzo vyao
Mungu wetu ukawavushe salama na ukawaokoe,Baba wa Mbinguni ukawasamehe na ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako nazo ziwaweke huru,Amani ikatawale katika maisha yao,Nuru ikaangaze katika maisha yao,Yahweh tunaomba ukasikie kulia kwao Mungu wetu ukawafute machozi ya watoto wako wanokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu ukapokee sala/maombi yetu Baba wa Mbinguni ukatende sawasawa na mapenzi yako...
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina....!!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Nawapenda. |