|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana.. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "MUHUBIRI" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki...
Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"Wimbo Ulio Bora"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!!
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu sisi wenyewe. Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena,
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
nyinyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
1 Taz 1Fal 4:32 Wimbo wa Solomoni1:1 wa Solomoni: Au Kwa heshima ya Solomoni, au juu ya Solomoni. ulio bora kuliko nyimbo zote.
Shairi la kwanza
Bibi arusi
2Heri midomo yako inibusu,
maana pendo lako ni bora kuliko divai.
3Manukato yako yanukia vizuri,
na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa.
Kwa hiyo wanawake hukupenda!
4Nichukue, twende zetu haraka,
mfalme amenileta katika chumba chake.
Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako,
tutasifu mapenzi yako kuliko divai.
Wanawake wana haki kukupenda!
5Enyi wanawake wa Yerusalemu,
mimi ni mweusi na ninapendeza,
kama mahema ya Kedari,
kama mapazia ya Solomoni.
6Msinishangae kwa sababu ni mweusi,
maana jua limenichoma.
Ndugu zangu walinikasirikia,
wakanifanya mlinzi wa mashamba ya mizabibu.
Lakini sikutunza shamba langu la mizabibu.
7Hebu niambie ee wangu wa moyo,
utawalisha wapi kondoo wako?
Ni wapi watakapopumzikia adhuhuri?
Kwa nini mimi nikutafute
kati ya makundi ya wenzako?1:7 Kwa nini … wenzako: Kiebrania si dhahiri.
Bwana arusi
8Ewe upendezaye kuliko wanawake wote;
kama hujui, fanya hivi:
Zifuate nyayo za kondoo;
basi, walishe mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.
9Wewe ee mpenzi wangu,
nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao.
10Mashavu yako yavutia kwa vipuli,
na shingo yako kwa mikufu ya johari.
11Lakini tutakufanyizia mikufu ya dhahabu,
iliyopambwa barabara kwa fedha.
Bibi arusi
12Mfalme alipokuwa kwenye kochi lake,
marashi yangu ya nardo yalisambaa kila mahali.
13Mpenzi wangu ni kama mfuko wa manemane kwangu,
kati ya matiti yangu.
14Mpenzi wangu ni kama maua ya hina yachanuayo,
kwenye mashamba ya mizabibu huko Engedi.
Bwana arusi
15Hakika u mzuri, ee mpenzi wangu,
hakika u mzuri!
Macho yako ni kama ya hua!
Bibi arusi
16Hakika u mzuri ewe nikupendaye,
u mzuri kweli!
Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu;
17mierezi itakuwa nguzo za nyumba yetu,
na miberoshi itakuwa dari yake.
Wimbo Ulio Bora1;1-17
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.