Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana? Asante Baba Mungu kwa Neema/Rehema,Umetupa kibali cha kuiona siku hii tena..Tunakushukuru na Kukusifu na Kulitukuza Jina lako linaloyashinda yote,Wewe Mwenye-Enzi,Muumba mbingu na dunia,Mungu uponyaye,Mungu utoshaye, Mwenye huruma,Husamehe,Hufariji,Mshauri wa Ajabu,Mwenye Nguvu,na Muweza wa yote tunakuja mbele zako Baba ukatuongoze kwa kila jambo,Tuingiapo/Tutokapo,Vilaji/Vinywaji,Kunena/Kutenda,Kazi,Biashara,Elimu na yote tusiyoyataja Baba wewe unatujua zaidi,Ukatupe sawasawa na Mapenzi yako Mfalme wa Amani uendelee kutawala... Ukawaponye wanaopitia Magumu/Majaribu mbalimbali,Wagonjwa,Wafiwa,Wenye Shida/Tabu..Wakakutane nawe Baba.. Tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini na kushukuru .. Amina...!! Muwe na wakati mzuri. |