|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo... Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Mwenyezi-Mungu amewaagiza watu wa Israeli watenge kidari hicho na mguu huo wa mnyama wa sadaka zao za amani, wampe kuhani Aroni na wazawa wake, maana sehemu hiyo wamewekewa hao makuhani milele.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Hiyo ndiyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe kutoka katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, tangu siku walipotawazwa kuwa makuhani wa Mwenyezi-Mungu. Walipowekwa wakfu kwa kupakwa mafuta, Mwenyezi-Mungu aliamuru Waisraeli wawape sehemu hiyo ya sadaka; hiyo itakuwa daima haki yao.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe... Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako siku zote za maisha yetu... Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Basi, hayo ndiyo maagizo kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya kuondoa dhambi, sadaka ya kuondoa hatia, kuhusu kuwekwa wakfu na kuhusu sadaka ya amani. Mwenyezi-Mungu alimpa Mose amri hizi mlimani Sinai siku ile alipowaamuru Waisraeli wamletee sadaka zao, kule jangwani Sinai.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru... Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele... Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake... Nawapenda. |
1Anayeonywa mara nyingi akawa mkaidi,
ataangamia ghafla asipone tena.
2Waadilifu wakitawala watu hufurahi,
lakini waovu wakitawala watu hulalamika.
3Apendaye hekima humfurahisha baba yake;
lakini aandamanaye na malaya hufuja mali yake.
4Mfalme akitumia haki huipatia nchi uthabiti,
lakini akipenda hongo taifa huangamia.
5Mwenye kumbembeleza jirani yake,
anatega mtego wa kujinasa mwenyewe.
6Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake,
lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi.
7Mwadilifu anajua haki za maskini,
lakini mtu mwovu hajui mambo hayo.
8Wenye dharau huutia vurugu mji mzima,
lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu.
9Mwenye hekima akibishana na mpumbavu,
mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia.
10Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia,
lakini watu wema huyalinda maisha yake.
11Mpumbavu huonesha hasira yake wazi,
lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza.
12Mtawala akisikiliza mambo ya uongo,
maofisa wake wote watakuwa waovu.
13Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja:
Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu.
14Mfalme anayewaamua maskini kwa haki,
atauona utawala wake umeimarika milele.
15Adhabu na maonyo huleta hekima,
lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.
16Waovu wakitawala maovu huongezeka,
lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao.
17Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi;
yeye ataufurahisha moyo wako.
18Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu;
heri mtu yule anayeshika sheria.
19Mtumwa haonyeki kwa maneno matupu,
maana ingawa anayaelewa yeye hatayatii.
20Wamwona mtu apayukaye bila kufikiri?
Mtu mpumbavu ni afadhali kuliko yeye.
21Ambembelezaye mtumwa wake tangu utoto,
mwishowe mtumwa huyo atamrithi.29:21 mwishowe … atamrithi: Au Mwishowe mtumwa huyo atakataa kumtii.
22Mwenye ghadhabu huchochea ugomvi,
mtu wa hasira husababisha makosa mengi.
23Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe,
lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima.
24Anayeshirikiana na mwizi anajidhuru mwenyewe;
husikia laana ya aliyeonewa bila kusema neno.
25Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe,
lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama.
26Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala,
hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu.
27Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu,
naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu.
Methali29;1-27
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment