|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki/nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Nilipitia karibu na shamba la mvivu; shamba la mzabibu la mtu mpumbavu. Nilishangaa kuona limemea miiba, magugu yamefunika eneo lake lote, na ukuta wake wa mawe umebomoka.
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....
Nilitazama, nikawaza, mwishowe nikapata funzo: Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo! Kunja mikono yako tu upumzike!
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako wakasimamie Neno lako nalo likawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye.... Nawapenda.
|
Mungu awalaumu watu wake
1Msikilizeni Mwenyezi-Mungu,
enyi Waisraeli.
Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii.
“Hamna tena uaminifu wala wema nchini;
hamna anayemjua Mungu katika nchi hii.
2Kuapa, uongo, mauaji, wizi na uzinzi huzuka humo.
Umwagaji damu hufuatana mfululizo.
3Kwa hiyo, nchi yote ni kame,
wakazi wake wote wanaangamia
pamoja na wanyama wa porini na ndege;
hata samaki wa baharini wanaangamizwa.
Mungu anawashutumu makuhani
4“Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe;
maana mimi nakushutumu wewe kuhani.
5Wewe utajikwaa mchana,
naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku.
Nitamwangamiza mama yako Israeli.
6Watu wangu wameangamia kwa kutonijua,
maana wewe kuhani umekataa mafundisho.
Nimekukataa kuwa kuhani wangu.
Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako,
nami pia nitawasahau watoto wako.
7“Kadiri makuhani walivyoongezeka,
ndivyo wote walivyozidi kuniasi.
Basi, nitaigeuza fahari yao kuwa aibu.
8Wanajishibisha kwa sadaka za watu wangu wenye dhambi.
Wana hamu sana ya kuwaona wametenda dhambi.
9Lakini yatakayowapata watu yatawapata makuhani;
nitawaadhibu kwa sababu ya mwenendo wao,
nitawalipiza matendo yao wenyewe.
10Watakula, lakini hawatashiba;
watazini, lakini hawatapata watoto,
kwa sababu wameniacha mimi Mwenyezi-Mungu,
na kufuata miungu mingine.
Mungu alaani ibada za miungu
11“Divai mpya na ya zamani
huondoa maarifa.
12Watu wangu huomba shauri kutoka kwa mti;
kijiti chao cha ramli ndicho kinachowapa kauli.
Nia ya kufanya uzinzi imewapotosha;
wamefanya uzinzi kwa kufuata miungu mingine,
wakaniacha mimi Mungu wao.
13Wanatambikia kwenye vilele vya milima;
naam, wanatoa tambiko vilimani,
chini ya mialoni, migude na mikwaju,
maana kivuli chao ni kizuri.
“Kwa hiyo binti zenu hufanya uzinzi,
na bibiarusi wenu hufanya uasherati.
14Lakini sitawaadhibu binti zenu wanapofanya uzinzi,
wala bibi arusi wenu wanapofanya uasherati,
maana, wanaume wenyewe ndio wanaofuatana na wazinzi,
na kutambikia pamoja nao katika ibada za uzinzi.
Watu hawa watovu wa akili hakika wataangamia!
15“Ama kweli nyinyi Waisraeli ni wazinzi!
Lakini, msiwafanye watu wa Yuda wawe na hatia!
Msiende mahali patakatifu huko Gilgali,
wala msiende kule Beth-aveni.4:15 Beth-aveni: Neno kwa neno: Nyumba ya ukaidi; labda mahali pa Betheli, yaani “Nyumba ya Mungu”.
Wala msiape mkisema,
‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo!’”
16Waisraeli ni wakaidi kama punda.
Kwa nini basi Mungu ashughulike kuwachunga,
kama kondoo kwenye malisho mapana?
17“Watu wa Efraimu4:17 Efraimu: Utawala wa kaskazini au Israeli. wamejifunga na sanamu.
Haya! Waache waendelee tu!
18Kama vile genge la walevi,
wanajitosa wenyewe katika uzinzi;
wanapendelea aibu kuliko heshima yao.
19Basi, kimbunga kitawapeperusha,
na watayaonea aibu matambiko yao kwa miungu ya uongo.
Hosea4;1-19
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe